Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Hiyo EIA imefanywa na nani ikafikia hitimisho hilo?Mzee Mwanakijiji.
Mradi huo wa Stiegler Gorge ni bomu. Gharama yake kimazingira itazidi faida ya huo umeme. Athari yake kwenye Ruaha basin na Rufiji delta ni kubwa mno.
Kama huna cha kuchangia bora ukae kimya na sio kuja kuharibu thread hapa. Hoja hapa ni kupata uvumbuzi wa kudumu wa tatizo la umeme. Hii ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa sasa na kutafuta vyanzo vingine vya umeme.
Mzee Mwanakijiji.
Mradi huo wa Stiegler Gorge ni bomu. Gharama yake kimazingira itazidi faida ya huo umeme. ........
Mkuu, wewe ndiye uliyemuingiza Idriss humu. Hamna cha rhetoric whatever. Usitake kukwepa responsibility kama anavyotaka kufanya huyo unayemtetea.
Tatizo sio kuwa matengenezo yalikuwemo kwenye bajeti au la. Tatizo ni item kama ya maua ya plastiki iliingiaje kwenye hiyo bajeti. Tatizo ni kuwa katika wakati huu mgumu, kiongozi makini anaweza kupeleka maombi kama hayo kwa bodi yake? Kupitishwa na bodi si hoja. Bodi zetu mara nyingi zinategemea fadhila za menejimenti au unadhani vibahasha vinatoka wizarani au bungeni?
Wakati mwingine tunahitaji kubomoa kabla ya kujenga. Hapa hakuna anayemchukia Dr. Idriss kama mtu bali tuna kila haki ya kupinga kuwa anastahili kuendelea kama ilivyo kwako kumtetea kuwa anafaa.
Amandla.......
Wabunge ndio hupitisha mipango ya muda mfupi na ya muda mrefu ya serikali na ni wao huitengenea fedha. Na pale ambapo hakuna sheria ya kusababisha jambo fulani kufanyika wabunge wana uwezo (kama kundi -chama, au kama mtu mmoja mmoja) kuleta mswada wa sheria wa kusababisha jambo hilo kutendeka au kutotendeka.
Suala la tatizo la nishati siyo geni kwa TAnzania na kwa eneo letu la Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara. Kwa upande wetu Tanzania tatizo hili ni dalili tu ya tatizo lenyewe tulilonalo ambalo ni mipango mibovu ya wanasiasa wetu. Tanzania haina sababu hata chembe ya kuwa upungufu wa nishati ya umeme.
Leo hii kuweza kuyarejesha mabwawa yetu yote ya kuzalishia umeme kwenye full capacity inakadiriwa kutumia karibu dola bilioni 2! Lakini tukifanya hivyo zaidi tutakachopata ni kama Megawatts 1000 hivi (kama sikosei). Lakini wakati huo huo tukitamua kujenga bwawa moja kubwa la Stielger's Gorge itatugharimu karibu dola bilioni 2 vile vile lakini tunaweza kupata Megawatts zaidi 2900!
Wanasiasa wetu hawajui wachague nini! suluhisho lao ni kuingiza majenereta ya umeme na kutoa tenda zaidi ya majenereta. Wako tayari shilingi milioni nyingi kila siku na ukiwauliza hadi leo (kuanzia 1995) serikali imetumia kiasi gani katika kulipia mafuta na IPPs, jibu lake litawafanya muinamishe kichwa kwa aibu!
Sasa, Mhe. Dewji,
a. una mpango gani wa kuleta mswada Bungeni wa kusababisha ujenzi wa Stielger's gorge au kutengea fedha mradi huo mkubwa ilii hatimaye tuondokane na tatizo la umeme?
b. Una msimamo gani kuhusu kampuni ya Dowans ambayo iliingia nchini kitapeli na hadi leo tunahangaika na majenereta yao. Je, kwa maoni yako serikali itaifishe mitambo hiyo na kuwachukulia hatua wahusika wote?
c. Unafikiri Kamati yenu Teule ya Bunge ilifanya kazi yake vizuri katika suala la Richmond na hivyo kazi yake iheshimiwe na wabunge wote au unaamini ilikuwa imewaonea watu mbalimbali?
mpango wao ndio huo!
