Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

Habari wana Jamii naombeni Msaada nimekuwa nikisumbuliwa sana Na vipele kwenye kidevu Mara kwa Mara vipele hivi haviishi...nimejaribu kunyoa Ndevu kwa kutumia wembe ,Magic powder hata Machine na kupakwa After shave lakini wapi haviishi ...Msaada dawa gani itanisaidia
 
Nilijaribu kutumia dawa zaidi ya aina 45 kwa nyakati tofauti tofauti bila kupata tiba ya vipele vya ndevu.
Dawa iliyobaki ni kunyoa bila kuzimaliza zote,yaani hukwangui zote.
Kila la kheri
 
Nilijaribu kutumia dawa zaidi ya aina 45 kwa nyakati tofauti tofauti bila kupata tiba ya vipele vya ndevu.
Dawa iliyobaki ni kunyoa bila kuzimaliza zote,yaani hukwangui zote.
Kila la kheri
Asante sana Ngoja niache zikue nikinyoa nifanye hivyo....Asante sana
 
Asante sana Ngoja niache zikue nikinyoa nifanye hivyo....Asante sana
Nilitumia bump patrol kama chupa 20 lakini wapi
Nilitumia aina tofauti za sabuni za kukausha vipele lakini wapi
Nilitumia dawa kadha wa kadha za hospital lakini wapi
Vitunguu,limao,mawe ya bahari nimepaka sana lakini wapi!

Nikaamua kuanza kunyoa na kuzibakiza kidogo(kisha napitisha maji ya uvuguvugu) huku zikichongongwa vizuri na nazipaka mafuta yake vipele haviji na naonekana smart tu.
 
Usinyoe wakati bado ndo zinaanza kuota subiria zikuekue ndo Usinyoe na baada ya kunyoa unaweza Kanda kidevu kwa maji ya moto. hata nilitumia dawa nyingi hazikunisadia.
 
uwe unazipunguza tuu sio kuzinyoa zote hiii huwa ndo solution ya vyote katika yote
 
Kwa mda mrefu sana mm nimekuwa nikisumbuliwa sana na tatizo hilo. Lkn kupitia jumba hili la jf nilipata tiba.

Niliuona ushauri kwamba osha vzr kidefu kabla hujanyoa. Tena tumia nyuzi na sabuni kuonsha kidevu. Sugua kuhakikisha mafuta/lotion uliyojipakaa imetoka yote. Kisha kausha kedevu vzr na nyoa kwa wembe mpya. Usirudie mara nyingi wembe huo ktk kunyoa (mwanzo utumie wembe mara mbili tu)

Nikatekeleza hayo masharti. Na sasa sina shida kabisa. Kuna wembe unaitwa BICK, jaribu huo mkuu unaweza kusaidia

Lakini kumbukumbu yawezi isiwe suruhisho kwa sababu matatizo ya ngozi yanatofautiana.
 
Wakuu kwa wanasumbuliwa na vipele mmewai kutumia hii sabuni ni nzuri sana aixe mi vipele vyote kwishaa
 
Tumia rungu max mimi imenisaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…