Tatizo la Nguruwe kula kuku

Tatizo la Nguruwe kula kuku

zabron k

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2015
Posts
943
Reaction score
1,107
Habari ya leo.

Nina mradi wa ufugaji nguruwe mix kuku wa kienyeji Kijijini kwetu Songea. Tatizo lililopo ni Nguruwe kukamata na kula kuku wanaoingia bandani kuokota punje za mahindi. Sio chini ya kuku 10 wamefanywa kitoweo.

Naomba msaada changamoto hii wafugaji mnatatuaje?
 
Habar ya leo

Nina mradi wa ufugaji nguruwe mix kuku wa kienyeji Kijijini kwetu Songea. Tatizo lililopo ni Nguruwe kukamata na kula kuku wanaoingia bandani kuokota punje za mahindi. Sio chini ya kuku 10 wamefanywa kitoweo

Naomba msaada changamoto hii wafugaji mnatatuaje?
Hao nguruwe konk master hawataki chakula chao kiliwe na kuku,
Tenganisha mabanda weka wavu around mabanda ya nguruwe kama kuku ni wakienyeji na huwafungii
 
Kuna uwezekano umemzoesha hilo mkuu.
Nguruwe hali kuku kama wewe hujamzoesha kula hiko kitu.
Labda Kama haujawahi kufunga nguruwe mkuu,huyu mnyama hata akikuta mtoto mchanga nje usipokua makini anapita nae. Yeye anakula chochote kinachompitia mbele akiwa na njaa, ingawa si nguruwe wote hufanya hivi

Tulikuwa tunafunga nguruwe tunawapa pumba na vyakula vingine,siku tukichelewa kuwapa chakula wanakula tena zile pumba walizokunya
 
Nguruwe wanakula chochote kilichopo mbele yao, hasa wakiwa na njaa, tena mwingne akiwa mkali usimsogelee ni hataree. Kaka angu aliwahi jeruhiwa na nguruwe wetu wakati yupo ndani ya zizi anasafisha

Nguruwe kula kuku hasa pale na wao wanapodowea pumba zao, au laah mfugaji kumzoesha nguruwe kula kuku.

All in all Ufugaji wa Nguruwe ni mtaji mkubwaa, Songea home kwetu kumenogaaaa!
 
Sikuwa nalijuwa hili, fuatilia kwa makini wanyama karibu wote tunaokula binadamu ni wale wanaokula majani, majani ni nature.
Aaaah sasa hilo ni suala jingine Mr, na unataka kutoka nje ya mada. tusiende huko.
 
Habar ya leo

Nina mradi wa ufugaji nguruwe mix kuku wa kienyeji Kijijini kwetu Songea. Tatizo lililopo ni Nguruwe kukamata na kula kuku wanaoingia bandani kuokota punje za mahindi. Sio chini ya kuku 10 wamefanywa kitoweo

Naomba msaada changamoto hii wafugaji mnatatuaje?
Wewe umesema kuku wanafuata mahindi, si uache kuweka mahindi huko kwa nguruwe? Pia, uimarisha mabanda ya mifugo yako ili kuku wasiweze kuingia huko kwa 'kitimoto'.

Kwa kifupi, tatizo hapa ni mfugaji kutokufuata ufugaji bora na wala sio kitimoto!
 
Back
Top Bottom