Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Wakuu Kwema?
Nimekaa nimetafakari nimeona wacha niwasaidie hawa watani zangu. Afande Sele aliwahi kuuliza "Mfano Yanga Ikifa Simba itacheza na Nani?", hivyo hata kama ni Mwana Msimbazi sio vibaya nikiwasaidia.
Ligi Kuu ina timu 20. Ukiiondoa Simba S.C hakuna timu katika 18 zilizobaki zinazoikuta Yanga kwa ubora wa matokeo Kiwanjani, msimamo wa Ligi ni Shahid katika hili.
Ukiondoa Simba iliyofungwa mabao 8, Yanga ndio ya pili kwa kufungwa mabao machache kuliko timu zote ikiwa imelingana na Tanzania Prison ambao wote wamefungwa mabao 14.
Ukiondoa Simba iliyofunga mabao 45, Yanga ndio ya pili kwa kufunga mabao mengi ikiwa imefunga mabao 36.
Yanga sasa inaongoza Ligi japo ni swala la muda tu itaondolewa kileleni lakini itakua ya pili, Yanga imefungwa mechi chache kuliko timu ingine yoyote ile ya Ligi Kuu, why wanapoteana? Why hawaelewani? Jibu ni kua kivuli cha Simba ndio kinawatisha.
Yanga kila akiifikiria Simba anakosa raha. Anawaza kua Simba atamkuta na kumpita tu siku moja. Yanga anataka kua pale aliko Simba kwa Sasa.
Anachopaswa kujua Yanga ni kua kwa sasa Simba sio level yao tena. Mpira wa Scotland Giants ni Glasgow Rangers na Celtic Glasgow. Hawa wamekua wakipokezana miaka nenda, miaka rudi. Waliobaki wote hushindana kutafuta nani atakua wa tatu nyuma ya hawa wawili.
Mpira wetu nao ulikua hivyo kama wa Scotland. Ila sasa umebadilika. Giant ni Simba S.C tu. Yanga atatakiwa kushindana na kina Azam kutafuta nani atakua wa pili. Kombe analocheza Simba sasa la Africa angekua Yanga asingefika hapo. Na siku akibahatika kuingia basi atakua kama Petro de Luanda au El Mereikh.
Yanga wakitambua kua Simba sio level yao kwa sasa wakaacha KUJILINGANISHA nayo wakabaki wanafanya ya kwao wanayoyaweza basi watakya salama. Maana wataacha kuweweseka na kivuli cha Simba, kila wanachogusa wanawaza itakuaje kwa Simba mwishowe wanachanganyikiwa.