Mjue mtu kabla ya kumlaumu. Kwa muda mrefu sijachangia hapa JF. Na cha ziada nilichofanya ni kuwa One man family.
Pole kama ulikumbwa na maswaiba
Bin Maryam, it's been a while, welcome back. Hiyo habari ya Poland kuzalisha umeme zaidi ya Afrika combined inahuzunisha sana....
Afrika bara zima na utajiri wote huo?Binafsi naamini tunahitaji viongozi wenye mawazo mapya,viongozi wenye mawazo kama Rev Kishoka na wengi tu humu JF, tunaweza kuona kuna pengo kubwa sana,hakuna kiongozi wa kutuvusha kwenye kipindi cha mpito ambapo Afrika ni lazima inegehitaji mwelekeo mpya,viongozi wapya wenye mawazo mapya na ya tofauti yenye kuendana na wakati tuliopo, viongozi tulio nao ni wale wale wenye mawazo yale yale.
Kubwa na baya zaidi ni tatizo la kuomba omba na wakati utajiri wa rasilimali unatolewa kwa mlango wa nyuma kwa maslahi binafsi,na nishati tulizo nazo hakuna anayejisumbua kila siku ni kufikiri wapi kiguu na njia kuomba na kutalii tuu!
Hakuna kufikiri kuhusu mustakabali wa wananchi na mwelekeo wa Taifa kwa ujumla, mabadiliko ni lazima, mabadiliko yatakayopelekea mwamko kwa wananchi ambao nao hawajui kuwa kuna rasilimali za kutosha kutuondoa kwene umasikini, na wao pia wameadapt kuridhika na umasikini na kuomba omba....
Mpaka tutakapoweza kuwatumia wale viongozi wenye ability ya kuona hilo pengo na kufikiri pamoja na kutenda kinyume na reflection ya wananchi hence revolution....Ndio maana umeona mara nyingi kumekuwa na madikteta Afrika, maana hata Nyani Ngabu ana ubavu wa kusema ndivyo tulivyo, imagine mtu kama huyo awe Rais.
Naamini bado tunaweza kupata viongozi ambao si madikteta lakini wenye kuweza kuchochea mabadiliko ya kijamii na kiuchumi Afrika Tanzania ikiwemo.