Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

Hii shabu inauzwa maduka gani??? Ya dawa auu

Mkuu,

Pitia mitaa ya soko lililo karibu na wewe.

Ukikosa basi tembelea maduka ya dawa za asili.

Tumia halafu leta mrejesho

Shukrani
 
Mkuu,

Pitia mitaa ya soko lililo karibu na wewe.

Ukikosa basi tembelea maduka ya dawa za asili.

Tumia halafu leta mrejesho

Shukrani
Sio Mimi nnae enda kutumia
 
Mimi nilihangaika sana na hilo tatizo kwa muda mrefu. Nikaamua hivi. Kila nikimaliza kunyolewa ndevu, kinyozi ananikanda na maji ya uvuguvugu na sabuni yoyote ya dawa. Mpaka leo ni miaka mingi imepita sijawahi kupata vipele.
 
Msaada wakuu,
Saivi nikinyoa ndevu natoka mapele utadhani kikoi cha jasusi. Hii ni hususan nikitumia shaving mashine, angalau kidogo saluni. Naombeni msaada wazee, mtu unaonekana smart usoni lakini kidevu kimechakaa kama soksi za mwamnyeto
 
Kuna sehemu nilisoma..unanunua Asprini..unayeyusha na maji KIdogo alafu unapaka eneo husika baada ya kunyoa..

Jaribu
 
Msaada wakuu,
Saivi nikinyoa ndevu natoka mapele utadhani kikoi cha jasusi. Hii ni hususan nikitumia shaving mashine, angalau kidogo saluni. Naombeni msaada wazee, mtu unaonekana smart usoni lakini kidevu kimechakaa kama soksi za mwamnyeto
Hii siyo ya ndevu, ila inafanya kazi.

Kama unaweza kuipata, chukua yenye 2% Salicylic acid.

Kwangu inafanya kazi vizuri sana.

C4C37AD4-EE8A-4792-BDAA-B7CDC3B618AA.jpeg
 
Nina uhakika na Ni effective kabisa. Ila Kama anamashaka atafute njia Nyingine.

Ila Aspirin ukiyeyusha unachukua na kakitambaa kasafu au pamba.. unapaka
Yaan unachovya Yale maji yenye aspirin na pamba unapaka kidevuni?
 
Sijui unatumia nyembe zenye ubora gani. Ila mimi natumia nyembe mpya, double blade, au triple, original, napaka sabuni kidevu nanyoa.

Swaafi kama cha mtoto miaka lukuki.

Sasa natafuta shaving cream ya kupaka tu...nisubiri muda, nikiosha kwa maji ndevu ziwe hakuna.

Kuna anayeijua?
 
[emoji3][emoji3][emoji3]kikoi cha jasusi.

Daah pole mkuu.ila ninavyojua hutakiwi kukwangua ndevu zote.nyoa saluni na umwambie asirudie rudie sana.
 
Back
Top Bottom