Tatizo la Yanga ni "kujilinganisha na Simba"

Tatizo la Yanga ni "kujilinganisha na Simba"

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
Wakuu Kwema?

Nimekaa nimetafakari nimeona wacha niwasaidie hawa watani zangu. Afande Sele aliwahi kuuliza "Mfano Yanga Ikifa Simba itacheza na Nani?", hivyo hata kama ni Mwana Msimbazi sio vibaya nikiwasaidia.

Ligi Kuu ina timu 20. Ukiiondoa Simba S.C hakuna timu katika 18 zilizobaki zinazoikuta Yanga kwa ubora wa matokeo Kiwanjani, msimamo wa Ligi ni Shahid katika hili.

Ukiondoa Simba iliyofungwa mabao 8, Yanga ndio ya pili kwa kufungwa mabao machache kuliko timu zote ikiwa imelingana na Tanzania Prison ambao wote wamefungwa mabao 14.

Ukiondoa Simba iliyofunga mabao 45, Yanga ndio ya pili kwa kufunga mabao mengi ikiwa imefunga mabao 36.

Yanga sasa inaongoza Ligi japo ni swala la muda tu itaondolewa kileleni lakini itakua ya pili, Yanga imefungwa mechi chache kuliko timu ingine yoyote ile ya Ligi Kuu, why wanapoteana? Why hawaelewani? Jibu ni kua kivuli cha Simba ndio kinawatisha.

Yanga kila akiifikiria Simba anakosa raha. Anawaza kua Simba atamkuta na kumpita tu siku moja. Yanga anataka kua pale aliko Simba kwa Sasa.

Anachopaswa kujua Yanga ni kua kwa sasa Simba sio level yao tena. Mpira wa Scotland Giants ni Glasgow Rangers na Celtic Glasgow. Hawa wamekua wakipokezana miaka nenda, miaka rudi. Waliobaki wote hushindana kutafuta nani atakua wa tatu nyuma ya hawa wawili.

Mpira wetu nao ulikua hivyo kama wa Scotland. Ila sasa umebadilika. Giant ni Simba S.C tu. Yanga atatakiwa kushindana na kina Azam kutafuta nani atakua wa pili. Kombe analocheza Simba sasa la Africa angekua Yanga asingefika hapo. Na siku akibahatika kuingia basi atakua kama Petro de Luanda au El Mereikh.

Yanga wakitambua kua Simba sio level yao kwa sasa wakaacha KUJILINGANISHA nayo wakabaki wanafanya ya kwao wanayoyaweza basi watakya salama. Maana wataacha kuweweseka na kivuli cha Simba, kila wanachogusa wanawaza itakuaje kwa Simba mwishowe wanachanganyikiwa.
 
Hili ndio tatizo la Tanzania. Kipimo ni Usimba na Uyanga!

Kama kuna kitu Yanga wamefanikiwa mwaka huu ni kuwaaminisha washabiki wao kuwa mwaka huu hakuna mpinzani!

Yanga wakiwaandaa mashabiki wao,kuwa ufalme was Simba ea miaka mitatu umekwisha!

Yanga walitamba miaka minne ya Manji!

Bahati mbaya haukuwa uwekezaji endelevu, leo wahaha!

Yanga sio timu mbaya,Ila matarajio ni makubwa ndio maana wanaishi kwa shinikizo kubwa!

GSM wameanikiwa Sana kyk propaganda!

Wameteka vvyombo vya habari kuwasaidia!

Angalia jinsi Mchezaji Fiston alivopaishwa,kumbe ana tofauti ndogo Sana na Sarpong
 
Hili ndio tatizo la Tanzania. Kipimo ni Usimba na Uyanga!

Kama kuna kitu Yanga wamefanikiwa mwaka huu ni kuwaaminisha washabiki wao kuwa mwaka huu hakuna mpinzani!..
Duh, mzee si usome ulichoandika kabla hujapost? Ni ngumu kusoma ulichoandika
 
Minashangaa sana, ligi wamepoteza mechi moja tu na wanaongoza, sasa wanaweweseka nini?

