Tatizo la umeme: Awamu ya tano haiwezi kukwepa lawama labda tu kama madai hayana ukweli

Tatizo la umeme: Awamu ya tano haiwezi kukwepa lawama labda tu kama madai hayana ukweli

Acheni upumbavu jamani!

Jk alikuwa na mgao wa umeme wa kufa mtu!

Magufuli hakuwa na mgao kabisa wa umeme...!

Samia kaingia tu tayari mgao, hebu twambieni huyu mnaemlaumu yeye alikuwa anatumia mitambo ipi?
Sio tu hakuwa na mgao pia alizima mitambo ya IPTL ya akina singa singa na rugemalila na walinyimwa leseni ya kuendesha biashara yao ya kuuzia umeme Tanesco.
Hizi blaah blaah za Waziri na wapambe ndio hujuma zile zimeshaanza ili kurejesha biashara ya IPTL ya kukusanya hela za kugawana kwenye viroba!
 
Nadhani kuna kitu ambacho wewe na mimi hatukijui. Inawezekana kabisa miradi yote hiyo ilikuwa na upigaji mwingi, yaani ilijaa rushwa na watu walikuwa wameshachukua rushwa tayari. Na ndiyo maana kwa sasa kinachotokea ni kuhakikisha "kazi iendelee" ya kufufua yale ambayo awamu ya 5 iliyaona hayafai yanaendelezwa. Kuhusu umeme wa maji nadhani nayo ilikuwa master plan. Kuhusu kukatika kwa umeme kwa kweli sijui awamu ya 5 hayo mambo hayakuwepo.
Vision ya Magufuli ilikuwa ni umeme wa bei nafuu wa maji ambao ungeongezea huu uliopo kwa kiwango kikubwa tu. Hata tungetengeneza wa gas ila wa maji uwepo kwanza!

Halafu kupungua kwa maji sio kosa sababu system ya hydropower inafanya kazi kwa kukusanya maji mengi sehemu moja kabla hayajaachiliwa kusukuma turbines kwenye poromoko!
 
View attachment 2015658

Zitto ni mtu ambae anatafuta information na kujenga premise uchwara anazotaka yeye.

TANESCO long term plan yao ya umeme inapatikana kwenye link hapo juu ☝️na kwenye pipeline kuna renewables, hydropower (stigler gorge is also mentioned), gas and coal. Hakuna priorities ya kipi kianze.

Yeye anachukua source moja na kujengea hoja kama makosa with very simple arguments, watu kama hao wakimpata mtu anaefahamu maswala ya energy kuwa expose limitations zao ni rahisi sana.

Ukiangalia tu ivyo vyanzo vyote vya gas gharama yake inafika $2.9 billion umeme ni megawatts 2500.

Bwawa la Nyerere gharama $2.9 billion umeme megawatts 2115.

Bwawa la Nyerere lina cheap unit costs.

More safe maana bomba la gas lina line moja tu hakuna back. Likichezewa nchi nzima aina umeme na tayari over 64% ya umeme wetu unatokana na Gas kuongeza tena hiyo sio hatua nzuri ya kumitigate energy security risks.

Ukishatengeneza vyanzo inabidi uajiri na kuna gharama za matunzo. Bwawa la Nyerere linaondoa operation costs za plant kama nne hivi za kujenga gas plants.

Vitu vingine ata kuandika shida, I tell you kule Twitter ni kikundi cha wapuuzi tu huwa wanaandika vitu ambavyo awajawahi kuvifanyia research na kuviandikia report katika maisha yao; yaani ni ujinga mtupu.
Kuna kenge watakuja kukukejeli haya ndio mambo wengi hawaelewi! Magufuli hakuwa mjinga kama ambavyo wengi wanataka kuaminisha umma. When it came to infrastructures na project benefit analysis jamaa alikuwa ni mwamba.
 
Zitto saiz ni miongon mwa wanasiasa wanaohaha, sera zake hazina version, tangu kifo Cha mzee, mambo mengi yanadelay sana, kuanzia miradi yamaendeleo iliyokuwa inaenda kwakasi kubwa saizi imekuwa slow sana, na icho ndo kitu kilichofanya mirad ya umeme mingi ikwame kukamilika Kama matarajio yalivyokuwa na kufanya kuibuka kwa tatizo la umeme tunalokabiliana nalo saiz
Usimamizi mbovu
 
By Zitto kupitia twitter:

Mradi wa 300MW Mtwara ulisimama. Mradi wa 350MW Kilwa ulisimama. Mradi wa nyongeza Kinyerezi 185MW ulisimama. Mradi wa Kinyerezi 3 and 4 umesimama. Utapata wapi Umeme kulisha nyongeza ya shughuli za Uchumi baada kufungua Nchi?

