Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume: Chanzo cha tatizo na ushauri wa jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume: Chanzo cha tatizo na ushauri wa jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo

MBINU 10 ZA KUONGEZA WINGI WA MBEGU ZA KIUME (sperm count)

1. Kula lishe bora

Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula vingi vya kisasa havina uwezo wa kuongeza uwingi wa mbegu.

Kama utarekebisha tu aina ya chakula unachokula kunaweza kupelekea kutibu tatizo lako.

Punguza matumizi ya sukari na vyakula vya ngano. Ongeza zaidi matunda, mboga za majani na mafuta yenye afya.

Hii inaweza kusaidia kutibu tatizo lako la kuwa na mbegu chache kwa haraka sana.

2. Acha kutumia vinywaji au vyakula vyenye kaffeina

Kama una tatizo la kuwa na mbegu chache ni vizuri ukaacha kutumia vinywaji au vyakula vyote vyenye kaffeina kwanza.

Navyo ni pamoja na chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi zote, malta, redbull, chokoleti nk.

Hivi vitu vyenye kaffeina ni sababu ya kupungua kwa uwingi wa mbegu za kiume.

3. Tumia kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu ni maajabu ya Mungu mwenyewe. Kitunguu swaumu kina Selenium na pia kinaondoa sumu mwilini vitu viwili mhimu kwa ajili ya kuongeza spidi ya mbegu.

Kitunguu swaumu kina kitu kingine kiitwacho ‘Allicin’ ambacho huongeza msukumo wa damu kwenda kwenye uume.

Ongeza kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika.

Pia unaweza kutafuna punje 2 au 3 kila unapoenda kulala au unaweza kukatakata hizo punje 3 vipande vidogo vido (chop) kisha unywe na maji.

Usizidishe zaidi ya punje 3 kwa siku.

4. Kula ndizi

Ndizi hazifanani tu na uume kama unavyoweza kuwaza bali pia ni chakula kizuri kwa ajili ya afya ya uume wako. Ndizi zina kimeng’enya kimoja adimu sana kijulikanacho kama ‘Bromeliad’ ambacho husaidia kuziweka sawa homoni zinazohusiana na tendo la ndoa.

Ndizi pia zina Magnesiamu, Vitamini B1 na Vitamini C, vitu ambavyo ni mhimu sana kwa ajili ya kutengeneza mbegu za kiume.

5. Kula mbegu za maboga
Mbegu za maboga zina kiasi kingi ccha madini ya Zinki ambayo ni mhimu katika kuundwa au kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya testosterone.

Pia zina vitamini B, C, D, E, na K ambazo zote ni vitamini mhimu katika kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa na nguvu kwa ujumla.

Pia mbegu za maboga zina kalsiamu, potasiaumu, niacin na phosphorous.

6. Kula zaidi mboga za majani

Mama alikuwa sahihi kumbe ingawa nilikuwa nachukia nikikuta mboga majani badala ya nyama nikirudi kutoka shule.

Mboga za majani zinapunguza homoni ya ‘estrogen’ na hivyo kufanya homoni ya ‘testosterone’ ipatikane kwa wingi na kiurahisi zaidi na hivyo mbegu zako ziweze kuongezeka bila vipangamizi vyovyote.

7. Kunywa maji mengi kila siku
Maji ya kunywa
Hili ni suluhisho rahisi lisilohitaji gharama wala ugomvi wowote kukuelewesha. Mwenyewe unajua kuwa maji ni uhai na kuwa asilimia 75 ya mwili wako ni maji, sasa kama huna tabia ya kunywa maji ya kutosha kila siku sijuwi unategemea miujiza kutoka wapi.

Huhitaji kusikia kiu au mpaka upate hamu ya kunywa maji bali hili ni jambo la lazima kwamba huwezi kukaa bila kunywa maji halafu ubaki na afya bora.

Mbegu zako zimetengenezwa kwa maji, zipo kwenye hali ya kimiminika.

Kutokunywa maji ya kutosha kila siku kuna uhusiano wa moja kwa moja na kupungua kwa uwingi wa mbegu.

Kama utatekeleza mengine yote niliyoelekeza hapo juu halafu ukasahau kunywa maji hesabu umeshachemka tayari.

Kutegemea na uzito wako unaweza kuhitaji maji lita 2 mpaka 3 kila siku.

