Tatizo la tumbo kujaa gesi na kupelekea mara kwa mara kutoa hewa chafu linahatarisha ndoa yangu

Tatizo la tumbo kujaa gesi na kupelekea mara kwa mara kutoa hewa chafu linahatarisha ndoa yangu

Aisee nilikua na hilo tatizo wife kidogo akimbie chumba aisee

Nikapata dawa

Unga wa mdalasini ndio dawa. Unachukua nusu kijiko kikubwa unatia kwenye glass ya maji unachanganya unakunywa. Ukitumia gas inakata saa hiyo hiyo na ukitumia mchana na jioni kwa mwezi mmoja tatizo linaisha

Asante
 
Habari Jf

Binafsi nilikuwa nina tatizo la tumbo kujaa gesi lilinitesa sana kwa mda mrefu ilipelekea na hali ya kutoa ushuzi kila mara ilinifanya nishindwe kufanya baadhi ya mambo kama vile Ibada ikawa imenipatia stress kiasi.

Gesi ilikuwa inajaa tumbo kama linajazwa upepo,lakini sasa natumia chai ya viungo nashukuru tumbo yangu imekuwa bora zaidi chakula kinameng'enywa vizuri,tumbo haijawai kujaa gesi napata choo kila kutwapo leo huu ni mwezi wa tatu sasa nakula chochote bila kupata hadha yoyote.

Tiba yake.
Chai ya viungo ni suluhisho sahihi na inafaida nyingi sana.

•Karafuu ya unga
•Mdalasini ya unga
•Tangawizi iliyosagwa
•Iriki

Tumia kutwa mara 2 mfululizo ukiweza kila siku,kama radha itakushinda tia sukari kidogo au asali.

Tumia hii chai inaweza kuwa ya maziwa pia itakuondoshea matatizo yanayohusiana na mmeng'enyo wa chakula na minyoo itaisha na utapata faida nyingi kwa kwenye mwili kama vile kupoza maumivu ya misuri,kupata usingizi na kuchangamka mwenye nguvu.
images-4.jpeg
images-3.jpeg
 
Weka kwenye sufuria vitu vifuatavyo Saga tangawizi vijiko 2,karafuu ya unga vijiko 2, mdalasini vijiko 2 kisha weka iriki punje 5,tia maji vikombe 2 au 1½ cha chai chemsha kwa dakika 10 uku umefunika ikiwa tayari kunywa ni nzuri waweza kuweka sukari au inaweza kuwa maziwa.
Vipimo vya viungo vinabadilika kulingana na mahitaji yako.
Ntajribu na mm unaiandaaje hyo chai maana na mi nna tatz hilo pia
 
Weka kwenye sufuria vitu vifuatavyo Saga tangawizi vijiko 2,karafuu ya unga vijiko 2,mdalasini vijiko 2 kisha weka iriki punje 5,tia maji vikombe 2 au 1½ cha chai chemsha kwa dakika 10 uku umefunika ikiwa tayari kunywa ni nzuri waweza kuweka sukari au inaweza kuwa maziwa.
Vipimo vya viungo vinabadilika kulingana na mahitaji yako.
Asante sana
 
Mimi nilikuaga na tatizo hili, siku nikazidiwa kweli kweli. Kukimbizwa hospital sijitambui, pigwa X-Ray.

Majibu yakatoka, utumbo umejikunja. ilibaki 5% tu nife.
 
Mimi nilikuaga na tatizo hili, siku nikazidiwa kweli kweli. Kukimbizwa hospital sijitambui, pigwa X-Ray.

Majibu yakatoka, utumbo umejikunja. ilibaki 5% tu nife.
Pole sana umenikumbusha mjomba wangu kipenzi alikumbwa na hilo tatizo alikaa wiki 1 na zaidi bila choo baada ya kwenda hospital aliambiwa kama ulivyoambiwa wewe alifariki kwa hilo tatizo,alifanyiwa operation baada wiki 2 aliaga dunia,R.N.P Uncle. Tumia chai ya viungo inasaidia kupunguza tatizo japo zipo njia nyingi.
 
