Tatizo la mkopo wa kuongeza kwenye biashara yangu

Tatizo la mkopo wa kuongeza kwenye biashara yangu

Lomaa lolusa

Member
Joined
May 15, 2017
Posts
30
Reaction score
45
Mimi nimefanikiwa kujenga nyumba ya kupangisha eneo la chuo cha mipango Dodoma, ina vyumba kumi na tayari watu wanaishii.

Nina shida ya mkopo mil 20 kwa ajili ya kuchimba kisima na kujenga uzio nimeenda bank wanataka cash flow ambayo mimi sina.

Msaada tafadhari.
 
Connection mkuu
Ongea na watu vzr Kama dhamana IPO ela inapatikana tu
 
Masharti ni mengi mno kweny benki aisee! Yaani ndio maana watu wanaenda kwenye kaushaDamu... serikali na viongozi wanasema ukiwa na Hati tuu inatosha kuwa kama dhamani benki ili upate mkopo. Ukienda kwenye uhalisia sasa benki wenyewe yaani ni usumbufu mtupuu
 
Tatizo bank lengo lao sio kuuza nyumba yako, wanataka uhakika kwa wewe kulipa pesa,record zako za mikopo ,cash flow nk
 
Mimi nimefanikiwa kujenga nyumba ya kupangisha eneo la chuo cha mipango Dodoma, ina vyumba kumi na tayari watu wanaishii.

Nina shida ya mkopo mil 20 kwa ajili ya kuchimba kisima na kujenga uzio nimeenda bank wanataka cash flow ambayo mimi sina.

Msaada tafadhari.
Ninakushauri endelea kukomaa mwenyewe. Benki wako sahihi 100% kukunyima mkopo kama huna cashflow. Wanaokuambia connection wanakudanganya kwasababu hiyo hela ukipewa ukaitumbukiza kwenye huo ujenzi huku ukiwa huna wapangaji walioanza kulipa kodi utasumbuka. Kama watakupa Grace period itakusaidia.
 
Jibane ujenge mwenyew ukishaendekeza mikopo mingi huwa ni majuto tu
Mkopo ni kitanzi ni pingu ni jela unajifunga mwenyewe [emoji1787]

Shida ni kwamba kundunduliza inaweza mchukua miaka kutimiza lengo kitu ambacho mkopo unamaliza fasta within months.

Changua ni lako
 
Hivi cashflow unaipataje au ni kitu gan unapeleka bank kuonyesha hiyo cashflow???
 
Tafuta muajiriwa uoe/ awe mchepuko akukopee kwa niaba yako; ingawa utarejesha zaidi kutegemeana na miaka ya rejesho.
 
Back
Top Bottom