8. Tumia vyakula vyenye folic asidi kwa wingi

Katika utafiti mmoja wanaume walioongeza utumiaji wa folic asidi na zink waliongeza uwingi wa mbegu zao kwa zaidi ya asilimia 74 kwa muda wiki 2 tu.

Vyakula hivi ni pamoja na tunda la parachichi na karoti.

Hivyo isipite siku bila kula parachichi 1 kutafuna karoti moja kama una tatizo la mbegu chache.

Vingine ni pamoja na mbegu za maboga, ufuta, alizeti, maharage, chungwa, papai, bamia nk

9. Mayai

Mayai yanachukuliwa kama mbadala wa uhakika zaidi katika kuongeza uwingi wa mbegu pamoja na kuongeza spidi au kasi yake. Yana vitamini E nyingi na protini ya kutosha vitu viwili mhimu katika kuongeza mbegu.

Mayai yanafanya kazi nyingine mhimu nayo ni kuzilinda seli za mbegu za kiume kutoshambuliwa na vijidudu nyemelezi kirahisi ambavyo vinaweza kuwa sababu ya kupungua kwa mbegu zako.

Viinilishe vilivyomo kwenye mayai vinafanya kazi ya ziada ya kuzifanya mbegu zenye afya zaidi na zenye nguvu zaidi jambo ambalo ni mhimu kwa ajili ya uzazi kwa upande wa mwanaume.

Kumbuka ni mayai ya kuku wa kienyeji tu yanayofaa kwa kazi hii. Kila siku kula mayai mawili mpaka matatu kama una tatizo hili la kuwa na mbegu chache.

10. Spinach

Folic asidi ni kitu mhimu katika kuongezeka kwa mbegu za kiume. Spinachi na mboga nyingine za majani zenye rangi ya kijani ni mhimu kwa ajili hii sababu ya vitamini na kuweka sawa usawa wa ‘folate’ kwenye mfumo wako wa mwili.

Kama folate ipo chini kuna uwezekano ukawa unatengeneza mbegu zisizo na umbile linalotakiwa kwa uzazi na hiyo hupelekea shida na matatizo mengine ya uzazi upande wa mwanamke (birth defects) kama ujauzito kutoka mara tu mimba inapotungwa

Nilichogundua kula vyakula vyote fresh[emoji23]
 
Naomba msaada..jaman kama hospital umefanya sperm count three times no sperm..na wamechek testosterone zipo sawa,,,shida nn???
Nianze kwa kukupa pole. Kama umeenda hospitali na umeambiwa huna mbegu kabisa inawezekana ikawa kweli yaan una azoospermia. Vile vile inawezekana una low sperm count yaan oligospermia na hamkuelewana na daktari.

USHAURI;
1.Kama unatumia tumbaku kwa jamii zake, pombe ama una uzito ulikithiri tafta namna ya ku-bounce back.
2. Rudi hospital uongee na daktari wako muone namna ya kumanage tatizo kwasababu azoospermia ziko za aina 2 moja inaweza aghalabu rekebishika(obstructive azoospermia yaan inayotokana na kuziba mrija unaopitisha mbegu toka kwenye korodani) na nyingine inataabu kidogo(nonobstructive azoospermia yaan korodani hazitengenezi mbegu) hii technology bado hatuna nchini naamna ya kumanage.
3. Kama kwa upande mwingine una mbegu chache kwenye shahawa(oligospermia) na wataangalia sababu mostly ni infection watakutibu ila kama ni genetic yaan ya kuzaliwa nao na unataka mtoto basi inabidi ww na mwenzi wako mfanye tendo mara nyingi(mnaweza mkatenga siku moja) haswa siku ya 14 ya mzunguko wake(hii siyo kwa kila mwanamke? Hii inaongeza uwezekano wa kupata mtoto, pia zingatia kuishi maisha ya afya kama chakula kizuri na mazoezi.

Best of luck mkuu.
 
V-RX capsules have been developed from all-natural herbal ingredients, you will increase your size, volume of the sperms and improve your natural performance. When you begin to experience more frequent firmer erections, penis enlargment begins in a matter of weeks. First you will begin to see an increase in the girth, then as cell development really begins to take hold you will see an increase in penis length as well.
Yahhapo sawa
 
Nianze kwa kukupa pole. Kama umeenda hospitali na umeambiwa huna mbegu kabisa inawezekana ikawa kweli yaan una azoospermia. Vile vile inawezekana una low sperm count yaan oligospermia na hamkuelewana na daktari.