Fundi na Mo nashukuru kwa michango yenu/post na wachangiaji wengine walio toa Point endelevu,
Sasa Fundi mimi ningependa kuulizia Hii EIA ya Three Gorges kule China ilikuwaje Vs kujenga Nuklia Power Station maana wenzetu wana weza?
Pili Mo wewe ukiwa kama mbunge wa Singida, na kwa kuwa serikali kwa hivi sasa wamejikita zaidi katika kuwekeza kwenye Miradi midogo midogo ya MW 100 nk
je umefanya nini kushauri wadau binafsi kama wewe, au halmashauri ya Mji wa kauza Shares ilikupata mtaji wa kufungua katanesco kadogo hapo Singida, na mkiona Mtaji unao hitajika ni mkubwa, basi mnaweza omba mitaji toka nje ya Singida, na kutoka kwenye institution zingine kama world bank, na watu wa moja moja hapa Bongo na Nje?
Ili mradi shares ziwe zinauzwa pale DSE
Salaam JF,
Kuna msemo hapa wa Waafrika Ndivyo Walivyo. Mtoa mada ametoa takwimu moja nzuri sana. Mojawapo ni kuonyesha kuwa ukiondoa South Afrika ambayo nayo ina matatizo ya umeme, nchi zilizobaki zina matatizo makubwa ya nguvu za umeme. Na vilevile ameonyesha kuwa Poland inazalisha umeme kwa kiwango kikubwa kuliko nchi za kiafrika combined.
Hili suala sio la kisiasa. Japokuwa wanasiasa ndio waliochika ufunguo wa kutatua matatizo haya na mengine yaliokuwepo ya kijamii.
Mtamlaumu Kikwete, Idrisa, Nyani Ngabu mnavyotaka lakini ufumbuzi wa matatizo ya umeme unahitaji collective efforts. Miongoni mwa collective efforts ninazopendekeza:
1./ Vyanzo vya umeme wa maji sasa hivi havitabiliki. Hivyo ni lazima tujifunze kukabiliana na matatizo ya hali ya hewa.
2./ Ongezeko la watu nalo linasababisha upungufu wa upatikanaji wa umeme. Nchi nyingi za Ulaya zina ongezeko ambalo ni asilimia -1% au 1%. Hivyo kwa miundo mbinu ya miaka 20 iliyopita nchi za Ulaya zinaweza kupata umeme bila matatizo. Hiyo tuchague kukabiliana na ongezeko la watu au kuwa na sera zenye kwenda sambamba na ongezeko la watu.
3./Hakuna nchi inayofaidika na umeme bila kuwa na watu waliosoma sayansi na mathematics vizuri. Sasa hivi tunavuna mipango mibovu ya elimu tuka tumepata uhuru. Elimu ya darasa la saba haitoshi.
4./ Watanzania tuache biashara za uchuuzi na ulanguzi na kujiingiza kwenye biashara za innovations. Ingawaje serikali nyingi zinadhamini uzalishaji wa umeme, ni sekta binafsi iliyogundua. Nikola Tesla, Thomas Alva Edison walifanya uvumbuzi katika sekta binafsi.
5./ Vilevile ziwepo sera za maendeleo ya jamii ambazo zitazingatia miji iliyopangwa na sio kujengwa ovyovyo kama uyoga. Miji iliyopangwa inasaidia usambazaji na ukusanyaji wa mapato ambayo yataendeleza sekta ya umeme.
6./ Ushirikiano na nchi zingine katika maeneo yetu unaweza kutatua matatizo ya umeme kwa haraka. Kama kuna uwezekano wa kuanzisha shirika la nyuklia la nchi za Afrika mashariki na kati. Inakuwa bora zaidi. Na vile vile nchi ku-share mgao wa umeme. Kama Kagera inaweza kupata umeme kutoka Uganda, basi wasisubiri umeme wa Kidatu.
