Ninachojaribu kusema hapa siyo kuwashawishi wanawake wasioshika mimba kunywa pombe, ili waweze kupata mimba, hapana. Maana najua wahafidhina watanitia vidole vya macho. Ninachotaka kusema ni kwamba, huenda pombe hufanya mambo fulani yenye kuweza kuchochea upatikanaji wa mimba kwa haraka.
Kama ukichukua wanawake na kuwaambia kila mmoja apange kupata ujauzito kwa kipindi cha miezi miwili ijayo, tegemea kuona karibu wanane kati ya kila kumi kati ya watakaopata mimba, kuwa ni wale ambao wanakunywa pombe, angalau kwa kiwango cha chupa zisizozidi mbili kutwa. Halafu mmoja katika kumi atakuwa ni yule asiyekunywa pombe.
Wale wanaokunywa sana pombe kwa kiwango cha zaidi ya chupa tatu kwa siku hawa itawalazimu wasubiri kwa mwaka mzima kabla hawajapata mimba. Ni vigumu kwao kuamua kupata mimba na wakaipata kwa muda mfupi. Watafiti wanasema, kiwango cha wastani cha pombe huwachosha wanawake kushiriki zaidi kwenye tendo la ndoa, hivyo yamkini ya kupata ujauzito huongezeka sana.
Kama wanakunywa wastani wa bia mbili, wanakuwa kwenye nafasi ya kuhitaji kufanya tendo la kujamiiana kila baada ya siku moja, wakati wale wasiokunywa wanaweza kukaa wiki nzima bila kujisikia kujamiiana hasa kama mambo yanayowasonga ni mengi. Kupata mimba pia kunahitaji utulivu wa mawazo kwa kiasi fulani. Mwanamke akishakunywa bia mbili kwa mfano, mawazo yake huweza kutulia, hata kama ni kwa muda. Hapo uwezekano wa mimba nao huongezeka.
Dk. Peter Bowen, yeye anasema, kama mwanamke ni mnywaji pombe na anahitaji mimba, inabidi kila jioni anywe glasi moja ya ya mvinyo (wine) kabla hajaenda kulala. Anazungumzia mwanamke mwenye mume au mpenzi na mbaye mumewe yuko tayari kukutana naye kila anapohitaji. Vinginevyo mvinyo huo unaweza kuwa kero kwake. Dk. Bowen anasema, kusongeka kimawazo huwa kunawafanya wanawake wengi kushindwa kupata ujauzito. Hivyo kupata kitulizo cha mawazo cha muda mfupi kunaweza kusaidia.