Tatizo la Tanzania sio Katiba Mpya bali utii wa Katiba iliyopo

Na Mwalimu Nyerere alikuwa 'specific' kabisa: kwamba Katiba iliyopo inampa madaraka makubwa kiongozi wa juu kabisa. Kama kiongozi huyo atakuwa asiye na busara, basi ataitumia akiba hiyo hiyo kuvuruga nchi.

Kwa hiyo, hili pekee, angalau ni mwanzo, sehemu moja ya kutaka kuibadili katiba hiyo; hata kama tunakiri kwamba anaweza kuwepo kiongozi asiyeheshimu chochote kilichomo kwenye katiba.
 
Reactions: BAK
Kuanguka mkuu sio kosa,kosa ni kubaki pale pale ulipo anguka.

Tayali mwanga upo kwamba katiba sio rafiki sasa kitendo Cha kuendelea kuikumbatia hapo ndo utata unakuja hasa watawala wetu
 
Reactions: BAK
Sasa umeandika kitu gani.?

Watu hawaitii katiba iliyopo kwakua inawalinda. Laiti kama wasingelindwa, basi wangeitii maana baada ya kumaliza muda wao, wangepelekwa mahakamani kujibu mashtaka yao.....


Siungani na wanaodai katiba mpya kwa sasa.

Mimi nina maoni kuhusu suala la katiba mpya. Wangefanya mkakati wa kuhakikisha % kubwa ya watanzania wanaifahamu na kuielewa katiba iliyopo alafu waonyeshe mapungufu iliyonayo ndipo sasa tuanze kuidai hiyo mpya kwa kuainisha makosa ya iliyopo.
Mbali na hilo, watanzania ni wagumu sana kuungana kudai kitu ambacho hata hawajui ni kitu gani
 
Kwani kipindi kamati ya jaji warioba inakusanya maoni kuhusu katiba mpya walio kuwa wanatoa maoni si wananchi ina maana unataka kusema wananchi walitoa maoni kwa kitu wasicho kijua?
 
Reactions: BAK
Ikiwa katiba iliyopo haisemi huyu asiyeitii (katiba iliyopo) achukuliwe hatua gani ndio ubovu wenyewe huo wa katiba iliyopo.

Tunataka katiba inayomuwajibisha mkiukaji
 
Crap crap crap. Katiba inayotakiwa ni katiba ya kumfanya rais asiwe Mungu mtu na hata akitaka kuivunja anashindwa. Najua upeo wako ni mdogo kiasi ambacho huwezi kuona logic.
 
Kwani kipindi kamati ya jaji warioba inakusanya maoni kuhusu katiba mpya walio kuwa wanatoa maoni si wananchi ina maana unataka kusema wananchi walitoa maoni kwa kitu wasicho kijua?
Unajua ni % ngapi ya watanzania wanaijua katiba iliyopo?

Ukishafahamu hilo basi utajua kwanini hii issue ya katiba watu wanaona ni kupoteza muda.

Nimetoa maoni yangu hapo. Tunaodai au wanaodai katiba mpya inatakiwa wahakikishe % kubwa ya jamii inaufahamu wa kutosha wa katiba iliyopo. Kwa maana ya mapungufu na hasara za hayo mapungufu. Wakishafanikiwa hilo, ndipo wawahamasishe hao watu wawaunge mkono kwenye kudai katiba mpya.

Kinachofelisha katiba mpya ni uelewa mdogo wa wananchi kuhusu umuhimu wa katiba kwenye uhalisia wa maisha yao
 
Ni kweli kabisa... Utii wa katiba iliyopo bila shinikizo...
 
