Baba Mtu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2008
- 870
- 170
![]()
Matikiti Maji Yanaongeza Nguvu za Kiume
Watafiti wa nchini Marekani wamegundua kwamba matikiti maji yanaongeza nguvu za kiume na yanasaidia kutoa tiba kwa wanaume wenye upungufu wa nguvu za kiume. Watafiti katika chuo kikuu cha Texas A&M wamegundua kwamba matikiti maji yanaweza yakatumika kama "Viagra ya Asili" kwa wanaume wenye matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.
Watafiti hao walisema kuwa tikiti maji lina amino acid nyingi za citrulline ambazo huifanya mishipa ya damu itanuke na iwe katika hali kama ile ambayo mtu anayetumia viagra au madawa ya kuongeza nguvu za kiume huwa nayo.
Citrulline ikiwa mwilini hugeuka kuwa "arginine" mojawapo ya aina za amino acid. Hali hii husababisha kuongezeka kwa kiwango cha nitric oxide kwenye damu. Nitric oxide husaidia kuifanya mishipa ya damu itanuke.
Hata hivyo watafiti hao hawakuweka wazi idadi ya matikiti maji ambayo mwanaume anatakiwa kula ili aweze kuwa na nguvu za kiume kama za viagra.
Bhimu Patil, mkurugenzi wa maabara iliyofanya utafiti huo alisisitiza kuwa ulaji wa tikiti maji wa mara kwa mara unasaidia kuzuia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Mojawapo ya faida nyingine ya tikiti maji iliyotajwa ni kusaidia kushusha shinikizo la damu.
nifahamishe.com
Kwa maelezo zaidi pia tembelea tovuti hii
Viagra-Like Effects From Watermelon