Tatizo lolote la PC/device

Tatizo lolote la PC/device

Habari zenu wakuu!!

Nimeanzisha uzi huu tusaidiane kwenye matatizo yoyote yanayohusiana na technology kwa ujumla, kwa mtu yeyote ambae ana tatizo na ambaye anaweza kumsaidia mtu tatizo LOLOTE linalohusiana na computer, simu (zaidi smartphone) au devices zozote ambazo zinahusiana na teknolojia mpya.

Karibuni sana wakuu

Pirate
Habari wakuu.

Naomba msaada, printer yangu ya Epson L382 haiwezi print colored. Nimeinunua hata mwaka bado haujakata. Nipo Dar es salaam
 
Habari wakuu.

Naomba msaada, printer yangu ya Epson L382 haiwezi print colored. Nimeinunua hata mwaka bado haujakata. Nipo Dar es salaam
Printer zinakuwa na wino mweusi na wa Rangi, pengine wino wa Rangi umeisha?
 
Wino uko full color zote, sijui shida iko wapi?
Jaribu kwenda setting ama control panel tafuta printer yako Kisha right click Kisha properties kama kuna setting unaweza badili. Grayscale ndio hio black and white.
 
Nina laptop yangu dell latitude kila nikiitumia feni inazingua Kwa Kasi na matokeo yake inachemka sana na kujizima nimejaribu kubadili feni pamoja na heat sink lakini bado inasumbua tatizo ni nini wakuu?
 
Msaada wakuu..pC yangu number za kwenye keyboard hazifabyi Kazi..Ila alphabet ziko okey ..shida inaweza kuwa nini..natumia HP
 
Mkuu unamaanisha feni inazunguka Kasi Sana au inazingua???
 
Kama kuna vitu kwenye simu ukivifuta havifutiki unafanyaje?
 
Pc yangu ilikuwa ya plastic, imevunjika house take Ila unapiga kazi Kama kawaida, je bei ya housing mpya sh. Ngapi kwa anayejua?, Pc ni Lenovo ideapad100
Ulifanikiwa kuipata ? Tuma picha kama bado
 
Nina laptop yangu dell latitude kila nikiitumia feni inazingua Kwa Kasi na matokeo yake inachemka sana na kujizima nimejaribu kubadili feni pamoja na heat sink lakini bado inasumbua tatizo ni nini wakuu?
Ulipotoa heatsink uli apply thermo paste/ compound ?
 
Msaada wakuu..pC yangu number za kwenye keyboard hazifabyi Kazi..Ila alphabet ziko okey ..shida inaweza kuwa nini..natumia HP
Hizo alphabet zore zipo ok umetest? Kama Hiyo ni mini keyboard , jaribu ku bonyeza NUM Lock kisha ndio ubonyeze upande wa namba
 
LAPTOP YANGU INA MIEZI NANE TU, BAADHI YA BUTTONS ZA KEY BOARD ZIMEACHA KURESPOND, MPAKA URUDIE KUCKLIC MARA YINGI SANA, JE NINI SHIDA?
 
Hizo alphabet zore zipo ok umetest? Kama Hiyo ni mini keyboard , jaribu ku bonyeza NUM Lock kisha ndio ubonyeze upande wa namba
Alphabet ziko sawa..shida iko kwa namba za juu ya alphabet hazifanyi Kazi...pamoja na namba za pemben zile za pembeni ya alphabet ,japo hizi za.pemben Kuna siku zinafanya Kazi,Kuna siku hazifanyi kabisa .

Je hiyo NUM Lock naipata wapi kwenye laptop
 
Back
Top Bottom