USHAURI;
1.Kama unatumia tumbaku kwa jamii zake, pombe ama una uzito ulikithiri tafta namna ya ku-bounce back.
2. Rudi hospital uongee na daktari wako muone namna ya kumanage tatizo kwasababu azoospermia ziko za aina 2 moja inaweza aghalabu rekebishika(obstructive azoospermia yaan inayotokana na kuziba mrija unaopitisha mbegu toka kwenye korodani) na nyingine inataabu kidogo(nonobstructive azoospermia yaan korodani hazitengenezi mbegu) hii technology bado hatuna nchini naamna ya kumanage.
3. Kama kwa upande mwingine una mbegu chache kwenye shahawa(oligospermia) na wataangalia sababu mostly ni infection watakutibu ila kama ni genetic yaan ya kuzaliwa nao na unataka mtoto basi inabidi ww na mwenzi wako mfanye tendo mara nyingi(mnaweza mkatenga siku moja) haswa siku ya 14 ya mzunguko wake(hii siyo kwa kila mwanamke? Hii inaongeza uwezekano wa kupata mtoto, pia zingatia kuishi maisha ya afya kama chakula kizuri na mazoezi.

Best of luck mkuu.
Kwa hiyo apo kama korodani haiwezi kutengeneza sperm..finally we n mgumba??????
 
No sperm ? Au low sperm counts ?
Hii huwa inatokea mkuu, kuwa no sperm kabisa, kuwa low sperm, au volume ya ejaculation inakuwa nyingi lakini Hanna sperm, au sperm chache viscosity inakuwa Hamna, au sperm zinakuwa zipo lakin maumbo yao yanakuwa Round vichwa vyake kwa hivyo no vigumu kutoboa yai la mwanamke, hivyo kupata mtoto inakuwa no vigumu sana.

Zipo sababu nyingi sana ambazo unaweza Kumu report mtu/client kuwa anatatizo la uzalishaji.
>Kiwango cha PH = kuangalia Alkali au acidic is better In alkal 7.0- 8.9pH, ikiwa chini ya hapo means duct blocked

>Ubora wa Viscosity yani ule munyumbuliko kama mlenda= husaidia Ku move sperm

>Appearance/Odour = kichwa, mkia, body take,

>Volume = At least 3mls up to,,,

>Movement = Better forward movement to find woman egg where is,,,?
 
Pole sana mkuu. Tatizo la shahawa kukosa mbegu za kiume(sperms) lipo na ni moja ya visababishi vya ugumba(infertility). Na hili linaweza kusababishwa na matatizo ya ukosefu wa homone ambazo huchochea uzalishaji wa mbegu e.g Testosterone au matatizo kwenye kiwanda cha mbengu(testes) ama ukiwa na tatizo kwenye barabara inayotumiwa na mbegu kusafiri kutoka kwenye kiwanda(testes) kuja kwenye urethra( blockage of the vas defferens). Hivyo nakushaur ukaonane na wataalamu wa magonjwa ya uzazi wakuchunguze.
 
Mcheki huyu mimi ameponesha kabisa kwa kunipa formula yake ya matunda kwa gharama nafuu sanaa ni elfu 22 tu sikuamin nilivyopona maana nilihangaika sana kwa gharama nying0712505049
 
Pole sana mkuu. Tatizo la shahawa kukosa mbegu za kiume(sperms) lipo na ni moja ya visababishi vya ugumba(infertility). Na hili linaweza kusababishwa na matatizo ya ukosefu wa homone ambazo huchochea uzalishaji wa mbegu e.g Testosterone au matatizo kwenye kiwanda cha mbengu(testes) ama ukiwa na tatizo kwenye barabara inayotumiwa na mbegu kusafiri kutoka kwenye kiwanda(testes) kuja kwenye urethra( blockage of the vas defferens). Hivyo nakushaur ukaonane na wataalamu wa magonjwa ya uzazi wakuchunguze.
Wameniambia hormone ambazo zinachochea uzalishaji wa sperm zimekufa zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom