Tatizo lolote la PC/device

wakuu natumia hp elitebook840 tatizo haiwak mara ya mwisho kutumia jana usiku iliisha chaji leo nimechaji ili nitumie nawasha haiwak msaada inaweza kua shida nn?
 
wakuu natumia hp elitebook840 tatizo haiwak mara ya mwisho kutumia jana usiku iliisha chaji leo nimechaji ili nitumie nawasha haiwak msaada inaweza kua shida nn?

karibu ofisin kwangu tabata nikutatulie tatizo, au naweza fika ulipo gharama ni kidogo sana
 
mkuu una maanisha kuwa windows activation screen inakuzuia usiiingie kwenye account yako au display ipo black ila cpu inawaka si ndio ?
 
Nipo uncle 🙂
Siku ile nilikuwa nataka kuiondoa no hii 0xc0000005 but nikaamua kushusha window nikaweka ten but ikawa screen inaonesha imeminya hata ukitumia vcl player ikawa hai view video kubwa hata uki crop bado inakataa ikabidi nirudishe window 7 je hili ni tatizo gani hata browser ikawa haipatikani window ten ingawa ipo chap kufunguka desktop, hii ni nini tatizo ingawa aliyenijazia window ikamshinda niliisha malizana naye na ilipomshinda akairudishia 7 ile ile
 
Wadau wapi ntapata fundi mzuri kwa hapa Dar wa old laptop yangu aina ya Fujistu siemens anibadilishie speaker na vifaa vichache
 
mkuu hilo ni ishu ya resolution, na inapokuwa na picha ndogo ni tatizo linalotokana na driver ambayo imekuwa installed labda ili-corrupt, japo kuna njia huyo fundi wak alitakiwa apitie kabla ajarudisha windows 7, ni kumaximazime resolution kwenye desktop and displays settings. kama alipitia huko pia ikagoma inawezekana ikawa ni drivers au hiyo copy ya windows ilikuwa ina Tatizo pia.
 
PC yangu aina ya HP, nikiiwasha inawaka lakini inadisplay picha kwa mbali sana.
Yaani hadi nimulike kwa tochi ndo naona maandishi. Nimejaribu njia zote za kuongeza mwanga lakini wapi.
Nimejaribu kuunganisha kwenye flat TV inadispalay maandishi vizuri TU.
Je hapo wajuzi tatizo ni nini?
 
Nahitaji window 11, mtu wa kuifanyia installation ikiwa og itakuwa poa zaidi, ikiwa full na office
 

Mkuu kama ni PC za zamani basi hiyo ishu ni ya INVERTER, ni kifaa hivi kidogo kipo chini ya kioo cha laptop, ukiifungua hapo juu ndio ambayo inasadia kufanya regulation ya mwanga, so unaweza kwenda kwa fundi akaifungua na kukufungia mpya kisha itarudi vizuri.

Ila kama ni PC mpya hapo inabidi ubadili kioo.
 
PC yangu imechola kwenye kioo hivyo natafuta kioo kipya. Vile vile casing imechakaa Sana nahitaji kubadisha wapi nitapa Geita
Nina HP laptop, sasa kila nikianza kuboot inadisplay kisha inaganda hapo ktk hatua za awali kabisa! Tatizo nini mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app


 
Computer yako inachelewa sana kuwaka.. Baada ya kuweka password
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…