Tatizo la Upinzani Tanzania ni kukosa itikadi

Tatizo la Upinzani Tanzania ni kukosa itikadi

Besta Mlagila

Senior Member
Joined
May 29, 2018
Posts
101
Reaction score
192
Tatizo kubwa la upinzani wa Tanzania ni kufanya siasa za mazoea na mihemko, vyama vinashindwa kujenga wanachama kwa mifumo ya kiitikadi.

Pia vimeshindwa kutafuta wanachama kwa Makundi ya Vijana wa Vyuo, waliokosa ajira au wenye matatizo mbalimbali. Matokeo yake makundi hayo yanapotatuliwa matatizo yao hawataona umuhimu wa kuendelea kuendesha harakati na upambanaji kwasababu wanacho kihitaji wanakuwa wamekipata.

Ndio maana kila mwaka wa uchaguzi wanasiasa mbalimbali huama vyama vyao, wanajitokeza wanasiasa wapya, mikutano ya vyama inajaa lakini baada ya matokeo hutaona wakijitokeza na kuendeleza chama au harakati na hii inavingarimu vyama vingi vya upinzani hapa nchini.
 
Huko ndiko kukosa point kabisa, nani ana itikadi Tanzania kwa sasa?? CCM sasa hivi Neither Ujamaa wala Capitalism, wanafuata kokote kule, not defined. Chadema wamekosa resources, ukikosa resources unakuwa hauko organized kabisa. CCM wana resources, wana tumia pesa za serikali vile vile. Chadema hawana huo mwanya kabisa.
 
Tutazunguka sana,lakini tatizo kubwa ni uchu wa madaraka miongoni mwa viongozi wakubwa na wasimamizi wa vyama.viongozi wametanguliza maslahi yao mbele , lakini wakati wakuomba kura wana act as if wanatutetea kumbe uhalisia sivyo.... njaa kali sana jamani

■wananchi wengi wanahitaji mabadiliko tatzo viongozi
 
Kwenye mfumo wa communism/socialism/Marxism-Leninism/ujamaa, ni mapinduzi tuu ndiyo yanaweza kukitoa chama tawala madarakani. Na kama mapinduzi yakishindikana, nchi huwa zinagawanyika kwa mfano Ujerumani iligawanyika mashariki na magharibi na Korea iligawanyika kaskazini na kusini. Ni nchi moja zilizogawanyika kwa mifumo ya siasa. Tatizo siyo upinzani, tatizo ni mfumo wa siasa.
 
Nimecheka kwa nguvu huu utoto ulioandika hapa. Fungua katiba ya nchi yetu uone inasema kuwa nchi yetu ni ya ujamaa na kujitegemea, pitia kwa vitendo kinachoendelea humu nchini kisha uje ulete mrejesho.

Akitokea mtu asiyejua lolote akasoma huu utoto ulioandika hapa, anaweza kuamini una point. Ukifuatilia kinachoendelea kwenye siasa zetu ni maagizo yenye hila mbaya dhidi ya vyama vya upinzani vya kweli, kupitia kiburi cha madaraka ya urais.
 
Mm naona kwa sasa upinzani upo kwa ajili ya rika mbali mbali kujifunza na kupata uzoefu wa siasa lkn c kushinda uchaguzi na kuchukua madaraka kwa sababu ata ktk Mpira France vs USA ili mechi iwe fair marefa na Washika vibendera wanatoka nchi tofauti na hao wanaokutana,na sasa wameongeza na goal technology ili mchezo uwe fair zaid.

So kama Watoa maamuzi ya mchezo hawapo huru uwez kushinda kwa Haki au kufungwa kwa haki na hili upinzani wanalijua ndo maana mm nasema wanafanya mazoezi ya siasa na kuongeza vipato binafsi kwa njia mbali mbali.
 
