Tatizo lolote la PC/device

Tatizo lolote la PC/device

Pc kuganda kwny boot mode tatzo Nini wakuu ukuminya escape inarud apo apo
 
Pc kuganda kwny boot mode tatzo Nini wakuu ukuminya escape inarud apo apo
okay mkuu kama ujapata ufumbuzi bado,,,,
hili tatizo ni uwa linasababishwa na vitu vitofauti kama.
  1. kama umefanya updates hivi karibuni
  2. tatizo kwenye drivers
  3. MBR corruption
  4. apps nyingi kwenye kuwasha Pc
  5. Windows System corrupt
Na jinsi ya kusolve ni njia nyingi kidogo ila, unaweza kujaribu hizi baadhi
  • wakati unawasha Pc yako Bonyeza F8 hadi ikupeleke kwenye boot menu baada ya hapo chagua Safe mode baada ya kuwaka kwenye safe mode, fungua Run kisha andika sysdm.cpl kisha OK baada ya kufungua chagua Advance>Settings kisha inabidi uondoe tiki kwenye Automatically restart. kisha baada ya hapa restart kawaida uone.
  • Njia nyingine kama unaweza kufungua pC yako, kisha toa CMOS battery kisha irudishe kwa kuigeuza chini juu kwa sekunde 15 tu kisha irudishie kama kawaida na funga pc yako kisha jaribu kuwasha tena.
  • Njia ya mwisho ni Kufanya Restore au Clean format ya windows Os yako.
 
Mkuu naweza pata wapi kioo cha hii monitor ni nchi 21(wide) kwa 30cm (length)
Ilipata damage nikiiwasha inavilia wino ,yaani haionesh View attachment 2359799
Mkuu kwa sasa sipo Tz na namba za jamaa wa Kariakoo nyingi nilipoteza, kama aupo mbali na DSM unaweza kwenda Kkoo hasa kwenye maduka ya Pc kwa jumla uwezi kukosa hii.
 
PC yangu
Inagoma kufungua docs in word mpaka utumie option ya open with
Ni ikifungua hiyo doc huwezi edit chochote

Shida Iko wapi ?
Mkuu je ikikubali kufungua hiyo docs file uwa inafungua kupitia app gani kwenye Pc yako??
 
Mkuu me Disck Top computer nikichomeka USB cable nikakonnect sim haisomi bali inaniletea ujumbe kuwa
⚠️USB Device Not Recognazed
one of the USB device attached to this commputer has malfunction, and Window does not recognize it.
For assistance in solving this problem, click this message.

𝐍𝐢𝐭𝐚𝐥𝐢𝐬𝐨𝐥𝐯𝐞 𝐯𝐢𝐩 𝐦𝐤𝐮𝐮
Mkuu kama hiyo inatokea kwenye Usb Port moja tu basi ni port ndio ina tatizo lakini kama inatokea kwenye port zote basi tatizo lipo kwenye Usb chord ya simu yako au Usb Port ya simu yako.
 
Nina HP inazingua ukiikunjua inablink kama inawaka then inazima
Mwanzo ilianza inawaka masaa kadhaa, baadaye ikaja ikiwaka inakaa dakika kadhaa. Hivi sasa hata sekunde haiwezi

Nitatuma descriptions for further explanation
Mkuu kama bado ujafanikiwa unaweza kuelezea vizuri tatizo?
 
PC yangu ni mpya lakini nikijiunga kwenye vikao vya zoom na Microsoft Teams haitaki kuunganisha sauti, hata nikirusuhusu 'Join the meeting with device audio'

Pia nimeallow/nimetoa permission app zote zitumie Mic ya PC. Bado shida ipo palepale
 
PC yangu ni mpya lakini nikijiunga kwenye vikao vya zoom na Microsoft Teams haitaki kuunganisha sauti, hata nikirusuhusu 'Join the meeting with device audio'

Pia nimeallow/nimetoa permission app zote zitumie Mic ya PC. Bado shida ipo palepale
Kama umefanya hivyo vyote na bado jaribu hii nyia ya mwisho,
Fungua RUN kisha andika mmsys.cpl kisha OK
Nenda kwenye Recording Tab, kisha angalia kama microphone yako ipo enabled baada ya hapo set as Default kisha Ok, Kisha hapo hapo Right-click Microphone > Properties>Levels iweke hadi 100.
 
