Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume: Chanzo cha tatizo na ushauri wa jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619

Wajameni tunaulizia kwa wataalamu wa JF dawa gani za kuongeza mbegu za kiume yaani idadi zake na kuongeza nguvu za kiume ukiacha viagra.

Tuwe serious kutoa msaada.

Ufafanuzi wa jumla wa tatizo la nguvu za kiume na tiba yake
Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi. Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.

Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka siku had I siku. Tafiti mbalimbali zinasema wanaume wengi wenye umri kuanzia miaka 35 na kuendelea ndio wanaosumbuliwa na tatizo hili kwa kiasi kikubwa. Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili.

Hii ni kutokana na kwamba wengi wao wanakuwa hawaelewi aina ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, namna wanavyotakiwa kuishi ili kupunguza janga hilo, wanakunywa pombe na hawajishughulishi na mazoezi ya viungo. Mazoezi ya viungo hupunguza tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa sana.

Kupungukiwa nguvu za kiume kunaweza pia kuwa kumetokana na mambo ya kihisia, kwa kiingereza ‘emotional causes’. Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume ni pamoja na magonjwa kama vile ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la juu la damu.

Asilimia 51 mpaka 61 ya wanaume wanaosumbuliwa na kisukari wanapatwa na tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri. Kadharika wagonjwa wa kiharusi na wale waliotekwa na ulevi nao ni miongoni mwa watu wanaoweza kupatwa kirahisi na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Walevi wengi wa pombe kwa mfano wanakabiliwa na tatizo la uzalishaji mchache wa mbegu za kiume (manii).

Wengine wenye hatari ya kupatwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume ni pamoja na wanaume wenye shinikizo la juu la damu, wenye matatizo ya tezi, waliowahi kufanya upasuaji katika viungo vya uzazi wakabaki na majeraha, watu wanaotumia dawa zenye kemikali kiholela bila kushauriwa na wataalamu na wale wanaougua maradhi yanayodhoofisha msukumo wa damu kwenda katika mishipa ya uume.

Pamoja na hayo, tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza kutibika kwa watu wa rika zote.

Nini Sababu ya uume kushindwa kusimama?

Kushindwa kwa uume kusimama pia hutambulika kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenza wake.

Pamoja na ukweli kuwa mara zote Mwanaume lazima atafika kileleni, hali huweza kuwa tofauti kwa upande wa pili kwani mwanamke anahitaji mwanaume akawie zaidi ili na yeye (mwanamke) aweze kutosheka.

Mkeo hupendelea ukawie na ikiwezekana ukawie zaidi. Kama utakuwa unawahi kumaliza, basi mkeo anakuwa hapati raha kamili.

Ingawa, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wanakabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni au kupungukiwa kwa nguvu za kiume. Hata hivyo kutambuwa tu kwamba wanaume wengine pia wana tatizo kama lako siyo sababu ya wewe kukaa tu bila kutafuta suluhisho la tatizo lako.

Habari njema ni kuwa zipo njia zinazoweza kuleta matokeo mazuri na hatimaye kulimaliza tatizo hili bila madhara mabaya hapo baadaye.

Wakati mwingine uume kushindwa kusimama inaweza kuwa si tatizo, lakini jambo hilo linapojitokeza kila mara na kwa kipindi kirefu inaweza kuleta msongo wa mawazo kwa mume na hata kwa mke.

Sababu nyingine ambazo zinaweza kupelekea uume usisimame vizuri ni pamoja na matatizo ya mhemko kama:
  • Wasiwasi
  • Hasira
  • Msongo wa mawazo (Stress)
  • Huzuni
  • Hofu na mashaka
  • Kukosa hamu ya tendo la ndoa n.k
Ili uume usimame vizuri ni lazima:

Mfumo wako wa neva uwe na afya nzuri inayopelekea mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.

Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa Misuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa

Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.