7. Na mapendekezo mengime ..........
Mawazo yako ni sawa...lakini...whats next? Utandaji vipi? Wewe binafsi unaishia hapa JF na keyboard au unafanya nini cha ziada? Tunahitaji kuwa na impact kubwa zaidi ama sivyo hatutakuwa tofauti na hao wanasiasa.
Pole kama ulikumbwa na maswaiba Bin Maryam, it's been a while, welcome back. Hiyo habari ya Poland kuzalisha umeme zaidi ya Afrika combined inahuzunisha sana....Mjue mtu kabla ya kumlaumu. Kwa muda mrefu sijachangia hapa JF. Na cha ziada nilichofanya ni kuwa One man family.
Bin Maryam uko sahihi kwa kiasi kikubwa katika maelezo hapo juu!
Kimsingi mimi (na taasisi yangu) nimeanza na miradi midogo midogo ya umeme kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini (micro hydro electricity). Lengo ni kusaidia wakulima kuongeza kipato kwa kufanya agroprocessing pale pale walipo kwa kutumia umeme huu.
Umeme wa gridi haufiki maeneo ya vijijini kutokana na gharama kubwa za kuusafirisha, hivyo inakuwa ni hasara kwa Tanesco! Umeme huu mdogo ni rafiki wa mazingira. Hata Tanesco wana mitambo ya namna hii, kama ule wa Uwemba Njombe, Tosamaganga na Mbalizi.
Polepole tutafika.
Na ndio maana na mimi nasisitizia wadau wakila sehemu. iwe wabunge, wafanya baishara, halmashauri etc etc wajikite katika kuhamasishana katika kutatua tatizo la umeme sehemu zao, kwa hii ndio itaongeza vipato na kuchochea maendeleo sehemu zao. na pia kuongeza ushindani wa kibiashara na hata kukuza soko letu la mitaji.Haya ndiyo maneno. Hii ndiyo miradi niliyokuwa nikizungumzia siyo hiyo ya Stiegler Gorge. Miradi hiyo itawafaidia makonsaltant na wala 10%! Mwananchi wa kawaida ataishia kulipia gharama ya madeni tutakayoingia na kupandishiwa bei ya luku kila kukicha.
Ni lazima tubadilishe mwelekeo.
Amandla........
Engineers (FM nadhani ni mmoja wao) huwa tunaamini kwamba always tunaweza kuja na sustainable solution which meets the present needs without compromising the environment or future generations. Kuna faida gani kuacha maji yatiririke tuu hadi baharini kisa species fulani za samaki, vyura etc. zitaangamia. Watu wa environment tunawajua sana - huwa wanapinga kila kitu - nuclear, hydro, fossil enegy. Technologies za kuzalisha substantial solar/wind energy bado sana na ni ghali.
Tusisahau vilevile kwamba kuna faida zingine kiuchumi zaidi ya umeme kwa kuwa na miradi kama hii. Itakomesha mafuriko, itaendeleza shughuli za uvuvi na hata utunzaji wa maji kwa ajiki ya kilimo cha kuwagilia, etc. Chukua mfano wa Hoover Dam/mto Colorado ilivyosaidia ustawi wa Maeneo ya Las Vegas NV & Central Valley (California). Unaambiwa hakuna hata tone na maji ya mto Colorado yanayofika Atlantic ocean. Haya tuna mifano yetu ya Mtera & Nyumba ya Mungu na faida zake kibao.
Bin Maryam uko sahihi kwa kiasi kikubwa katika maelezo hapo juu!
Kimsingi mimi (na taasisi yangu) nimeanza na miradi midogo midogo ya umeme kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini (micro hydro electricity). Lengo ni kusaidia wakulima kuongeza kipato kwa kufanya agroprocessing pale pale walipo kwa kutumia umeme huu.
Umeme wa gridi haufiki maeneo ya vijijini kutokana na gharama kubwa za kuusafirisha, hivyo inakuwa ni hasara kwa Tanesco! Umeme huu mdogo ni rafiki wa mazingira. Hata Tanesco wana mitambo ya namna hii, kama ule wa Uwemba Njombe, Tosamaganga na Mbalizi.
Polepole tutafika.