Tatizo la mtu kuongea peke yake: Fahamu visababishi na namna ya kutatua shida hii

Tatizo la mtu kuongea peke yake: Fahamu visababishi na namna ya kutatua shida hii

Salam sana!

Bila kupoteza muda. Nina miaka around 30 now naona life inaniumiza sana. Najua hii imechangiwa sana na swala la mahusiano (love love love). Nahisi kama nimekosea hatua muhimu sana katika maisha yangu.. Kuwaza hilo imenifanya niwe nafikiria hata sumu! Imekuwa badala ya Kuwaza namna ya kufanya maendeleo, nachukua mda mreeef sana kulala baada ya kutoka job.

Imefika mahali namfukuza rafiki yangu wa kike toka toka hapa kaa mwenyewe huko
japo siko nae yaan hiyo toka toka hapa nakuwa nazungumza mwenyewe! mshana jr amewahi leta thread hapa Wanaoongea peke yao wanazidi kuongezeka kweli kwenye hiyo listi nipo. Nipeni msaada nini nifanye ili mawazo hayo ya kujitoa uhai yafe, ama KUZUNGUMZA MWENYEWE ikome, kwa sababu imefika mahali nawaza then nafika mahali natoa neno kwa sauti toka hapaa.

Halafu nikigundua mtu kaskia naunganisha kawimbo kakuzugia ili ajue nilikuwa naimba.
Tafadhali nategemea sana hekima yako, naomba usinitukane mtu wa Mungu.
 
Tayari wenzeko wameshakupata..wahi haraka ongea na wakubwa usaidiwe una hali mbaya sana.
 
ESPIRIT,

Kaka pole sana;

kwanza naomba nikupe pole, lakini pia nikushauri kuwa hari uliyofikia ni mbaya; hiyo inaitwa depression, kaka sikia hii, usipende kukaa peke yako ukishatoka kazini; kama wewe ni mkristu nakushauri ukitoka job nenda kanisani, kila siku jioni kuanzia saa 11:30 kuna kuwaga na ratiba za ibada, semina na maombi kwenye makanisa mbalimbali.

Lakini kama wewe ni muislamu hakikisha unaenda msikitini kusikiliza mawaidha, nasisitiza usikae pekee yako mahala kwa muda mrefu, kunaweza tokea roho chafu ikakupelekea kujinyonga au kunywa sumu; na pia wewe kama sio mfuasi wa dini yeyte pliz nenda sehemu zenye mkusanyiko wa watu kadhaa ambao mnaweza kubadilishana mawazo.

lakini katika yote; nia njema itakayokuokoa ni nafsi yako kuamua kumove on kwa njia yeyote ile

nakutakia mafanikio mema
 
ESPIRIT,
Mkuu you need a wife. Miaka 30 si muafaka kuwa peke yako. Ila utulie upate mwanamke anayefaa. Utaongea naye badala ya kuongea peke yako. Nahisi unampenda huyo rafiki yako na imekuchanganya kiasi ndiyo maana unaongea peke yako. Solution oa.
 
ESPIRIT,
Hahaha, hapo kwenye red umechekesha sana, mbona hiyo kitu haiko kwako tu mkuu! Mwanzo wa bandiko lako hili kuna jibu la swali lako na hata wewe umejua kwamba matatizo ndio chanzo, basi shughulikia matatizo hayo upate muhafaka ili nafsi yako iridhike.
 
pole, huyo mtu/watu wamefanya wamefanya kazi yakufanya ujione huna thamani, wewe sio kitu, ni mjinga, hufai, huwezi kupendwa na yoyote dunia hii.

HAPANA
wewe ni wa thamani sana, wapo watu wanaokupenda,kukujali, kukuthamini kuliko hao walokuumiza na nafasi hiyo waliikosa kwa wewe kuwa na hao vichomi

hebu tulia, shukuru kuwajua ndivyo walivyo mapema wamekuepusha na uzee mbaya jikubali
dunia / nchi hii ina watu mamilioni kukataliwa/kuumizwa na mtu 1 usipate uchizi wanaokupenda niwengi zaidi ya huyo.