Wakuu pc yangu ina tatizo la kunasa gafla na inatoa muungurumo kama jenereta kwa chini shida nini wakuu nateseka sana
 
Nataka kuunganisha laptop yangu na na Screen mbili za desktop.
Nafanyaje
 
Naombeni msaada nataka kununu pc kwa izi features ni nzuri kwa matumizi ya graphics?
Hp pavilion 14

SYSTEM

Manufacturer: HP

Model: HP Pavilion Laptop 14.

Processor: Intel(R)Core(TM) i5- 7200CPU

(7th Generation)

@2.20GHZ, ~2.5GHZ

Ram 4gb Ddr4

Hard disk drive: 500gb

DISPLAY

Name: Intel (R)HD Graphics 620

Manufacturer: Intel corporation Chip type: Intel (R) HD Graphics Family

Device type : Full Display Device

Approx. Total Memory: 4166MB

Display Memory: (VRAM) 128MB

Shared Memory: 4038MB

RENDER

Name : NVIDIA Geforce 940MX

Manufacturer: NVIDIA

Approx. Total Memory: 4118MB

Display Memory (VRAM) : 2080 MB

Shared Memory: 2038 MB

SOUND

Name: Speakers (3- High Definition Audio Device)

BANG & OLFUSEN

Screen size: 14 inches
 
Na PC yang HP natumia window 10 shida ipo kwenye kuongeza mwanga(brightness) nikibonya fn then button za mwanga kweny keyboard inaniletea frame to za mwanga ila mwanga hauongezek shida ni nn?na Kama drives nili update zote nili activate mbka ya graphics
1. Weka graphics driver
 
Mkuu kama ni PC za zamani basi hiyo ishu ni ya INVERTER, ni kifaa hivi kidogo kipo chini ya kioo cha laptop, ukiifungua hapo juu ndio ambayo inasadia kufanya regulation ya mwanga, so unaweza kwenda kwa fundi akaifungua na kukufungia mpya kisha itarudi vizuri.

Ila kama ni PC mpya hapo inabidi ubadili kioo.
Nilikutana na ishu ya kushangaza, pc dell latitude d series, nilabadili inverter ikakataa, kubadili kioo ikakubali
 
Msaada laptop aina ya fujitsu zipo mbili moja haiwaki kabisaaaaa ila nilijaribu Kutoa ram, betri, hdd na Kuweka kwenye laptop nyingine aina hiyo hiyo ile pc Ikawaka nikajua issue sio ram wala betri wala Hdd, pc ya pili yenyewe inaonyesha kuwa chaji inaingia ila haiwaki kabisaaaaa so msaada tatizo nini
 
Wakuu Nina Pc Dell latitude E6420 nimeiwasha haioneshi kitu inatoa rangi ya dark blue nimechomoa betri na kuirudishia ikaonesha hivi
20230511_103618.jpg
20230510_174806.jpg

Nime click F2 ikaniletea settings naomba kuelekezwa setting yake.
 
Msaada laptop aina ya fujitsu zipo mbili moja haiwaki kabisaaaaa ila nilijaribu Kutoa ram, betri, hdd na Kuweka kwenye laptop nyingine aina hiyo hiyo ile pc Ikawaka nikajua issue sio ram wala betri wala Hdd, pc ya pili yenyewe inaonyesha kuwa chaji inaingia ila haiwaki kabisaaaaa so msaada tatizo nini
Mkuu hizo pc mbili zote ni aina moja ambazo ulijaribu hizo ram,hdd,betri?
Kutokuwa kwa Pc uwa kunahusihwa na vitu vingi ila cha kwanza ukichomeka charger inaonyesha inacharge na ukibonyeza button ya kuwashia inatoa indicators yoyote au kuna Taa yoyote inawaka kwenye kiboard yako?
nikipata majibu hayo ndipo nitajua jinsi ya kukusaidia mkuu.
 
Back
Top Bottom