Hoja hii ni ya msingi sana ninkubaliama nayo by 100%. Shida ni utii wa katiba hapo ndipo kwenye changamoto.Kwa kweli tatizo ni watawala kutotii misingi ya katiba na maudhui na maelekezo ya katiba yenyewe na ndiyo maana tunasema katiba iwe ya sasa au mpya inahitaji utashi wa kisiasa kuitii na hapo ndiyo kwenye tatizo. Nishauri viongozi wawe wa CCM inahitajika kuelewa kuwa katiba ndiyo mwongozo na mkataba wa watawala na wananchi iwe na mapungufu au nzuri muhimu ni kuiheshimu iliyopo. Hofu iliyopo ni kuwa katiba ya sass ni dhaifu siyo hivyo watu ndiyo dhaifu hata amri kumi za Mungu alizopewa Musa zinavunjwa ili hali tunajua hasira za Mungu. Binadamu anahitaji kurekebishwa kila wakati. Hoja nyingine ni kutoaminiana kwa viongozi wa CCM na CDM kila moja akitafuta namna ya kupenya kushika madaraka kwa kutumia katiba na upande mwingine kuwa na umakini kuwa marekebisho yoyote yanamwondoa mtawala madarakani. Hapa wapinzani waweke nia ya dhati ya mabadiliko kwa win win.
 
Umendika gazeti la mzalendo?
Uzi mrefu utazani report ya makinikia
Hapa kwetu ni pagumu sana kuna watu wanajiona wana akilisa kuliko wengine nadhani tunatakiwa kupiginia katiba mpya kwa wingi wetu pia inatakiwa kila Chama cha siasa kuwa na jeshi ili kuondoa huu ujinga
 
Umeandikwa pumba nyingiiiii.
Swali moja ni JE, akina nani walishiriki kutunga Katiba ya 1977?
JE, wananchi walishirikishwa kwa kiwango Gani?
Je, wananchi wana nguvu ya maamuzi kuhusu mustakabali wa uongozi na utawala?
Je, nini kifanyike ili hiyo Old Katiba ianze kuheshimika!
 
Sasa utamfundishaje mtu kutii katiba ambayo haihusiki kumuadhibu akitenda makosa?
 
Katiba mpya ni sawa na tume huru ya uchaguzi kwa CCM,kuzungumzia katiba mpya ni sawa na kudiriki kuiua CCM,suala ambalo kamwe wanaCCM hawatokubali!hili suala bado bichi kabisa,Mwenye maamuzi ya namna gani nchi iendeshwe ni mwananchi mwenyewe,Ila bahati mbaya Sana hajui hata hilo LIKATIBA ndo li nini?!!

Kuna gharama za uhai ili katiba mpya ipatikane ,wanaotakiwa kufa ndiyo haoo hawajui Katiba ina umuhimu gani!!
 
Hauja jibu swali mkuu
 
Pumbavu.
Tunasema ikiyopo haijabalance ndio maana unaweza kuichezea, ikiwepo ilio balance huwezi pata hiyo jeuri ya kuichezea maana ukiichezea inakunyoa.
 
Mnajifanya mna akili kuliko wazee wetu wote akina Kikiwete, Waryoba, Butiku... waliona katiba mpya inahitajika. Katiba nzuri inawabana wanaoivunja. Hii haina hicho kitu.
 
Reactions: BAK
Katiba mpya si kuwanufaisha wanasiasa bali Watanzania wote. Wewe na Watanzania wote tutakuwa na uhuru na haki ya kuchagua madiwani, Wabunge na Rais tuwatakao badala ya mtutu wa bunduki kutumika kutuwekea wale ambao HATUKUWACHAGUA.

Uchumi MBOVU unasababisha na VIONGOZI WABOVU ambao HATUKUWACHAGUA. Hawa hawana wasiwasi hata kama WATAVURUNDA kwani wanajua maccm watatumia tena mtutu wa bunduki ili wabaki madarakani.



 
Katiba iliyopo ni chama kimoja iliyoandikwa ba maccm 1977. Katiba hiyo imejazwa VIRAKA chungu nzima na maccm vile wavitakavyo wao bila ya KUWASHIRIKISHA vyama vya upinzani kitu ambacho si sawa.
Hatuwezi kuendelea kujidanganya kwamba tuna mfumo wa vyama vingi nchini wakati katiba husika ni ya chama kimoja.

Hivyo ulichoandika hakina usahihi wowote ule.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…