Tatizo la umeme: Awamu ya tano haiwezi kukwepa lawama labda tu kama madai hayana ukweli

Tatizo la umeme: Awamu ya tano haiwezi kukwepa lawama labda tu kama madai hayana ukweli

Futa kauli yako mkuu, hujawahi kuona mgao kweli au kwa sababu haikusemwa ni mgao? Jiulize pia ni Watu wangapi wameunganishwa baada ya Samia kushusha bei mpaka 27000,matumiz yameongezeka na production imeshuka.
Labda kama huoni hili jua na joto basi kwako itakuwa uzalishaji uko pale pale
Samia yupi alieshusha umeme mpaka 27000?

Nina uhakika baada ya Samia kuingia madarakani walioungdanishiwa umeme nchi nzima hawazidi elfu 1
 
Ukiona watu hawakumbuki ujue it was immaterial damage, sawa na kutafuta tone la maji kwenye bahari.. Ila ya sasa ni gumzo..

Jaribu kujiuliza hata kidogo why now tention iko juu sana? Kwa mizania ya idadi ya nyuzi zilizofunguliwa ndani ya siku hizi chache tu..

Hitilifu za hapa na pale hazikosekani ila zisikithiri.
Ni kwamba hawakumbuki au ni Praise Team?!

Watu wanakaa wiki 2 bila umeme halafu unaita "hitilafu za hapa na pale"?!

Na swali ambalo mara kwa mara nimekuwa nikihoji bila kupatiwa majibu ni vyanzo gani vipya vya umeme ambavyo vilianzisha hata nchi iwe na umeme wa bwelele?!

Hata ukisoma ripoti za wizara wenyewe tena enzi za JPM, wanaonesha umeme uliokuwa unategemewa sana ni wa gesi... yaani gesi ile ile ambayo kutokana na ushabiki tu, wanakejeli ili kutetea mradi wa Bwawa la Nyerere!!

Hata mipango ya awali ya kujenga Kinyerezi III na Kinyerezi IV ikaachwa kwa sababu ya Bwawa la Nyerere!!!

Watu ukiwapa huo ukweli, wanatoa povu!!!
 
View attachment 2015658

Zitto ni mtu ambae anatafuta information na kujenga premise uchwara anazotaka yeye.

TANESCO long term plan yao ya umeme inapatikana kwenye hapo juu ☝️na kwenye pipeline kuna renewables, hydropower (stigler gorge is also mentioned), gas and coal. Hakuna priorities ya kipi kianze.

Yeye anachukua source moja na kujengea hoja kama makosa with very simple arguments, watu kama hao wakimpata mtu anaefahamu maswala ya energy kuwa expose limitations zao ni rahisi sana.

Ukiangalia tu ivyo vyanzo vyote vya gas gharama yake inafika $2.9 billion umeme ni megawatts 2500.

Bwawa la Nyerere gharama $2.9 billion umeme megawatts 2115.

Bwawa la Nyerere lina cheap unit costs.

More safe maana bomba la gas lina line moja tu hakuna back. Likichezewa nchi nzima aina umeme na tayari over 64% ya umeme wetu unatokana na Gas kuongeza tena hiyo sio hatua nzuri ya kumitigate energy security risks.

Ukishatengeneza vyanzo inabidi uajiri na kuna gharama za matunzo. Bwawa la Nyerere linaondoa operation costs za plant kama nne hivi za kujenga gas plants.

Vitu vingine ata kuandika shida, I tell you kule Twitter ni kikundi cha wapuuzi tu huwa wanaandika vitu ambavyo awajawahi kuvifanyia research na kuviandikia report katika maisha yao; yaani ni ujinga mtupu.
Naam, Zitto na watu wake walishaelezwa humu kuwa Levellised Cost of Energy ya hydropower ni ndogo kuliko ya umeme wa gas! Hivyo hydropower inatija kwa wananchi kuliKo umeme wa gas.

Halafu yeye ni mchumi, ndiyo maana nakuunga mkono kuwa anatumia namba kusway opinions za watu bila uangalifu!
 