Pole sana umenikumbusha mjomba wangu kipenzi alikumbwa na hilo tatizo alikaa wiki 1 na zaidi bila choo baada ya kwenda hospital aliambiwa kama ulivyoambiwa wewe alifariki kwa hilo tatizo,alifanyiwa operation baada wiki 2 aliaga dunia,R.N.P Uncle. Tumia chai ya viungo inasaidia kupunguza tatizo japo zipo njia nyingi.
Daaah... Hatari sana. Maisha haya
 
fika hospitali mkuu, ufanyiwe kipimo cha choo na "stool H.Pylori Antigen"... majibu atayatumia daktari kujua shida n nn ns kukupa dawa!
 
Haloo wadau naomba mnijuze shida itakuwa nn
Jichunguze unakula vyakula gani vinavyo sababisha wewe upate tumbo lako kujaa gesi? Hapo ndipo utakapo weza kujitibia maradhi ya tumbo kujaa gesi.

GESI TUMBONI (COLIC): Ikiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri tumboni, hukusanya gesi tumboni na kufanya mingurumo humo na kumsababishia maumivu, humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka jasho na machovu bila ya kufanya kazi. Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu kuumwa kwa mgongo au kiuno. Ikiwa gesi hii itakosa kutoka kwa njia ya haja kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya presha sehemu au karibu ya moyo na kusababisha maumivu ya moyo.

TIBA: Chukua asali robo lita , unga wa arki susi vijiko vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili vikubwa. Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni.
 
Haloo wadau naomba mnijuze shida itakuwa nn
mi langu lilikuwa linajaa gesi nilitibu kwa kacha vyakula vyenye GLUTEN. kwa sasa nakula Glueten free tu, hata uzito wa kilo zangu umekuwa sawia. mwanzo tumbo lilikuwa kubwa kuzidi mwili
 
Kanunue dawa moja ya edmark inaitwa shake off utakuja kuniambia inatoa uchafu wpte tumbo linakuwa safi hutopata kujamba ovyo utaharisha hasa watakupa maelekezo namna ya kutumia kisha njoo utupe marejesho
Inapatikana maduka ya dawa?
 
mi langu lilikuwa linajaa gesi nilitibu kwa kacha vyakula vyenye GLUTEN. kwa sasa nakula Glueten free tu, hata uzito wa kilo zangu umekuwa sawia. mwanzo tumbo lilikuwa kubwa kuzidi mwili
Vyakula vya gluten ni vipi hivyo
 
Haloo wadau naomba mnijuze shida itakuwa nn
Gastric juice ikimwaga kuburn Chakula kwa ajili ya kumeng'enywa kwa urahis ukiwa na ulaji mbovu mtindo wa maisha mbovu ni vyanzo vyake unfortunately hospital utaishia kupoteza muda wako tu hakuna tiba zaidi ya kujaza sumu za madawa katika mwili wako solution pekee ni therapy ya Supplements wasiliana nami kuzipata kwa gharama nafuu 0620258276
 
Waungwana naomba ushauri wenu katika hili tatizo hili limekuwa sugu kwangu huwa natumia dawa za kupunguza gesi lakini zikiisha tatizo linaendelea

Mwenzi wangu kwa maana ya mke kanivumilia kwa kipindi chote lakini sasa anasema nisipo tafuta utatumizi wa hili swala anaachana nami

Njia pekee inayo nipunguzia maumivu ya tumbo kujaa gesi na kunifanya nijihis na ahueni ni hii ya kupumua yaan kujamba

Nishauri ndugu zangu nifanye nini ili niondokane na hili tatizo lakini pia ni inusuru ndoa yangu
Tibiwa kwa tiba acupressure therapy. Hili ni tatizo la kuhama kwa SP, ikirekebishwa tatizo linakwisha. Msaada mwingine tafuna pilipili manga punje 4 na sukari kidogo asubuhi kabla ya kula chochote na usile chochote hadi nusu saa
 
Back
Top Bottom