Huko ndiko kukosa point kabisa, nani ana itikadi Tanzania kwa sasa?? CCM sasa hivi Neither Ujamaa wala Capitalism, wanafuata kokote kule, not defined. Chadema wamekosa resources, ukikosa resources unakuwa hauko organized kabisa. CCM wana resources, wana tumia pesa za serikali vile vile. Chadema hawana huo mwanya kabisa.
Hoja dhaifu, CHADEMA walikosa resource Mpaka wakamweka LOWASSA kugombea 2015 na kukigawa chama??? CHADEMA wamekosa resources mpaka wanachama wake kila siku wanahama chama??? Chadema wamekosa resources Mpaka sasa BAWACHA imepasuka??? Ukweli ni kwamba CHADEMA hakuna mfia chama wote wanatafuta maslahi ndio maana yasipokuwepo au yakipatikana kwengine wanasaliti chama
 
Nimecheka kwa nguvu huu utoto ulioandika hapa. Fungua katiba ya nchi yetu uone inasema kuwa nchi yetu ni ya ujamaa na kujitegemea, pitia kwa vitendo kinachoendelea humu nchini kisha uje ulete mrejesho.

Akitokea mtu asiyejua lolote akasoma huu utoto ulioandika hapa, anaweza kuamini una point. Ukifuatilia kinachoendelea kwenye siasa zetu ni maagizo yenye hila mbaya dhidi ya vyama vya upinzani vya kweli, kupitia kiburi cha madaraka ya urais.
Nchi yetu ni ya ujamaa na kujitegeme hivyo vyama vinatakiwa kuwa na Itikadi zisizokinzana na Katiba, Haya tuambizane Itikadi gani ya chama inahakisi Katiba ya nchi??
 
Huko ndiko kukosa point kabisa, nani ana itikadi Tanzania kwa sasa?? CCM sasa hivi Neither Ujamaa wala Capitalism, wanafuata kokote kule, not defined. Chadema wamekosa resources, ukikosa resources unakuwa hauko organized kabisa. CCM wana resources, wana tumia pesa za serikali vile vile. Chadema hawana huo mwanya kabisa.
CCM inaujamaa wa kubebwa na dola
 
Shida ya itikadi ni kwa vyama vyote Sio upinzani Wala chama tawala.wanasiasa wetu wamegeuza siasa sehemu ya kuvuna sio kutumikia watu kwa itikadi zao
 
Mm naona kwa sasa upinzani upo kwa ajili ya rika mbali mbali kujifunza na kupata uzoefu wa siasa lkn c kushinda uchaguzi na kuchukua madaraka kwa sababu ata ktk Mpira France vs USA ili mechi iwe fair marefa na Washika vibendera wanatoka nchi tofauti na hao wanaokutana,na sasa wameongeza na goal technology ili mchezo uwe fair zaid. So kama Watoa maamuzi ya mchezo hawapo huru uwez kushinda kwa Haki au kufungwa kwa haki na hili upinzani wanalijua ndo maana mm nasema wanafanya mazoezi ya siasa na kuongeza vipato binafsi kwa njia mbali mbali.
Mnaongea ujinga baada ya kupora uchaguzi
 
Itikadi ipo kabisa, tatizo ni njaa!! Kama ilivyo rahisi kumdanganya ama kumshawishi mtu kwa kutumia DINI ndivyo ilivyo vyepesi kumdanganya ama kumshawishi tu kwa kutumia pesa na rushwa ya madaraka.

Njaa na Ubinafsi ndiyo adui number moja wa Upinzani nchini.
 
Nchi yetu ni ya ujamaa na kujitegeme hivyo vyama vinatakiwa kuwa na Itikadi zisizokinzana na Katiba, Haya tuambizane Itikadi gani ya chama inahakisi Katiba ya nchi??
Hata haujitambui, ujamaa upi na mliachana na Azimio la Arusha?
 
Huko ndiko kukosa point kabisa, nani ana itikadi Tanzania kwa sasa?? CCM sasa hivi Neither Ujamaa wala Capitalism, wanafuata kokote kule, not defined. Chadema wamekosa resources, ukikosa resources unakuwa hauko organized kabisa. CCM wana resources, wana tumia pesa za serikali vile vile. Chadema hawana huo mwanya kabisa.
Naungana na wewe kwenye resources 🤜
 
Nchi yetu ni ya ujamaa na kujitegeme hivyo vyama vinatakiwa kuwa na Itikadi zisizokinzana na Katiba, Haya tuambizane Itikadi gani ya chama inahakisi Katiba ya nchi??

Nchi ya kijamaa? Peleka ujinga mbali.
 
Back
Top Bottom