Uume kshindwa kusimama vizuri kunaweza kusababishwa pia kama kipengele kimojawapo hapo juu hakifanyi kazi vizuri. Mambo mengine yanayopelekea kupunguwa kwa nguvu za kiume, uume kushindwa kusimama vizuri na kuwahi kufika kileleni ni:
  • Uzee
  • Kisukari
  • Kujichua/Punyeto
  • Uzinzi
  • Kukosa Elimu ya vyakula
  • Kutokujishughulisha na mazoezi
  • Shinikizo la juu la damu
  • Ugonjwa wa moyo
  • Uvutaji sigara/tumbaku
  • Utumiaji uliozidi wa kafeina.
  • Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
  • Madawa ya kulevya
  • Kupungua kwa homoni ya testerone
  • Athari kutoka kwa baadhi ya dawa
  • Pombe
Nguvu za kiume na mzunguko wa damu: Kitu gani husababisha uume usimame?

Unaweza kujibu ni msisimko. Ni kweli, Jibu lako linaweza kuwa sahihi. Hata hivyo msisimko ni matokeo. Kipo kinachosababisha kutokea huo msisimko. Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza kutokea.

Kila mwanaume anatakiwa kujuwa jibu sahihi la swali hili ili atakapopatwa na tatizo atambuwe wapi pa kuanzia na pa kuishia. Siyo lazima uwe daktari, Elimu ya kutambua mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama watu wengi mnavyodhani.

Kutokusoma soma lolote kuhusu miili yetu inavyofanya kazi ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia dawa kiholela na hivyo kujikuta tunapata madhara zaidi badala ya kujitibu.

Mzunguko wa damu ndicho kitu kinachofanya uume USIMAME. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja muhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri upendelee Kunywa maji bila KUSUBIRI KIU.

Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele muhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na kusimama kwa uume wako.

Tiba yake.
Chakula bora ni tiba ya kwanza ya nguvu za kiume na mazoezi ya viungo pia kama tatizo litazidi unashauriwa kwenda hospitali kumuona dakari ili upatiwe matibabu ya kitaalamu.

Baadhi ya vyakula unavyoshauriwa kutumia ili kuondoa tatizo la nguvu za kiume.

1. Blueberry


Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina virutubisho vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume. Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.

2. Mtini (Figs)
Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.

3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)
Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume. Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na nguvu zaidi.

Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.

4. Karanga



Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.

5. Vitunguu saumu



Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.

6. Ndizi



Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).

Vyakula ni bora kuliko madawa makali

Mie binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako yote ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona kuna tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa. Kutumia madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa kufanya kazi kama inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.

Mara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko, lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hutibua mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri uangalie jinsi unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa kupanda mtungi, ruksa kuangalia njia mbadala.

Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi, kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa makini.

Kama ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini. Ni vizuri ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa mara ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni hapo chini nasi tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua tatizo la nguvu za kiume.

BAADHI YA MAONI NA UFAFANUZI ULIOTOLEWA NA WADAU WA JF KUHUSU TATIZO HILI
---
---
---
---
---
---
---
---
---
-----


PIA UNASHAURIWA KUSOMA MADA HIZI:
= > Suluhisho rahisi kwa wanaodhani wamepungukiwa nguvu, wanaosumbuka kurudia tendo au kuwahi kufika

= > Ushuhuda: Upungufu wa nguvu za kiume - Tiba halisi

= > Tatizo la kuwahi kufika kileleni kwa wanaume: Fahamu chanzo chake na namna ya kutibu tatizo hili

= > Jinsi ya kutibu tatizo la nguvu za kiume
 
Dawa nzuri ni lishe tu. kula mlo kamili, matund ana mboga mboga kama kawaida. pata muda wa kutosha kupumzika. epuka sigara na kunywa pombe kwa kiasi kama mywaji.
 
V-RX capsules have been developed from all-natural herbal ingredients, you will increase your size, volume of the sperms and improve your natural performance. When you begin to experience more frequent firmer erections, penis enlargment begins in a matter of weeks.

First you will begin to see an increase in the girth, then as cell development really begins to take hold you will see an increase in penis length as well.
 
Causes for low sperm count:

Infected semen

Tight underpants, bathing in very hot water, sitting for long hours, over weight in which fat layers sag on testicles reduce sperm count

Very frequent semen ejaculation also lead to lowered sperm count and man may become effectively infertile. Hence maintaining a gap of 3 days between two consecutive ejaculations keeps a man more fertile.

