Heshima kwenu wana JF,
Kuna hii tatizo la viganja vya miguu kuwaka moto na haswa tatizo linakuwa kubwa nyakati za usiku wakati wa kulala mpaka unashindwa kupata usingizi kwa wakati.
Tatizo lenyewe ilianza hivi; Mwaka 2007 wakati naenda kuanza kidato cha tano nilianza kuhisi miguu kuwa moto wakati nikiwa kwa gari na safari ilikuwa ndefu sana ilibidi nivue viatu ili nipate ahueni. Hiyo ilikuwa safari ya kutoka babato to tanga.
Hali hii iliendelea kwa muda wote huo nikiwa tanga na hasa nikiwa class either tunafundishwa au najisomea huwa navua viatu na soksi ili viganja viguse sakafu ndo angalau vinapoa
Sasa tatizo lilianza kuwa kubwa 2009 nikiwa morogoro na kila nikienda hospital inaonekana uelewa wa madaktari ni mdogo kuhusu tatizo langu.
Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu bila muafaka wa tatizo nilijaribu kuwashirikisha baadhi ya ndugu zangu ndo wakaniambia kuwa utakuwa umefanyiwa mambo ya kishirikina na nilielekezwa kwenda kwa mtumishi moja wa mungu hapo DAR.
Mwaka 2010 nilienda kwa mtumishi huyu anayepatina kivule na akaniombea akasema niwekewa vitu vingi sana mwilin na wachawi na akatoa midude mingi ya ajabu na nikaacha sadaka ya20,000/- angalau nilipata nafuu nikarudi moro kuendelea na masomo. Baada ya muda tatizo lilirudi ikabidi nirudi tena kwenye huduma kama mbili na nilikuwa na acha kiasi hicho hicho cha sadaka.
Sasa nikiwa kazin mwaka 2014 niliamua kwenda DAR maana tatizo ndo limeongezeka nilipofika niliambiwa sadaka ya huduma ya maombezi imepanda mpaka 60,000/-Tsh na mazaga mengine ya maombi pia lazima ninunue.
Na wakati wa maombi huwa nabaki na boksa ninapakwa mafuta na kunyiziwa mapafyum ndo anaanza kuomba na kunitoa hayo madude.
Sasa wakuu nikisharudi maskani tatizo lile lile huku nikiwa nimetumia garama kubwa ya nauli Babati to Dar and Dar to Babat, garama za logde, sadaka, chakula lakin hakuna mafanikio. Sasa wadau naombeni msaada kwa wenye ufaham wa tatizo hii.
NAWASILISHA