Kumekuwa na malalamiko mengi sana yanayo wakuta wanandoa ambapo hupelekea kutokuwa na maelewano mazuri kati yao pale tu linapokuja swala la kushiriki tendo la ndoa na kutofurahia ndoa zao kwa ujumla kwa sababu ya tatizo la maumivu anayohisi mmoja kati ya wanandoa hao.
Hivyo basi twende sambamba tukajifunze kwa pamoja juu ya swala hilo kwa undani zaidi.
Maumivu wakati wa tendo la ndoa huweza kutokea kwa mwanamke au mwanaume, hali ya kuwa na tatizo hili huwakumba sana hasa wanawake ukilinganisha na wanaume.
sababu zinazopelekea kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa (dyspareunia) ni kama zifuatazo;
1. Kupungua au kukauka kabisa kwa ute ute ukeni (vaginal mucous) hali hii humpekekea mwanamke kuhisi maumivu kutokana na msuguano wakati wa tendo la ndoa vile vile huweza kumsababishia michubuko ukeni.
2. Maambukizi ya magonjwa katika via vya uzazi vya mwanamke kama vile fangasi sugu wa ukeni (vaginal fungus), mashambulizi ya maambukizi katika ukuta wa nje wa kizazi (endometriosis).
3. Ukomo wa hedhi (menopause),maumivu huwakumba pia wanawake waliofikia ukomo wa hedhi kutokana na kupungua kwa hali ya unyevuvyevu ukeni (vaginal moisture) na kuwa mkavu ukeni.
4. Kushiriki tendo la ndoa mara tu baada ya kujifungua, baada ya kuvifungua misuli na tishu za uke hulegea na huwa zinarudi katika hali yake pole pole, hivyo basi endapo mwanamke atashiriki tendo la ndoa wakati huo humpelekea kuhisi maumivu makali sana.
5. Matatizo ya kisaikologia (psychological factor)kama vile uoga (anxiety). msongo wa mawazo. Hata mwanaume huweza kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa wa wakati wa kutoa mbegu (Ejaculation), maumivu hayo hutokana na maambukizi au vidonda kwenye (gland)ambazo huruhusu mbegu kutoka (prostate gland). Wakati mwingine maumivu kwa wanaume husababishwa na maambukizi kwenye ngozi inayofunika uume.
*Mpendwa rafiki, magonjwa ya zinaa huchangia tatizo hili kwa kiasi kikubwa, hivyo ni vyema kwenda na mwenza wako mkachunguzwe na kutibiwa kwa pamoja
mara nyingi tiba hufanyika kutokana na tatizo husika.
Ni namna gani unaweza kujikinga na tatizo hili?
Ni muhimu kuzingatia usafi kwani hupunguza uwezekano wa kupata maambukizi.
Kila mtua anatakiwa kumuandaa mwenza wake kabla ya kushiriki tendo la ndoa ambalo husaidia kuzalishwa kwa maji maji ya kulainisha njia ya uzazi (ukeni).
Kuepuka kufanya tendo la ndoa mara tu baada ya kujifungua, ni vyema kushiriki tendo la ndoa angalau wiki sita baada ya kujifungua.
Tiba na ushauri
Endapo mwanamke au mwanaume anapokuwa na tatizo la maumivu makali wakati wa tendo la ndoa, ni vyema akaenda kwenye kituo cha afya na kuonana na mtaalamu wa afya ya uzazi na mtoto kwaajili ya ushauri, vipimo na matibabu.