Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

Tatizo la upele Kidevuni: Chanzo na matibabu yake

Ukimaliza kunyoa chemsha maji adi yawe ya moto sana. Chukua taulo Au kitambaa laini chovya kwene ayo maji jikande kidevuni. Hakikisha joto linapenya sawasawa kwene ngoz ya kidevu. Kama Kuna madonda akikisha ayo maji unayaweka chumvi.
 
Tafuta vidonge vya paracetamol, vitwange hadi viwe kama poda kwa kadiri ya mahitaji yako, then baada ya kushave paka sehemu husika kama poda. thanks me later
 
Kama huna after shaving lotion, tumia "tincture iodine" ni ile dawa ya madonda mabichi, chukua Cotton bud na chovya katika hiyo tincture iodine na pakaze sehemu yenye upele (kidevuni) baada ya kunyoa au hata kama hujanyoa, hii dawa pia inaweza kutumiwa na wale wanaisumbuliwa na vipele chini ya kichogo baada ya kunyoa nywele. Ila usipokuwa muangalifu unaweza kuchafua nguo zako, unatakiwa uwe mwangalifu usichafue nguo nk,

Hii "tincture iodine" pia hutumika kuondoa "skin tags" (viotea kwenye ngizo), watu wengi hawajui kuwa hii sio dawa kwa ajili ya madonda mabichi pekee.

Dawa nyingine ya kuondoa vipele ya ndevu:- chukua kikopo cha mafuta mgando (petroleum jelly etc) changanya na vijiko 3 vya asali mbichi na vijiko viwili vya Mafuta ya nazi, koroga huo mchanganyiko na uwe ukipaka kila baada ya kunyoa ndevu.

Pia hakikisha kila unapotaka kunyoa hiyo mashine yako uifanyie sanitazation na methylated spirit nk, pia tumia nyembe zilizokuwa standard zilizokuwa na hadhi kama Gillette au Laser nk. hope help.
Asante mkuu
 
Mkuu nakupa dawa imenisaidi Sana hakika utanikumbuka tumia KIBIRITI UPELE unapo maliza kunyoa paka kidevu chote zinapoishia ndevu,usiache kuleta marejesho
Naipataje hiyo mkuu
 
Ukiweza kupata hii kitu umetatua tatizo. Nilikuwa na shida hiyo kwa miaka mingi na hili ndio likawa suluhisho.

Naipataje hiyo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakuu vip swala la vipele vinavyotoka kwenye masharubu ,naomba msaada

je kunyoa unaanzia juu au chini na njia ya kutibu ni ipi..?,,siyo siri vipele vya masharubu vinanikela sana yaan mtu unakuwa kama kinda la ndege
 
Angalia video hiyo hapo juu kisha fuata maelekezo kwa umakini na tatizo la vipele vya ndevu litaisha kabisa
 
Mkuu unatumia wembe ? kama unatumia wembe acha tumia mashine kama wanazotumia vinyozi. baada hapo pakaza B&C SKIN TIGHT ni kiboko hii kesho yake tu ukiamka utaona tofauti.endelea siku mbili tatu vitapotea kabisa acha kutumia siku ukikata ndevu tena pakaza kidogo hivyo hivyo na utaona tofauti yake.
Hii yapatikana duka gani kwa jiji la Dar
 
Ukimaliza kunyoa chemsha maji adi yawe ya moto sana. Chukua taulo Au kitambaa laini chovya kwene ayo maji jikande kidevuni. Hakikisha joto linapenya sawasawa kwene ngoz ya kidevu. Kama Kuna madonda akikisha ayo maji unayaweka chumvi.
Hii inafanya kazi vizuri sana
 
Nimesumbuliwa sana na vipele vya ndevu hadi nikaamua nisinyoe kabisa, angalau sasa nimekuwa na amani ingawa ndevu zimejaa sana.

Sent using Samsung J1
 
Nasumbuliwa na vipele baada ya kunyoa ndevu shingoni. Before nlikuwa natumia Skderm lakini sioni kwa sasa tena ikinifaa. Nadhani imeshanizoea.

Matumizi ya spirit pia after shaving hayajawa na manufaa kwangu. Napomaliza kunyoa kesho yake najikuta kuna vipele vingi shingo hadi chini ya taya. Binafsi napendelea kuondoa ndevu zote za chini na mustache pia nikiacha tu sharafa.

Naombeni solution ya hili ili nibaki kuwa na ngozi yangu laini kama awali. Natumia Gillete kunyolea na sometime machine hizi za kisasa cha kucharge. Bado shida inakuwepo. Msaada please.
 
Tupo wengi
 
Back
Top Bottom