SoC03 Tatizo la udumavu au utapiamlo kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano hasa katika maeneo ya vijijini

SoC03 Tatizo la udumavu au utapiamlo kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano hasa katika maeneo ya vijijini

Stories of Change - 2023 Competition

stier chris

Member
Joined
Jun 7, 2023
Posts
5
Reaction score
2
Habari zenu wanajamii wenzangu wa JamiiForums , katika makala hii fupi ninayoandika ni kwa lengo la kuelimisha na kufundisha wazazi na walezi juu ya umuhimu wa lishe bora hasa kwa watoto wadogo walio chini ya umri wa miaka mitano katika maeoneo ya vijijini na hii itaweza kusaidia kutengeneza afya bora ya mwili na akili kwa watoto na kutengeneza taifa imara la kesho.

Maana ya utapiamlo
Ni hali ambayo mwili unapata upungufu wa lishe muhimu au unapata lishe duni kwa kiasi kinachosababisha matatizo ya kiafya. Hali hii hujitokeza kutokana na ulaji wa chakula usiokidhi mahitaji ya mwili au matumizi mabaya ya lishe.

144525FA-FF23-497A-B5CE-DA4EA9773C42.jpeg


picha kutoka mtandaoni

Kuna aina mbili za utapiamlo
Moja; utapiamlo wa aina ya upungufu ( undernutrition). Hii ni hali ambapo mtu hapati lishe ya kutosha na kwahiyo mwili unakosa virutubisho muhimu kama vile protini na vitamini. Na aina hii ya utapiamlo unaweza kusababisha kupungua kwa uzito, udumavu na matatizo mengine ya kiafya.
Mbili; utapiamlo wa ziada ( over nutrition). Hii ni hali ambapo mtu anapata lishe yenye nishati nyingi kuliko mahitaji ya mwili. Mara nyingi hii husabishwa na ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, sukari na chumvi na pia huweza kusababisha unene kupita kiasi, hatari ya magonjwa ya moyo, kisukari na matatizo mengine ya kiafya yanayo husiana na lishe mbaya.

Sababu zinazo pelekea afya duni kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano katika maeneo ya vijijini

1. Upatikanaji mdogo wa huduma za afya
Hii ni moja kati ya sababu nyingi zilizopo na zinazosababisha afya duni kwa watoto walio chini ya miaka mitano, kutokana na kukabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya ambapo vituo vya afya katika maeneo hayo ya vijijini zinaweza kuwepo lakini mbali na maeneo yao ya kuishi na mara nyingi huduma katika vituo hivo zinakua ni duni. Hii huweza kupelekea na kusababisha kuchelewa kwa utambuzi na matibabu sahihi kwa watoto wenye afya mbovu.

2. Umaskini
Wakazi wengi wa maeneo ya vijijini hukabiliwa na tatizo la umaskini ambapo hali hii inaweza kuadhiri upatikanaji wa chakula bora kwa watoto na pia inaweza kusababisha wazazi na walezi wengi kushindwa kwenda katika vituo vya afya kwa kupewa elimu juu ya lishe bora kwa watoto.

3. Usafi wa mazingira
Katika maeneo ya vijijini mara nyingi huwa na changamoto katika mazingira bora na safi, ambapo kutokana na uchafu wa mazingira watoto wanaweza kukabiliana na magonjwa ya mripuko ambayo yanaweza kusababishwa na mazingira hayo kama kipindupindu, kuhara.
10380F6F-3E7F-485D-811B-488EE488B887.jpeg

Picha kutoka mtandaoni

4. Elimu duni ya afya
Kwa wazazi na walezi katika maeneo ya vijijini elimu kuhusu ya afya inakua duni ambapo kunakua na ukosefu wa ufahamu juu ya kanuni za afya kama vile lishe bora, usafi wa mazingira na kinga dhidi ya magonjwa. Na kutokana na uhaba wa maarifa au taarifa hizi zinaweza kusababisha matatizo ya afya ambayo yangeweza kuzuiwa.

