hii article yako yote umeitoa NY times halafu umeitafsiri, sio kitu kibaya lakini unge wa acknoledge. usiposema source watu tunaona ni plagiarism.
link hii hapa
Hatujawekeza ipasavyo kwa miaka 15 hadi 20 katika kitengo cha uzalishaji na usambazaji wa umeme, hayo maneno yalitamkwa na Lawrence Musaba, Meneja wa Southern African Power pool, muungano na mtandao wa nchi kumi na mbili kusini mwa Sahara.
Ukiitoa nchi ya Afrika Kusini kwenye mambo hayo, nchi zote zilizobaki za kusini mwa jangwa la Sahara lenye watu milioni 700, linapata umeme sawa na wananchi wa Poland ambao ni milioni 38 tu.
http://www.nytimes.com/2007/07/29/world/africa/29power.html
hii ndio article ya kiingereza ambayo umetafsiri kwa kiswahili. maneno haya yafananishe na hapo juu
"We've had no significant capital injection into generation and transmission, from either the private or public sectors, for 15, maybe 20 years," said Lawrence Musaba, the manager of the Southern African Power Pool, a 12-nation consortium of electricity utilities at the continent's tip.
The gravity of this year's shortage is all the more apparent considering how little electricity sub-Saharan Africa has to begin with. Excluding South Africa, whose economy and power consumption dwarf other nations',
the region's remaining 700 million citizens have access to roughly as much electricity as do the 38 million citizens of Poland.
http://www.nytimes.com/2007/07/29/world/africa/29power.html
hii article inanikumbusha uk 2007 nikiwa nimekaa na watu kutoka kenya, uganda, nigeria, ghana, ivory cost na cameroon tukawa tunajidili jinsi waandishi wa habari jinsi wanavyoiandika vibaya africa na effect zake kwenye tourism na kuzuia investment flows. niliposoma hii ya kwako kwa kiswahili nikajua tu utakuwa umeitafsiri, nikatumia kama nusu saa kuitafuta mpaka nikaipata.
mo ukisoma hizi habari au research paper yeyote lazima uingalie kwa makini
na uitafakari. "
the region's remaining 700 million citizens have access to roughly as much electricity as do the 38 million citizens of Poland".
huu ni uongo wa hali ya juu ambao unaandikwa na waandishi wa habari wa nje juu ya africa, kina chosikitisha na wewe ume copy na ku paste na kuja kutulisha hapa JF. huyu mwandishi ni watu ambao wanakuja mara moja tu africa na kuondoka na hawajui hali ya africa na kazi yao ni kuandika negative about africa.
ukiangalia TZ peke yake tukasema dar na mwaza kuna umeme, kwa ajili sio kila mtu ana umeme katika mikoa hii miwili kwa hiyo tuseme mikoa mingine yote ya tz haina umeme (arusha, mbeya, kilimanjaro, tanga na kwingineko kote hamna umeme). watu wa dar + mwanza ni 8mil, kwa hiyo ni watu mil 8 out of 40m wana access to electricity which is 20% of all tanzanians.
nimetembea kenya sehemu mbali mbali, na kenya watu wengi wana umeme zaidi ya tanzania.
jamaa zangu wa nigeria, ghana, ivory cost, cameroon na uganda walinitolea mifano hiyo hiyo na wakanihakikishia kuwa more than 20% of their pop has access to electriicty. ukijumlisha 20% ya inchi zote utaona inapita 38mil by miles.
hata UN estimate ni 12% which is 84mil.
tuachane na data turudi kwenye mada
tatizo kubwa ambalo linaikabili sekta ya umeme africa ni uongozi/corruption. nchi za africa zina viongozi ambao wanafikiria matumbo yao tu na si kutatua matatizo ya watu waliowapigia kura.
mfano ethiopia wanajenga bwawa kubwa sana la umeme (huu ni mpango wa long term) lakini shutuma ndio zile zile kwamba ni hela nyingi imeliwa na hela pia haitoshi.
http://news.bbc.co.uk/1/hi/world/7937480.stm
tukienda nigeria obasanjo na wenzake wametafuna karibuni $2bn ambazo zilikuwa zitumike kwenye umeme.
tukirudi dar rashid ametuambia tusiponunua mitambo ya rafiki yako dowans tutakaa kwenye giza, hii ni dhairi kabisa watu hawataki kufanya mipango ambayo haifaidishi matumbo yao.
karibu JF