Smoking, Excessive alcohol intake.

Over exertion physically and mentally

Zinc deficiency

Infections present in prostate gland.

Malformed genital organs.

Anabolic steroid use

10 Ways you can Increase Your Sperm Count

1. Have sex & masturbate less often - the more times you ejaculate, the less dense your semen will be. Maintain a gap of 3 days between two consecutive ejaculations.

2. Refrain from habits like smoking, alcohol consumption etc. - Alcohol affects your liver function, which, in turn, causes a dramatic rise in estrogen levels. Even two drinks a day will have long-term effects on sperm production

3. Exercise regularly.Exercising your PC muscle can help you shoot further than ever before.

4. Eat Nutritious Food - Diet that's low in fat, and high in protein, vegetables, and whole grains is good for your health and for your sperm. Avoid bitter, astringent and spicy foods.Reduce caffeine intake

5. Avoid heating of testicles - Wear loose, cotton boxer shorts, Avoid hot baths and saunas

6. Lose any excess weight, which tends to cause testosterone/oestrogen imbalances.

7. Reduce stress levels by learning relaxation techniques - Keep your mind and body healthy by regular practice of YOGA and MEDITATION.

8. Massage body with herbal oil, which improves blood circulation.

9. Try supplements - Certain natural supplements promise to increase sperm production. Checkout some Natural and Herbal, no side effects supplements at

10. Make love in the early morning or afternoon. Sperm levels are often highest in the mornings.
 
Bibie hapo mtihani wala sikupi tena nitaibika mwenyewe jibu amelipata
 
Kuongeza mbegu za kiume:
Kula sana korosho but they are expensive,

To improve your natural performance:
Kula na kunywa supu ya pweza kwa sana if possible three times@week.
 
Hamjui kitu, mineno mingi tu kwa ufupi kabisa hakuna kitu au kirutubisho kama kalanga au kwa wengine wanaziita njugu nyasa ,hizo ndio hadi sasa zinaongoza yaani ni nambari wani kabisa, yaani kama huamini jaribu kula robo kilo kwa siku nzima alafu nisikilisie siku inayofuata.

Kama hazikukusaidia basi mwone daktari.
 
Kwa nini wanaume wengine ni shughuli kurudia sex baada ya bao la kwanza?
 
Inawezekana ulikuwa umezoea kujichua hizo ni moja ya adhari zake mdogo wangu
hapana sio.....kupiga nyeto ni salama na hakuna madhara yoyote ila kuna faida mashine inakuwa kubwa kadri....

.....kwenda mzunguko wa pili kuna sababishwa na vitu kibao....hata mashine ya shori kama hailipi huwezi kujisikia kwenda mzunguko wapili....
 
nasapoti hiyo kwani mashine inapokuwa tofauti hamu inapotea lakini mashine kama ni bomba unaweza kwenda hata mara nane
 
Asante sana kwa mleta swali maana sio siri nilikuwa mbioni pia kuuliza swali kama hili hili! kwa maana hiyo mashine za wanawake siku hizi ni mbovu! maana ukipita kila kona wimbo ni huu huu, jamaa akipiga goli moja ndo mpaka kesho yake au baada ya siku hata tano hivi! yani mpaka unaanza kumuhisi vibaya yani.

Kama mimi nilishawahi kuuliza, nilishoambiwa kwamba uchovu ndo unaomfanya awe hivyo? Kwa hiyo kwa kuwa unampenda inabidi uvumilie na kuamini hivyo hivyo siku ziende.
 
Mimi nadhani kuna kaugonjwa kamewaingia hivi viumbe si bure. Naunaitwa 1ejaculatio swine.
 
ndo manake bibie mashine ikiwa mbovu hailipi kwa mzunguko wa pili dadake.....mtu hata ile ya kwanza anaogelea weee ndio hiop akimaliza kama iliyokutokea akimaliza anasingizia kachoka...

...tiba: zingatieni vyakula vya kufanya mashine iwe mwake.....fanyeni mazoezi ya kubana misuli ya kule kama ukitaka kujua yanavyofanyika uliza....
 