5. Lishe duni
Hii pia ni moja ya sababu zinazopelekea afya duni kwa watoto wadogo ambapo kutokana na changamoto ya umaskini katika maeneo ya vijijini husababisha upatikanaji duni wa vyakula bora kwa watoto kama protini, madini na vitamini ambavyo vingeweza kuwasaidia watoto kujenga afya ya mwili na akili kwa watoto. Na hii pia husababishwa na ukosefu wa elimu kwa wazazi juu ya lishe bora kwa watoto.

6. Mazingira hatarishi
Watoto wengi wanaoishi katika maeneo ya vijijini mara nyingi wanaishi katika mazingira hatarishi kama vile ukosefu wa makazi bora na safi, hatari za ajali, matumizi ya nishati chafu ambapo haya mazingira yaweza kusababisha magonjwa ya upumuaji, maambukizi na majeraha ambayo yanaweza kuepukika.

Njia ambazo zinaweza kusaidia kuepuka matatizo yanayoweza kusababishwa na udumavu kwa watoto wadogo

1. Kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo ya vijijini- hii itafanikiwa kwa kuongeza miundombinu mizuri ya afya katika maeneo hayo, hii inajumuisha kujenga vituo vya afya vya kutosha, kupeleka wataamalu wa afya katika maeneo hayo na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa kutoa elimu kwa wazazi na walezi juu ya afya bora kwa watoto kuzuia magonjwa yanayoweza kuzuilika.

2. Kutoa elimu ya afya
Serikali kupitia wizara ya afya inatakiwa kuwekeza katika mipango ya elimu ya afya katika maeneo ya vijijini. Hii inaweza kujumuisha utoaji wa elimu kwa wazazi na walezi juu ya lishe bora, usafi wa mazingira, kinga dhidi ya magonjwa na inaweza kutolewa kupitia njia za intanenti , mawasiliano , televisheni na vituo vya redio ambazo zinafikika kwa jamii kwa urahisi .
A47779A5-7850-485D-A86D-C2006F0E9B48.jpeg

Picha kutoka mtandaoni

3. Kupambana na umaskini
Hii inaweza kusaidiwa kwa kutoa fursa za ajira kwa wakazi wa vijijini, kutoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na kuwekeza kwenye kilimo na miundombinu ya kijamii, ambapo hii itasaidia kupunguza tatizo la umaskini na kutawezesha familia mbalimbali katika maeno hayo kuwa na uwezo wa kununua vyakula bora kwa watoto.

4. Kuwekeza katika miundombinu ya maji safi na usafi wa mazingira
Serikali inapaswa kuimarisha upatikanaji wa maji safi na huduma za usafi wa mazingira katika maeneo ya vijijini, hii inajumuisha uchimbaji wa visima, kujenga mifumo ya maji na kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya maji safi na mazingira safi ambazo zitaweza kuzuia hatari ya magonjwa ya mripuko.

Njia zinazoweza kutumika kutoa elimu kwa wazazi na walezi katika maeneo ya vijijini

1. Vituo vya redio ya jamii
Hii inaweza kusaidia kufikisha elimu kwa wazazi na walezi kwa urahisi na kufikika kwa kupitia Matangazo yanayoweza kuwa ya vipindi vya elimu ya afya ambapo wataalamu wa afya wataweza kutoa elimu na ushauri juu ya lishe bora kwa watoto.

2. Vikundi vya jamii
Hivi vikundi vinaweza kuwa njia moja wapo kwa kutoa elimu na kufikisha maarifa hayo kwa wazazi na walezi kwa urahisi katika maeneo hayo , vikundi hivyo ni kama mama lishe ambapo wanaweza kufanya vikao mara kwa mara ambapo wataalamu wa afya wataweza kutoa mafunzo ya afya.

3. Kampeni za elimu
Hizi kampeni zinaweza jumuisha mikutano ya hadhara, maonyesho na semina zitakazohusu masuala ya afya na lishe bora kwa watoto.