Ukweli ni kitu adimu sana kwenye ulimwengu wa siasa.
Magufuli alikuwa na upendo wa kipekee sana na Tanzania na kizuri zaidi Magufuli alikua na uwezo mkubwa wa kuelewa na kutafakari mambo. Lazima tukubaliane na uhalisia wa sasa kwamba tumempoteza kiongozi(head) hivyo kila mwenye dili lake anatumia ujuzi wa lugha na ushawishi wa namna yake kutwist ukweli ili agenda yake ipite.
Magufuli aliweka wazi ni hatari sana nchi kupoteza control kwenye eneo nishati hivyo kupunguza utegemezi ndio maana alifufua agenda ya strigler. Na aliamua kwenda kwenye maji kwa kutambua eneo ya natural gas limeshakamwata na wabia (kampuni za nje) hivyo tutakuwa tumepoza eneo hilo.
Lazima uelewe taifa lina idadi kubwa ya viongozi wabinafsi na wala rushwa hivyo ni nadra kwao kufikiri miaka 50 baada ya leo na kukubali kupokea 10% ambazo zinazaa manufaa binafsi na mzigo mkubwa kwa nchi.
Kwamba Magufuli alikuwa na upendo kwa watanzania nakupinga vibaya sana ! na bila shaka utatandikwa laana kwa uongo wako huu .
 
Ushauri kwa serikali ya awamu ya 6

1.Endelezeni kazi kama kauli mbiu yenu inavyosema ili na nyinyi muache legacy kama JPM.

2.Huku mtaani wananchi wamewachoka mnawafanya wamtamke Magufuli kila uchwao.

3.Mkidhani kujitetea kwenu kwa kushindwa kuongoza nchi ni kutupa lawama kwa uongozi uliopita MNACHEMKA VIBAYA.

4.Watanzania wa zama zile sio watanzania wa sasa kuweni makini mchape kazi zionekane acheni blabla.

5.Acheni kutumia watu kama zitto kuja mitandaoni na kuwatetea mnazidi kuwatia hasira watanzania.

MLIDHANI UONGOZI NI LELEMAMA EEEH,TUNATAKA KUONA KAZI KAMA ZA AWAMU YA 5 YA MWAMBA JPM.

Ni mimi

Mwakilishi wa wananchi wanyonge ambae anaeleza hali halisi sio hizo taarifa zenu zilizopambwa za uongo mnazomdanganya chief hangaya kama anafanya vizuri wakati wananchi wanalalamika kutwa.
 
By Zitto kupitia twitter:

Mradi wa 300MW Mtwara ulisimama. Mradi wa 350MW Kilwa ulisimama. Mradi wa nyongeza Kinyerezi 185MW ulisimama. Mradi wa Kinyerezi 3 and 4 umesimama. Utapata wapi Umeme kulisha nyongeza ya shughuli za Uchumi baada kufungua Nchi?

Miradi yote ya Umeme iliyokuwa kwenye power system master plan ilisimama kupeleka hela kwenye Stigler’s gorge ambayo wataalamu wote walituambia itachukua Miaka 7 kukamilika 100%.Lakini Kwa kuwa Sisi ni Watu wa kukubali uongo na propaganda tukaamini. Leo tunaambiwa delays tunawaka.

Siamini kuna hujuma. Ninaamini ni mambo ya kisera na madhara ya Miaka 5 unusu ya incompetence katika uendeshaji wa Uchumi. Tulidanganywa na tukaamini uongo huo. Sasa tunatumia uongo ule kuwapima wenye Mamlaka sasa. NCHI HAINA UMEME WA KUTOSHA. Hatujaongeza Hata 1MW kwa Miaka 5
Hizi nazo ni propaganda ambazo Zitto anajiingiza mzima mzima na kujiweka ndani ya boksi.

Pamoja na kutopenda kutetea uovu na uozo mwingi uliokuwepo kwenye serikali ya Magufuli, lakini pia ni dhahiri sasa kwamba kuna kundi la hawa akina Zitto wanaojipambanua kutetea maslahi wanayoyajua, na ambayo si lazima yawe maslahi ya waTanzania.

Zitto aeleze tujue hao wataalam waliokuwa na hakika ya miaka 7 ya kukamilika kwa bwawa, kwa maana wengine hatujui ushauri huo unatokana na nini hasa, kukosa pesa, au kutokana na ugumu wa kazi iliyopo? Tusitishwe tu kwa kuambiwa umeme ilijulikana usingepatikana katika hiyo miaka 7, huku ni kutishana na kupiga propaganda.

Hiyo miradi ya gesi anayoitaja, ilipangwa kukamilika katika muda gani na kwa gharama zipi! Je, ni kweli hele zilizopangiwa kutekeleza miradi hiyo ndizo zilizopelekwa kwenye bwawa? Hii miradi haikuwa ya wawekezaji? Haelezi! Huu nao utakuwa ni upotoshaji wa kupiga propaganda kwa minajiri ya kujinufaisha kwa makundi fulani.

