Tatizo la umeme: Awamu ya tano haiwezi kukwepa lawama labda tu kama madai hayana ukweli

Mataga lazima usikitike
Sawa mzee ila maji na umeme tunakosa wote ikibidi na majenereta yao utanunua! Alafu sikia hii, 5 yrs ago hiki hakikutokea! Endeleeni kusikiliza hii chain ya upigaji. Tulifikiri ni kilio cha machinga, sasa wote tunalia na bado mbona .....
 
Kupanga ni kuchagua SG ingekamilika tungekuwa mbali mbo
 
Fuatilia huo uzi uone watu walivyokuwa wanalalamika kuhusu umeme, tena February!!

Nyuzi nyingine....

1. Kuna mgao wa umeme wa kimya kimya December 05, 2020
2. Mgao mkali wa umeme Morogoro mjini - December 21, 2020
3. Wilaya ya Ubungo kuna mgao wa umeme? Mpaka sasa hakuna umeme March 01, 2021
4. TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini March 04, 2021

Hayo ni malalamiko yaliyotokea sehemu mbalimbali za nchi ndani ya miezi 3 TU!!!
 
Kuna watu wanapita hivi hivi bila kutazama uzi wako, hii yote kwa kuwa wanamchukia Rais wa sasa. Ukitaka kuwatawala watanzania wape maneno matamu hata kama uongo.
 
Mnataka kutuambia wakati wa Magufuli umeme ulikuwa haukatiki?

Nani angethubutu kutangaza mgao?
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe. Hata Adolf Hitler Wajerumani wanamheshimu kwa kuchangia sana ukuwaji wa teknolojia ya viwanda vikubwa.
Hakuna dhambi kukiri yale mazuri yaliyofanywa na Magufuli. Lakini huyu mama atawaacha wengi sana kwenye great disappointment.
 
Hakuna mtu analazimisha Samia atawale kama Magu!

Watu wanalalamika kuona kuna uhaba wa maji na umeme alafu lawama anatupiwa Magu ambae kipindi chake hatukuona magao kabia
Hao wanaomtupia lawama Magu ni wajinga pia, Magu ameshakufa, ni kuachana naye, tulio hai tusonge mbele, harudi tena! Na nyie mnaopambana kumtetea Marehemu as if yupo hai mnakosea pia, Mnapotaka kumgeuza Magu kuwa SI UNIT ya kutawala nchi hii mnakosea zaidi, hakuwa perfect!! Kinachoshangaza ni nyie wapambe kushupalia haya mambo, Sijawahi kumsikia Samia hata siku moja akimuongelea vibaya Magu, zaidi ya kummwagia sifa!! Siku Samia akiongea chochote kibaya kuhusu aliyekuwa bosi wake hapo mnaweza kuja juu na kutoa mapovu
 
Kama wewe ni msomi sababu za uhaba wa maji huko china kulingana na hii habari ni tofauti kabisa na hizi zetu hapa
Tofauti, lakini yanatokea kipindi kimoja.....Why hayo matatizo yote yatokee kipindi kimoja? Kwa nini miaka yote hayajatokea kwa pamoja namna hii? Lazima kuna common cause inayounganisha hayo matatizo dunia nzima
 

You said it all
 
Kumbe hujui lolote...

To prove me wrong, nijibu maswali yafuatayo:-

1. Je, hivi sasa ni kweli kuna ukame au hakuna?
2. Baada ya kuvutwa gesi kutoka Mtwara, serikali ilipanga Kinyerezi I, II, III, na IV ili kupunguza tatizo la umeme! Je, hadi sasa zimejengwa ngapi?
3. Katika umeme uliongizwa kwenye gridi ya taifa, umeme wa maji ni % ngapi na umeme wa gesi ni % ngapi?

Tuanze hapo kwanza ili nifahamu najadiliana na mtu anayejua anachokiongea au ni mropokaji tu ambae huko vichochoroni akisikia hiki, nae anakimeza kama kilivyo bila kutafuta taarifa za ndani!!
 
Inamaana miradi ya umeme waliyokuwa wanaizindua ,nyuma na mbele ya mikamera yalikuwa ni maigizo? duu! mnanikumbusha 'ze comedy'
 
Na wewe ukaamini kwamba Tanzania kuna umeme zaidi ya ule unaohitajika?!

Hivi katika pitapita yako, unafahamu chanzo chochote kipya kilichoongezwa wakati wa JPM na kikawa kinazalisha umeme hivi sasa ulio kwenye grid ya taifa?

Lakini ndo yale yale... yaani serious issues zinapokuwa raised, oh wanalenga kumchafua Magufuli wakati kila mwenye uelewa anafahamu kwamba Magufuli alipiga chini miradi yote ambayo hivi sasa ingekuwa imeshakamilika, na akahamishia nguvu kwenye Bwawa la Nyerere mradi ambao tungetakiwa kuanza moja!!

Na alifanya hayo wakati taifa limeshaingia gharama ya kujenga bomba kutoka Mtwara, na ambacho kilibaki ni kujenga mitambo tu ya kuzalisha umeme pale Kinyerezi... Je, alijenga hiyo mitambo ukiacha Kinyerezi II ambayo alikuta mchakato umeshaanza?
 
Nchi ilikuwa mali binafsi ya mtu
 
Huyu alikuwa mpiga dili tupu
 
Kwa hiyo wewe unamwamini.nani akisema kuna kitu flani basi unamwamini lakini kwa tanzania huamini?
 
Usiwe zwazwa kama huyo Zito wako!

Habari za watu kuokotwa kwenye viroba ulitangaziwa ila ya mgao wa umeme usitangaziwe?

Hivi umeme ukikatika watu hawawezi kujua?

Kwamba mgao ulikuwepo lakini hauonekani? Hivi mgao ni jambo la kuficha kweli? Kuna mambo Baba wa watu atasingiziwa sana kwa vile hayupo.
 
Kongole kwa uchambuzi
 
Kuna mitambo ililetwa ya kuzalisha umeme wa gesi kama huelewi nenda kaulize tanesco na ndio maana walizima mitambo ya mafuta baada ya kukamilisha ujenzi wa hiyo mitambo na kupanua kinyelezi one na two ili kuongeza mgwt,
Kaulize huko tanesco kama hujui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…