Mimi nadhani kuna kaugonjwa kamewaingia hivi viumbe si bure. Naunaitwa 1ejaculatio swine.
Pia na wanaume nao hawajui kudeal na ishu za namna hii.....wengi wa wanaume wanafikria mapenzi ni kuchoma choma nje ndani kibaoo....

..mapenzi sio kihivyo....wajifunze kuzamia 30-45 mins wafanye window sex shori akiwa kesha score 2 yeye ndio aingie amalizie na kabao kake ka1.....
 
Mods hii ngoma ilifaa iende kwenye mambo ya kikubwa, sioni mwelekeo wa majibu ya kitabibu hapa..........!

Staili pia zimekuwa nyingi, sasa ufundi ukizidi mashine ikiingia upepo ladha yake inapotea kabisaaaaaaaa......
 
Men with premature ejaculation who used a topical spray five minutes before intercourse were able to delay their orgasm six times longer than normal, according to a study in the April issue of BJU International. Three hundred men with clinically diagnosed lifelong premature ejaculation (PE) from 31 centres in the UK, Czech Republic, Hungary and Poland, were randomised into two groups.

Two hundred used the PSD502 spray, which contains 7.5mg of lidocaine and 2.5mg of prilocaine, and 100 used a placebo spray with no active ingredients. Every time they had intercourse during the three-month study period, each couple measured the time from vaginal penetration to ejaculation with a stopwatch. The men were asked to abstain from sexual activity or masturbation for 24 hours before each recorded encounter.

The time from penetration to ejaculation increased from an average of 0.6 minutes to 3.8 minutes in the medicated group and to just 1.1 minutes in the placebo group. When these figures were adjusted to take account of any variations between the two groups, these showed that the treatment group were able to last 6.3 times longer after penetration when they used the spray.

The placebo group lasted 1.7 times longer. "Premature ejaculation can be a very distressing condition for men and can cause distress, frustration and make them avoid sexual intimacy" says lead researcher Professor W Wallace Dinsmore from the Royal Victoria Hospital, Belfast, UK. The research team used the evidence-based definition of lifelong PE developed by the International Society for Sexual Medicine to select their study subjects.

This states that ejaculation occurs within about one minute of vaginal penetration in the majority of encounters. "Because this definition was only launched in 2008, studies have yet to determine the prevalence of lifelong PE in the male population" says Professor Dinsmore.

"But previous research suggests that as many as 40% of men will experience premature ejaculation at some time in their lives." The 300 men who took part in the phase three, multicentre, double-blind, randomised study had an average age of 35.

The majority had used other treatments before, the most common being oral antidepressants. After three months of treatment the researchers reported that: -- 90% of the men in the treatment group were able to delay ejaculation for more than one minute following vaginal penetration, compared with 54% in the placebo group.

-- 74% of men in the treatment group managed to last more than two minutes before ejaculation, compared with 22% in the placebo group. -- 62% of men in the treatment group said their orgasms were 'good' or 'very good' after three months, compared with 20% before the study started. The figures for the placebo group were slightly lower at the end (19%) than at the start (21%).

-- 66% of men in the treatment group said the medication was 'good' or 'excellent' compared with 15% in the placebo group. -- A significantly higher percentage of the patients and partners in the treatment group reported improvements when it came to perceived control, personal distress, satisfaction with sexual intercourse and interpersonal difficulties.

-- There were no serious adverse events reported during the study. Adverse treatment-related reactions were reported by five men and six women from the treatment group and one man from the placebo group. The most common problems were loss of erection and a burning sensation in the vagina.

"Our study shows that when the PSD502 spray was applied to the man's penis five minutes before intercourse it improved both sexual performance and sexual satisfaction, which are key factors in treating premature ejaculation" says Professor Dinsmore.

"It was well tolerated by both patients and their partners, with no systemic side effects and a low incidence of localised effects and was rated favourably by the majority of users. "We believe that this shows that PSD502 offers significant advantages over other therapies being developed for the treatment of premature ejaculation." Source: Wiley - Blackwell
 
Mmmh makubwa, na hapo hapo unasifiwa kuwa machine ni bomba, au huwa ni fix. Haya ndugu nionyeshe hayo mazoezi yakhe ya fanywaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…