Yeye anaamini hakuna hujuma kwa haya tunayoyaona leo. Lakini mbona imekuwa ghafla namna hii, na kwa nguvu kiasi hiki? Ili wananchi walainishwe?

Sasa sikiliza yanayosemwa: mabwawa hayana maji ya kutosha ndiyo maana umeme utakuwa wa mgao. Sawa! Je, majenereta ya gesi yaliyopo nayo imekuwaje kwa haraka na kwa mara moja tusiweze kuyatumia kuepuka adha ya mgao? Wanasema yako "maintence"? Hii inaingia kwenye akili kweli? Maintenance wakati ambapo yalikuwa yanatakiwa yawe standby' kufanya kazi?

Magufuli alikuwa ni mwongo na mbabaishaji wa hali ya juu sana, lakini hii timu iliyoingia sasa inayopigiwa chapo na akina Zitto inaweza kuwa ni timu hatari zaidi kwa taifa hili la Tanzania.
 
Naam, Zitto na watu wake walishaelezwa humu kuwa Levellised Cost of Energy ya hydropower ni ndogo kuliko ya umeme wa gas! Hivyo hydropower inatija kwa wananchi kuliKo umeme wa gas.

Halafu yeye ni mchumi, ndiyo maana nakuunga mkono kuwa anatumia namba kusway opinions za watu bila uangalifu!
Halafu hizo estimates wanazotumia ni za 2010, walau tunajua gharama za bwawa la Nyerere $2.9 billion ni current costs.

Hiyo miradi ya gas hadi ikamilike inahitaji inflation adjustments kutokana na makadirio yake ni 2010 currently inaweza pita $4 billion.

Zitto ni mwanasiasa ambae anasoma mipango ya serikali ila anatabia ya ‘cherry picking’ on information kwenye kujenga hoja kutokana na agenda zake.
 
Au mimi ndo sijaelewa eti mama kufungua nchi ndo umeme umekuwa on demand mpaka kufikia level ya magao!?
Ukitaka kuwaelewa vizuri hawa watu (akina Zitto), jitahidi kuelewa lugha rasha rasha kama hiyo ya "kufungua nchi" wanayoitumia 'subconsciously' bila ya kustuka watakavyoeleweka.
 
By Zitto kupitia twitter:

Mradi wa 300MW Mtwara ulisimama. Mradi wa 350MW Kilwa ulisimama. Mradi wa nyongeza Kinyerezi 185MW ulisimama. Mradi wa Kinyerezi 3 and 4 umesimama. Utapata wapi Umeme kulisha nyongeza ya shughuli za Uchumi baada kufungua Nchi?

Miradi yote ya Umeme iliyokuwa kwenye power system master plan ilisimama kupeleka hela kwenye Stigler’s gorge ambayo wataalamu wote walituambia itachukua Miaka 7 kukamilika 100%.Lakini Kwa kuwa Sisi ni Watu wa kukubali uongo na propaganda tukaamini. Leo tunaambiwa delays tunawaka.

Siamini kuna hujuma. Ninaamini ni mambo ya kisera na madhara ya Miaka 5 unusu ya incompetence katika uendeshaji wa Uchumi. Tulidanganywa na tukaamini uongo huo. Sasa tunatumia uongo ule kuwapima wenye Mamlaka sasa. NCHI HAINA UMEME WA KUTOSHA. Hatujaongeza Hata 1MW kwa Miaka 5
Kama unakumbuka serikali ilishasema mara nyingi kuwa umeme uliopo ni zaidi ya matumizi ya tanzania yote na wakasema kuna ziada ya mgw 270 au zaidi
Sasa je nini kimepunguza hizo ziada mpaka kuwepo na upungufu?
Ni.bwawa gani lina zaidi ya mgw 260 hapa tz na limesimama kufanya kazi?

Kauli ya waziri mara ya kwanza ni kuwa wanafanya ukarabati et watu waliogopa kukata umeme.
Mara ya pili wanasema ni kupungua kwa maji
Sasa jiulize hizo kauli kinzani zina maana gani kama sio kutaka kutupiga ili wanunue mafuta mazito kwa bei kubwa ili wagawane chao?

Wazili hajui nini tatizo la umeme na kesho atasema gesi imepungua.
Lengo amchafue magufuli kisha atupige wadanganyika huku tukilaumu kitu kisichokuwapo.

Kwa hiyo hata kutoa taarifa kuwa wanakata umeme nalo ni kosa la magufuli?
Makamba na zito sasa wanataka kuitafuna tanesco,
?walianz kutaka kuibinafsisha tena wamekuja na mambo mengine.
 
Back
Top Bottom