Tatizo la uvivu wa wananchi na bunge ni vya kulaumiwa kwenye bei ya chakula

Tatizo la uvivu wa wananchi na bunge ni vya kulaumiwa kwenye bei ya chakula

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Utamaduni wa uvivu ndiyo umesababisha tatizo kubwa la bei ya Chakula. Hakuna sababu ya Tanzania kuagiza mbolea, ngano, mafuta ya kupikia na sukari.

Uvivu huu sio kwa Tanzania nzima lakini mikoa ya pwani, kati na mashariki inaongoza kwa uvivu. Vijana wanataka kukaa mijini tu bila shughuli wakati kilimo na mifugo inalipa sana.

Serikali bila kusema ukweli huu watatoa kila pesa lakini tatizo la uvivu ni lazima tulitatue. Mikoa ya kati na Pwani hakuna uzalishaji wowote wa maana lakini ndiyo walaji wakubwa wa nafaka.

Waziri wa Kilimo anafanya kazi nzuri lakini ukweli ni kwamba wananchi wengi nao ni wavivu. Kuna mzee mfano nimemuweka kwenye shamba langu bagamoyo mpaka nimeweka watu wa kumlimia lakini bado anaweka uvivu na kusubiri mimi ndiyo nimtumie pesa ya kutumia!.

1. Mbolea uwekezaji ulikuwa haupo huko nyuma kwasababu kilimo bado kilikuwa kidogo na hatukuwa na mashamba ya kimkakati hivyo sasa ndiyo tuna amka na kupata uwekezaji wa kiwanda kutoka Burundi!. Mbolea mahitaji zaidi ya tani 700,000 tunazalisha tani 30,000. Mafuta mahitaji tani 600,000 tunatengeneza tani 270,000 tu

2. Masoko ya Kilimo tunayo hasa Kenya lakini vijana wetu hawataki kulima ingawa kwasasa kilimo kinalipa kuanzia kilimo cha matunda mpaka nafaka

3. Uvivu wa bunge kulikuwa na sera za kilimo kwanza miaka zaidi ya 15 lakini bunge letu linajali zaidi kudidimiza upinzani badala ya kufuatilia sera za nchi
 
Naona wanaanza kunielewa sasa

..unasema kuna uhaba wa ngano, na mafuta ya kupikia, halafu unawalaumu wenyeji wa mikoa ya pwani na mashariki ya Tz.

..kwa taarifa yako ngano haistawi pwani au mashariki ya nchi yetu.

..Kama unataka kutoa lawama kwa uhaba wa ngano hapa Tz, basi ungezielekeza kwa wakulima wa maeneo kunakostawi na kulimwa ngano.

..Lakini kabla ya kutoa lawama hizo, umejiridhisha kwamba mazingira ya kilimo cha ngano hapa Tz ni rafiki, na yanawezesha wakulima wetu kuzalisha vya kutosha, kwa ubora, na kuweza kushindana na ngano inayoagizwa toka nje?
 
Tatizo ukipiga sana jembe la mkono mpaka scanner za NIDA zinakutema
 
Tatizo ukipiga sana jembe la mkono mpaka scanner za NIDA zinakutema

Sijasema wavivu kwenye kilimo bali wana utamaduni wa uvivu kwenye kila kitu. Acheni uvivu

"Uvivu huu sio kwa Tanzania nzima lakini mikoa ya pwani, kati na mashariki inaongoza kwa uvivu"
 
Back
Top Bottom