Hata wasipochukua ligi watakua nafasi ya pili, shida ni kama mleta mada alivyosema.

Kujilinganisha na Simba.

Na kuaminishwa kubeba ubingwa wa ligi.
 
Timu moja inabeba kombe miaka minne. daah hata ingekuwa mimi lazima nidate
Mkuu, hivi Borussia Dortmund anaweza kuweweseka kwa Bayern kubeba kombe miaka nenda miaka rudi? Jibu ni hapana sababu BVB washajua kua nafasi ya kwanza always ina Mwenyewe, so wao ni kupigania ya pili na kina RB Leipzig.

Sasa hata hapa ndicho Yanga wanatakiwa kukifanya. Simba iko pale ilipo sababu imewekeza kwa umakini, imesajili kwa umakini. Yanga iridhike na nafasi iliyoko, isitishike na kasi ya Simba. Huwezi kupanda nyasi ukavuna mahindi.

Wafanye tu vile vilivyo ndani ya uwezo wao.
 
Yanga wanajiwekea malengo makubwa halafu wanashindwa kuyafikia, Yanga kujilinganisha na Simba ni kujitafutia kuugua pressure tu, waache hayo mambo waishi kwa amani wao level zao ni Azam.

Kwani muungwana akisema; "Sisi hatuna uwezo wowote" kuna shida gani?
 
Yanga wanajiwekea malengo makubwa halafu wanashindwa kuyafikia, Yanga kujilinganisha na Simba ni kujitafutia kuugua pressure tu, waache hayo mambo waishi kwa amani wao level zao ni Azam.

Kwani muungwana akisema; "Sisi hatuna uwezo wowote" kuna shida gani?!.
ni sawa na zile biashara za kuwekeza milioni upate milioni 100
 
Mashabiki wa yanga wanadekezwa sana hasa kipindi hiki.

mpira ni gharama.na gharama ya kwanza kabisa ni uvumilivu.

Katika
Wachezaji wote wa yanga hakuna aliyedumu pale walau kwa miezi 24 ukiondoa makapu na kaseke.

Pale simba; boko, chama, mkude,zimbwe,kagere, manula,kapombe, hd wana misimu zaidi ya 3-6
hao ni baadhi tu.
dirisha lijalo la usajiri timu isiguswe..
 
Minashangaa sana, ligi wamepoteza mechi moja tu na wanaongoza, sasa wanaweweseka nini?

Hata wasipochukua ligi watakua nafasi ya pili, shida ni kama mleta mada alivyosema.

Kujilinganisha na Simba.

Na kuaminishwa kubeba ubingwa wa ligi.
Ikitokea kwamba Simba amecheza match zake 4 zilizo baki then asimpite Yanga. Baasi hao Utopolo ndio watajiona wajinga wa dunia
 
Ikitokea kwamba Simba amecheza match zake 4 zilizo baki then asimpite Yanga. Baasi hao Utopolo ndio watajiona wajinga wa dunia
Sema Simba atakapokua akicheza na Yanga nae atacheza, hivyo viporo sio rahisi kuisha leo. Ndo kusema kua Yanga wacha a enjoy tu pale kileleni kwa Sasa.

Siku tukirudi pale ndo hakuna kutoka mpaka ligi inaisha.
 
Wewe huwezi kujilinganisha na timu ya wananchi iliyosaidia kuleta uhuru nchi hii nani asiyejua kuwa ninyi mlikuwa upande wa wakoloni kujilinganisha ba Yanga ni sawa na mgeni umemkaribisha nyumbani kwake halafu baadaye na yeye anadhani ana haki sawa na mwenye nyumba acha bwana Yanga ni kitu kingine katika nchi hii
 
Back
Top Bottom