Tatizo la vipele vinavyotokana na kunyoa nywele kichwani chini ya kisogo (Acne Keloidalis Nuchae)

Tatizo la vipele vinavyotokana na kunyoa nywele kichwani chini ya kisogo (Acne Keloidalis Nuchae)

Linakuwa jeupe hivi, jina hata mimi silifahamu
c7bdede52d1ce621525ed4ea04dfd12a.jpg

Hilo jiwe as shown
Nimetumia pia bila matumain
Kwa ndevu linasaidia
But kwa huo upele hapo juu no home
Natoa hili kama mgonjwa na sio dr
Huo upele inatesa hasa kipondi cha joto ni balaaa
Please lets opt dawa nilizotoa hapo juu
Zimenisaidia kwa muda mfupi sana
Ikumbukwe miaka 10+ sikupata nafuu
 
Hii Hali Inaitwa kitaalamu Inaitwa Acne keloidalis nuchae inawapata mainly wanaume hasa wale wanaopenda kunyoa nywele chini kabisa au kuchonga nywele kisogoni, ni mchanganyiko wa Allergic reaction na infection hii inatokana na Shina la nywele lilibaki baada ya kukatwa chini kabisa ambalo liko sharp linatengeneza some sort of allergic respond kwenye ngozi linakuwa km foreign body, mwili unarespond kwa kutoa kipele then infection inaingia baadae kipele kinakuwa keloid like
Dawa
1. kwa wale wanaopenda kunyoa au kuchonga nywele kwa nyuma watumie cream za antiallergy baada ya kunyoa kupunguza chance ya kutokea reaction .
2.Kwa wenye tatizo tayari tiba ni cream za Allergy pamoja na Antibiotics kuua vijidudu
3.Kwa wale ambao yamekuwa makubwa yameungana na kutengeneza kovu baya tiba ni surgical removal Au hata mionzi
Cha Muhimu kabisa ni kuwaona Dermatologist (watalaamu wa mgonjwa ya ngozi kwa tiba sahihi)
 
Pamoja na maushauri yote yaliyotolewa, naomba wale wote mnaosumbuliwa na hivi vipele muache kula nyama ya nguruwe.

Ni hayo tu
 
c7bdede52d1ce621525ed4ea04dfd12a.jpg

Hilo jiwe as shown
Nimetumia pia bila matumain
Kwa ndevu linasaidia
But kwa huo upele hapo juu no home
Natoa hili kama mgonjwa na sio dr
Huo upele inatesa hasa kipondi cha joto ni balaaa
Please lets opt dawa nilizotoa hapo juu
Zimenisaidia kwa muda mfupi sana
Ikumbukwe miaka 10+ sikupata nafuu
Muda mwingine tiba hutegemea na aina ya ngozi
 
Aliniandikia dawa ya kupaka inaitwa candiderm cream na vidonge vya anti allergy kwa jina sivikumbuki nilikuwa nameza vinne kwa siku kwa muda siku 28. Pole Sana.
Ungetusaidia kujua na hiyo dawa ya vidonge tungeshukuru sana mkuu, kuna rafiki yangu ana hilo tatizo hadi namuonea huruma
 
Aliniandikia dawa ya kupaka inaitwa candiderm cream na vidonge vya anti allergy kwa jina sivikumbuki nilikuwa nameza vinne kwa siku kwa muda siku 28. Pole Sana.
Mimi nina tatizo hilo,tusaidie jina la hivyo vidonge ili tusaidike wengi
 
Bajati mbaya nasikitika nashindwa kuvikumbuka. Ila nashauri unaweza kuenda pale regency omba kumuona daktari bingwa wa ngozi. Kama unakadi ya bima Ni rahisi zaidi.
 
Ndugu zangu ndani ya JF habari zenu.

Mimi nina matatizo ya vipele mwisho wa nywele za kichwani upande wa kisogoni ambavyo vinatokana na kunyoa.

Nimepata ushauri kwa madaktari mbalimbali juu ya dawa za kutumia bila mafanikio.Kama kuna mtu anajua ni namna gani naweza kutibu na pia kuzuia visitokee tena naomba tuwasiliane humu JF.

Nimeona watu wengi hivi karibuni wamekuwa na hali hiyo ambapo baadhi inapelekea kuota nyama kubwa baadaye.Naomba anayejua asaidie,maana najua watu wengi wanahangaika sana kuutibu ugonjwa huo sasa.

Nitashukuru kwa mtu yeyote aliye tayari kutoa msaada wa ushauri na hata kama kuna dawa aiandike humu niitafute.

Asante.