Miradi yote ya Umeme iliyokuwa kwenye power system master plan ilisimama kupeleka hela kwenye Stigler’s gorge ambayo wataalamu wote walituambia itachukua Miaka 7 kukamilika 100%.Lakini Kwa kuwa Sisi ni Watu wa kukubali uongo na propaganda tukaamini. Leo tunaambiwa delays tunawaka.

Siamini kuna hujuma. Ninaamini ni mambo ya kisera na madhara ya Miaka 5 unusu ya incompetence katika uendeshaji wa Uchumi. Tulidanganywa na tukaamini uongo huo. Sasa tunatumia uongo ule kuwapima wenye Mamlaka sasa. NCHI HAINA UMEME WA KUTOSHA. Hatujaongeza Hata 1MW kwa Miaka 5
Kwahiyo sasa hivi haupigi mwingi
 
Kipindi cha magufuli umeme ulikuwa unakatika kama kawa ,thread zipo kibao humu ,sema ndiyo TANESCO wasingeweza kutangaza.
Unakatika ila sio kwa siku nzima au zaidi ya siku! Marekebisho ya muda mchache umeme unakuwa umerudi. Sababu ni za msingi kama ni transformer imebutuka replacement ya haraka watu wanaendelea na huduma.
 
Sio tu hakuwa na mgao pia alizima mitambo ya IPTL ya akina singa singa na rugemalila na walinyimwa leseni ya kuendesha biashara yao ya kuuzia umeme Tanesco.
Hizi blaah blaah za Waziri na wapambe ndio hujuma zile zimeshaanza ili kurejesha biashara ya IPTL ya kukusanya hela za kugawana kwenye viroba!
We waache waneng'eneke tu..

Muda utaongea
 
Fuatilia huo uzi uone watu walivyokuwa wanalalamika kuhusu umeme, tena February!!

Nyuzi nyingine....

1. Kuna mgao wa umeme wa kimya kimya December 05, 2020
2. Mgao mkali wa umeme Morogoro mjini - December 21, 2020
3. Wilaya ya Ubungo kuna mgao wa umeme? Mpaka sasa hakuna umeme March 01, 2021
4. TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini March 04, 2021

Hayo ni malalamiko yaliyotokea sehemu mbalimbali za nchi ndani ya miezi 3 TU!!!
Acha uongo Mimi naishi Tanzania usitete ujinga haitakusaidia
 
Unakatika ila sio kwa siku nzima au zaidi ya siku! Marekebisho ya muda mchache umeme unakuwa umerudi. Sababu ni za msingi kama ni transformer imebutuka replacement ya haraka watu wanaendelea na huduma.

Hapo sawa maana baadhi wanaconclude kwamba ulikuwa haukatiki kabisa.
 
Hao wanaomtupia lawama Magu ni wajinga pia, Magu ameshakufa, ni kuachana naye, tulio hai tusonge mbele, harudi tena! Na nyie mnaopambana kumtetea Marehemu as if yupo hai mnakosea pia, Mnapotaka kumgeuza Magu kuwa SI UNIT ya kutawala nchi hii mnakosea zaidi, hakuwa perfect!! Kinachoshangaza ni nyie wapambe kushupalia haya mambo, Sijawahi kumsikia Samia hata siku moja akimuongelea vibaya Magu, zaidi ya kummwagia sifa!! Siku Samia akiongea chochote kibaya kuhusu aliyekuwa bosi wake hapo mnaweza kuja juu na kutoa mapovu
Nani anapambana kumtetea?

Magu atajitetea mwenyewe kwa matendo yake.

Yani watu wameshindwa kutoa huduma ya umeme alafu lawama anatupiwa Magu ambae tulipata umeme wa uhakika kipindi chake chote?
 
By Zitto kupitia twitter:

Mradi wa 300MW Mtwara ulisimama. Mradi wa 350MW Kilwa ulisimama. Mradi wa nyongeza Kinyerezi 185MW ulisimama. Mradi wa Kinyerezi 3 and 4 umesimama. Utapata wapi Umeme kulisha nyongeza ya shughuli za Uchumi baada kufungua Nchi?

Miradi yote ya Umeme iliyokuwa kwenye power system master plan ilisimama kupeleka hela kwenye Stigler’s gorge ambayo wataalamu wote walituambia itachukua Miaka 7 kukamilika 100%.Lakini Kwa kuwa Sisi ni Watu wa kukubali uongo na propaganda tukaamini. Leo tunaambiwa delays tunawaka.

