Kwanza sina budi kukupongeza Mheshimiwa Dewji kwa kujumuika nasi hapa jamvini.Laiti tungekuwa na viongozi wa CCM japo watano tu wenye mtizamo kama wako basi tungeweza kupiga hatua kidogo.Kuna usemi wa busara kwenye stadi za siasa unaosema kwamba wanasiasa mahiri hupendelea mijadala kwenye hadhira yenye potential ya kutoafikiana nao.You truly have shown the way to your fellow wana-CCM but sitrajii kuone the like of Rostam,Lowassa,Sofia Simba,etc kujumuika nasi hapa unless "ramli" ziwajulishe kuwa kuna votes which their money can't buy.
Pamoja na kuafikiana na mtazamo wako lakini nadhani umekwepa kuangalia kikwazo halisi cha kufanikiwa kwa mipango yetu mingi ikiwa pamoja na katika sera ya nishati iliyogeuzwa "shamba la bibi",kila mwenye mbinu ya kuiba anataka kuweka mkono wake hapo.My point is,hakuna mpango wowote wa maendeleo utakaofanikiwa pasipo kudhibiti ufisadi.Tutakuwa wendawazimu kutaraji upatikanaji wa umeme wa uhakika ilahi asilimia kubwa ya waliotukwaza huko nyuma wanaendelea kubaki sehemu muhimu katika uandaaji na utekelezaji wa mipango hiyo.
Hivi Mshehimiwa Dewji,unadhani wakijitokeza wafadhili wa kutoa fedha za kuboresha sekta ya umeme,wezi wa Richmond hawatapenyeza watu wao kuhakikisha wanapiga panga sehemu ya fedha hizo?Kumbuka kwamba Mwenyeketi wako,ambaye ni Rais wetu,Jakaya Kikwete,aliwahi kutuahidi kuwa tatizo la umeme lingekuwa historia.Wapo waliomwamini kwa vile alishawahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini ambapo sekta ya umeme inaangukia humo.Matokeo yake tukaletewa majambazi wa Richmond.
Mipango ya muda mrefu haiwezi kufanikiwa iwapo watawala wetu wanataka kuishi kama wewe mfanyabishara uliyejijenga kwa muda mrefu.Naomba nieleweke kwamba hapa sikutupii dongo wewe bali namaanisha kuwa maisha ya watawala wetu hayaendani kabisa na hali halisi ya nchi yetu.Ninyi wafanyabiashara mna kila sababu ya kuendesha magari ya thamani kubwa,majumba ya kifahari,samani za bei mbaya,nk kwa vile ni matokeo ya jitihada zenu binafsi (exclunding ndoa ya mafisadi na watawala).Nchi ni kama familia,iwapo baba atataka kuvaa suti za bei mbaya ilhali uwezo wake ni duni basi ni dhahiri masuala kama ada za shule za wanawe au hata mlo hapo nyumbani itakuwa ni tatizo.
Halafu kingine ambacho naweza kukiita kama ushauri kwako ni kwamba mwenzetu uko katika nafasi ya ku-initiate change (of course,kwa kushirikiana na wazalendo wengine).Je hufikirii kwamba mawazo haya mazuri uliyonayo yanaweza kuwa even more productive iwapo utajaribu kuyasambaza kwa baadhi ya wanasiasa wenzio tunaowafahamu kama wanaopenda nchi kwa dhati (or at least that's how they portray themselves)?
I strongly believe kuwa unaguswa kwa dhati na matatizo yanayoikabili nchi yetu japo nafasi uliyonayo kama mbunge wa CCM inakwaza your full potentials.Kadhalika natambua kwamba mazinigra ya baishara katika nchi zenye nunu-demokrasia yanakuwa magumu iwapo mfanyabiashara hataonyesha kuafikiana na kila mtazamo wa chama tawala.Sasa kwa vile CCM imeshajitambulisha kuwa ngome muhimu ya ufisadi,napata shida kuona namna mawazo yako mazuri yatakavyoweza kuzaa matunda yanayokusudiwa.
Generally,kuna wanasiasa wanaoguswa kwa dhati na matatizo yanayoikabili nchi yetu lakini kinachowakwaza ni unity yao na CCM.Nadhani tunahitaji sana wazalendo wanaoweza kujitoa mhanga kwa manufaa ya nchi,na hiyo ni pamoja na kuweka maslahi ya taifa mbele badala ya kuendeleza itikadi za siasa.If you try that,Mheshimiwa Dewji,I'll be the first to shout aloud "MOHAMMED DEWJI FOR PRESIDENT OF TANZANIA"