Ukimaliza kunyoa na mashine, mkasi au wembe paka "apple cider vinegar". Unaweza kuulizia kwenye duka la dawa kubwa. hii itakausha na kuua wadudu halafu rudia kila ukimaliza kuoga. Tumia kwa siku tatu hivi. Kijiko kimoja uchanganye na maji nusu glass. Pia ulizia dawa ya fungus " sonaderm" ukimaliza kunyoa upake. Nafikiri vitasaidia. APPLE CIDER VINEGAR inasaidia pia kama umekula chakula kikakuletea matatizo kama kuharisha vile, unakunywa kijiko kikubwa kwenye glass ya maji. kuhara kunaisha.
upload_2017-5-23_11-54-32.jpeg
 
MyTanzania,

Kaka kuepukana na hayo majambo tumia poda kabla ya kunyoa na kisha paka poda baada ya kunyoa,epuka kutumia after shave au spirit.Mimi nimeweza kuepukana na hayo madude.
 
mwenye uufahamu wa hili tatizo anisaidie msaada wa tiba nini nifanye niweze kuepukana na hili tatizo wanduguView attachment 384093View attachment 384094
Kaka kwa vipele hivyo sahau ""DAWA maana mimi nilishakwenda mpaka nje ya nchi but ckupona....ila nilienda arusha kwa Dr Njela ana kitengo kwa ajili ya kuviondoa na anavifaa maalumu vya kuvinyofoa then atakupatia dawa za kupaka aina mbili...kwishaaaaa mie nipo poa sasa.

Hivi vipele huwa sio kuuma tuu bali humshusha mtu thamani nakujiskia kama hayupo sawa mbele ya watu wake wa karibu...

Usiombe sasa uwe boss ofisi fulani watu watakutungia jina "boss vipele"

Hao wadudu wanasambazwa na mashine za saluni na wakishajenge makao ktk ngozi ya hapo shingoni wahi kabla hawajazaliana na kuwa wengi..

ONYO: Usijaribu kutumia dawa za kienyeji wanazouza saluni!!!!! (wanachanganya maji ya betri, mafuta ya breki ya gari, unga wa betri-dry cell nakadhalika, utaweza kuja kupata kansa bureee)

JINSI YA KUFIKA KWA DR
Ukifika arusha Mianzini, shuka na road ya kwenda stendi kuu, ukifika round about pinda kulia kama unaenda makao mapya, mko wako wa kushoto utaona NHC Complex, ingia hapo ulizia huyo DR watakuonyesha office yake na utapata huduma.
Huyu sio mganga wa kienyeji bali ni Dr halali.

Poleni sana, mie nlishapona baada ya kuhangaika na kupoteza milions of money kwa 5 years, kumbe huduma ipo nyumbani na gharama ndogo sana.
 
Ukimaliza kunyoa na mashine, mkasi au wembe paka "apple cider vinegar". Unaweza kuulizia kwenye duka la dawa kubwa. hii itakausha na kuua wadudu halafu rudia kila ukimaliza kuoga. Tumia kwa siku tatu hivi. Kijiko kimoja uchanganye na maji nusu glass. Pia ulizia dawa ya fungus " sonaderm" ukimaliza kunyoa upake. Nafikiri vitasaidia. APPLE CIDER VINEGAR inasaidia pia kama umekula chakula kikakuletea matatizo kama kuharisha vile, unakunywa kijiko kikubwa kwenye glass ya maji. kuhara kunaisha.
View attachment 513184
Asante sana mkuu kwa maelekezo yako mazuri.
 
Kaka kwa vipele hivyo sahau ""DAWA maana mimi nilishakwenda mpaka nje ya nchi but ckupona....ila nilienda arusha kwa Dr Njela ana kitengo kwa ajili ya kuviondoa na anavifaa maalumu vya kuvinyofoa then atakupatia dawa za kupaka aina mbili...kwishaaaaa mie nipo poa sasa.

Hivi vipele huwa sio kuuma tuu bali humshusha mtu thamani nakujiskia kama hayupo sawa mbele ya watu wake wa karibu...

Usiombe sasa uwe boss ofisi fulani watu watakutungia jina "boss vipele"

Hao wadudu wanasambazwa na mashine za saluni na wakishajenge makao ktk ngozi ya hapo shingoni wahi kabla hawajazaliana na kuwa wengi..

ONYO: Usijaribu kutumia dawa za kienyeji wanazouza saluni!!!!! (wanachanganya maji ya betri, mafuta ya breki ya gari, unga wa betri-dry cell nakadhalika, utaweza kuja kupata kansa bureee)

JINSI YA KUFIKA KWA DR
Ukifika arusha Mianzini, shuka na road ya kwenda stendi kuu, ukifika round about pinda kulia kama unaenda makao mapya, mko wako wa kushoto utaona NHC Complex, ingia hapo ulizia huyo DR watakuonyesha office yake na utapata huduma.
Huyu sio mganga wa kienyeji bali ni Dr halali.

Poleni sana, mie nlishapona baada ya kuhangaika na kupoteza milions of money kwa 5 years, kumbe huduma ipo nyumbani na gharama ndogo sana.
Kaka naomba namba yako
 
Tumia mupiricin cream matokeo utapata mazuri bila shaka
 
Acha kupaka spiriti ndo chanzo hasa cha upele cha msingi paka poda tu mara baada ya kunyoa then kanawe na maji safi na sabuni. Hutasikia tena tatizo kama hilo.
 
Nasumbuliwa sana na vipele kichwani kwa muda mrefu,vinawasha na kutoa majimaji. Nimetumia dawa za kupaka na kunywa lakini bado tatizo haliishi. Mara nyingi nikitumia dawa vinaisha lakini baada ya muda vinarudi tena. Nimepima afya kuhusu hili gonjwa letu nipo salama. Hivyo basi naombeni ushauri nitumie dawa gani ili niweze kupona.
 
Vinauma? Unashave kwa kutumia nn? Hospital walikwambia nini?
 
Back
Top Bottom