Rudisha furaha yako hebu jiamini uwe unasali mara kwa mara kumshukuru Mungu na soon atakuonyesha mtu atakayekupenda mpaka ushangae. Furaha yako ndo kila kitu, wasamehe uepuke kujibebesha mzigo wao wa dhambi

Wewe ni wa dhamani amka tena usifadhaike utajiumiza na dunia imejaa options kibao
 
Kuna haja ya kufungua kliniki ya magonjwa ya akili na hisia huko mitaani. Hii ni fursa ambayo kuna wana JF wanaweza kufaidika nayo. mshana jr, waweza ukafanya part time service kwenye eneo hili
 
Pia jitulize uoe huu ni mda muafaka wa wewe kuwa na mwenza mtafarijiana, pia mweleze wazi tatizo lako ili aweze kukuvumilia nakukutibu kwa faraja baadae utakuwa poa, maana lazima utakuwa mtu wa hasira sana inabidi mtu akiwa nawe akuchukulie ulivyo baadae utapona
 
Pole mkuu.
Nasikitika hujaweka wazi kuwa hyo love imekufanya nini na imekuaje kuaje!!

Anyway, kwakua umepata ujasiri wa kupost hapa ni vema sasa ukachukua ushauri wa watu mbali mbali ukaufanyia kazi. Ushauri wangu kwako Mimi ni huu.

Huenda ulipenda usipopendwa na hatimae umeumizwa, kama umri wako ni around 30 naamini huenda ulikua bado hujamuoa huyo unaemfukuza hewani. Chakufanya, badili gia tafuta mwanamke wa aina yako na kua makini. Tambua ktk maisha kuna wanawake wa aina mbili pindi uwapo kijana, kuna mabinti kwa ajili ya shown off na sex, half kuna wife materials. Sasa ukikosea ukaoa haya mashankupe ya shown off utajuta.

Kingine, unapotaka kujiua tanguliza maswali haya mbele kabla ya kubugia dawa zako au kujining'iniza..

1. Hivi kweli lengo lako la kuhangaika kusoma miaka yote target ilikua ni kupata mwanamke au kupata maisha mazuri?

2. Hivi kweli Leo hii Ashura amekua bora kuliko wazazi na ndugu zako kiasi kwamba unywe sumu uwaache na wakose msaada wako kisa Ashura?

3. Hivi Ashura ndiye mwanamke pekee chini ya jua na huezi penda tena?

4. Hivi nikijiua vipi Ashura nae atakufa au atabaki duniani kuendlea kula bata na kuisaidia family yake ?

Nb. Wewe ni mdogo sana, half kwa umri wako bado sana, kumbuka wakat unahaso shule target yako kuu ilikua nini huenda ikakurudsha kwenye reli.
Pole.
 
accused,
Jamani! msifanye mchezo na kumpenda na kumwamini mtu asilimia mia 2, halafu akutende, its the hardest thing ever! Huyu jamaa mi namwelewa anavyohisi, ni ngumu, ngumu kupita maelezo, na itamchukua muda mrefu kuwa okay, could be over a year, Hamna neno linaelewekaga kirahisi rahisi yani kila kitu kinakuwa ovyooo, laiti watu wangekuwa wana value mapenzi ya kweli ya walio real.
 
Jamani samahani naomba nionyeshwe kitufe cha PM nimshauri jamaa kwa PM. I am a Professional Counselor.
Kifupi usikate tamaa maisha yana mambo mengi sana ya furaha na amini nakuambia yupo utakaemopata na kufurahia maisha. Hujaongea kama unafanya kazi/ biashara. Concentrate huko.

Ni kweli miaka 30 ni muhimu kuwa na mke lakini usikurupuke bado wewe ni kijana maisha ya sasa hivi watoto wawili wanatosha si kama zamani.

Concentrate na kinachokuletea Kipato kwa sasa, sala na kujichanganya. Kizuri umejitambua hivyo ni rahisi kujitibu. Aidha unaweza mtafuta mtu unayemuamini sana ( ndugu/ rafiki) ukamueleza
 
Comment bora hapa jamii forum kwa mwezi huu ni hii.. Mungu akubariki


Asante Mkuuu

the bible says on 1 Corinthians 9:19-23

"For though I am free from all, I have made myself a servant to all, that I might win more of them. To the Jews I became as a Jew, in order to win Jews. To those under the law I became as one under the law (though not being myself under the law) that I might win those under the law.

To those outside the law I became as one outside the law (not being outside the law of God but under the law of Christ) that I might win those outside the law. To the weak I became weak, that I might win the weak. I have become all things to all people, that by all means I might save some. I do it all for the sake of the gospel, that I may share with them in its blessings".

nimejitahidi kutekeleza wajibu wangu kama binadamu wa kawaida kama tulivyoagizwa na Muumba wetu

From Glory to Glory
 
Back
Top Bottom