Siamini kuna hujuma. Ninaamini ni mambo ya kisera na madhara ya Miaka 5 unusu ya incompetence katika uendeshaji wa Uchumi. Tulidanganywa na tukaamini uongo huo. Sasa tunatumia uongo ule kuwapima wenye Mamlaka sasa. NCHI HAINA UMEME WA KUTOSHA. Hatujaongeza Hata 1MW kwa Miaka 5
Uzuri watanzania sio wajinga na wapumbavu kama bavicha
 
Tofauti, lakini yanatokea kipindi kimoja.....Why hayo matatizo yote yatokee kipindi kimoja? Kwa nini miaka yote hayajatokea kwa pamoja namna hii? Lazima kuna common cause inayounganisha hayo matatizo dunia nzima
Kukosa kwao umeme hakuhalalishi na sisi tukose umeme huku.

Hao sababu zao ni tofauti kabisa tena za kisomi, hizi za hapa kwetu ni za kipumbavu.
 
Uk.jpg
 
Kwa hiyo wewe unamwamini.nani akisema kuna kitu flani basi unamwamini lakini kwa tanzania huamini?
Binafsi, huwa siamini mwanasiasa yeyote na ndo maana posts zangu ni nadra sana ukute natoa reference kutoka kwa wanasiasa!!

Kinyume chake, naifahamu Power Master Plan, na kuna siku hapa niliweka sehemu yake!

Kwa mfano, baada ya kujenga bomba, ilitakiwa pajengwe vituo 4 vya kuzalisha umeme pale Kinyerezi kwa sababu gesi ilishavutwa!!

Katika vituo 4 hivyo, JK alijenga kituo kimoja, na kingine kikawa kwenye mchakato! Ilitarajiwa Magu akiingia amalizie vituo 3 vilivyobaki!! Hadi umauti unamkuta, alijenga kimoja TU ambacho tayari mchakato wake ulishaanza, vingine vyote akapiga chini na kuhamia kwenye Bwawa la Nyerere ambalo tulitakiwa KUANZA MWANZO!!

What do you expect?

Na ingawaje watu mnaleta masihara sana, hadi sasa umeme wa gesi ni 57% ya umeme WOTE uliopo kwenye grid ya taifa!! Ulishawahi kujiuliza endapo Magu angejenga vituo vyote, hivi sasa kungekuwa na umeme kiasi gani kwenye grid ya taifa?!

Huku mkishangilia umeme wa maji, huku mkidanganywa kwamba mgao wa wakati wa JK ulitokana na watu kuziba maji, lakini ukweli ni kwamba umeme wa maji ni 36.6% TU!

Hapa chini ni Ripoti ya Wizara ya Nishati zama za JPM....
Power.png

Kumbe, ingawaje nchi ilikuwa inategemea zaidi umeme wa gesi, lakini bado tukatelekeza mradi wa ujenzi wa vituo vipya vya kuzalisha umeme pale Kinyerezi!!

Sasa unatarajia nini ile 36.6% tunayotegemea kutoka kwenye chanzo cha maji, inapokumbwa na changamoto ya ukame?! Au unakataa kwamba hakuna ukame?! Au unakataa kwamba vyanzo vya maji vimepungua?!

Na huyo aliyewahi kusema "tuna umeme mwingi" alizingatia kwamba kila siku wateja wapya wa umeme wanazaliwa, na matumizi ya umeme yanaongezeka?!
 
Kuna mitambo ililetwa ya kuzalisha umeme wa gesi kama huelewi nenda kaulize tanesco na ndio maana walizima mitambo ya mafuta baada ya kukamilisha ujenzi wa hiyo mitambo na kupanua kinyelezi one na two ili kuongeza mgwt,
Kaulize huko tanesco kama hujui.
Sasa hiyo so ndo Kinyerezi II ambayo nimekuambia ndiyo alijenga JPM, bila shaka kwa sababu alikuta tayari mchakato umeshaanza!!

Je, Kinyerezi III na Kinyerezi IV ilishajengwa?
 
JPM, tuombee kwa Mungu, unatamani urudi duniani ila mapenzi ya Mungu yalishatimia. Ama kweli tunakukumbuka kwa mazuri.
 
Kukosa kwao umeme hakuhalalishi na sisi tukose umeme huku.

Hao sababu zao ni tofauti kabisa tena za kisomi, hizi za hapa kwetu ni za kipumbavu.
Sababu ipi ya kipumbavu? Ukisema sababu ya Climate change ya kipumbavu (Which means kutumia umeme wa maji ni upumbavu) then hoja ya Zitto ina mashiko
 
Kukosa kwao umeme hakuhalalishi na sisi tukose umeme huku.

Hao sababu zao ni tofauti kabisa tena za kisomi, hizi za hapa kwetu ni za kipumbavu.
Na ninaweza kusema kuwa ni Upumbavu wa CCM wote, kwani haiwezekani miaka 60 yote (Haijalishi nani alikuwa Rais au Serikalini) wameshindwa kutafuta chanzo kingine cha umeme zaidi ya hiki kimoja wanachokitegemea!! Ni upumbavu wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli pamoja na wasaidizi wao wote waliounda serikali zao!!!
 
Back
Top Bottom