4. Watoa huduma za afya katika maeneo ya vijijini
Hawa wanaweza kutumika kama chanzo muhimu cha kutoa elimu ya watoto kwa wazazi na walezi , ambapo wanaweza kufanya ziara nyumba kwa nyumba ili kutoa ushauri binafsi kuhusu lishe bora, kinga dhidi ya magonjwa na huduma za kutembelea vituo vya afya kwa kujua afya za watoto.
787E86AC-FDF3-4415-8273-F0E556B3FC04.jpeg

Picha kutoka mtandaoni

5. Matumizi ya teknolojia ya mawasiliano
Hii ni moja kati ya njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwa kutoa elimu kwa wazazi na walezi kuhusu umuhimu wa lishe bora, ambapo teknolojia hizo ni kama intanenti, programu za simu na tovuti zinazoweza kutoa habari ya vidokezo juu ya lishe na pia ujumbe wa maandishi ( SMS) zinazoweza tumika kusambaza habari ya afya bora ya watoto kwa wazazi na walezi.

Hitimisho:
Kwa takwimu zilizooneshwa mwaka 2015-2016 ya afya imeonesha theluthi ya watoto wenye umri ulio chini ya miaka mitano wanaudumavu na 14% wanaupungufu wa uzito na hii inaweza kusababishwa na sababu mbalimbali kama zilivotajwa hapo juu. Na huu umekua mpango kwa Serikali kwa kuboresha lishe kwa kutoa elimu pamoja na kuboresha miundombinu ya vituo vya afya kwa maendeleo endelevu. Uwepo wa utapiamlo au udumavu unadhoofisha maendeleo katika nchi na lishe duni kwa watoto ndio imeweza kupelekea vifo vya watoto waliochini ya miaka mitano nchini Tanzania na inakadiwa kugharimu Serikali asilimia 2.6 ya Pato la Taifa kila mwaka. Kutokana na madhara mengi kuweza kutokea elimu bora inatakiwa kutolewa kwa wazazi na walezi kuhusu elimu ya afya kwa watoto hii itaweza kusaidia kupunguza magonjwa yanayoweza kuzuilika kupitia lishe iliyo bora kwa watoto na itasaidia watoto kukua vyema katika afya nzuri ina bora ya mwili pamoja na akili katika kuongeza nguvu kazi katika jamii na Taifa lijalo.

Jina: Salustia Christopher
Namba ya simu: 0682086313
Email: Christophersalustia gmail.com
 

Attachments

  • 54D1C511-F5EF-467B-8A76-2DEDB2EB02A0.jpeg
    54D1C511-F5EF-467B-8A76-2DEDB2EB02A0.jpeg
    142.3 KB · Views: 11
Upvote 4
Ishu ya utapiamlo ni suala la elimu na Sio umasikini kwa mazingira ya kijijini.
 
Mlonge unafanya Kazi nzuri sana ya kuondoa utapiamlo
 
Mkaa unafanya kazi nzuri Sana ya kusafisha maji machafu yakawa safi kabisa na salama kwa kunywa pasipo na wadudu.
Utengeneze mkaa wa mti usio na sumu.
 
Ishu ya utapiamlo ni suala la elimu na Sio umasikini kwa mazingira ya kijijini.
Ndio ni suala la elimu lakini katika maisha ya haswa maeneo ya vijijini watu wengi wanakumbwa na tatizo la umaskini hiyo inapelekea wazazi kushindwa kuwa pangilia watoto mlo ulio sahihi yani lishe bora zaidi watoto kuishia kula vyakula vya wanga tu ambavyo vinaenda kuwadumaza watoto wengi walio chini ya umri wa miaka 5
Mlonge unafanya Kazi nzuri sana ya kuondoa utapiamlo
Ni kweli lakini utapiamlo unaweza ondolewa na sababu tajwa hapo juu hizo zitapelekea afya Za watoto kuwa imara
 
Back
Top Bottom