Tatizo na Nyumba Ndogo...

Huyo ndiyo Babu Aspirin,

Hata hivyo jipe moyo kwani bado watoto wazuri wapo wengi na wengine unawajua mwenyewe...Sina sababu ya kukutajia!!!

Au umesahau?

Babu DC!!
Nafurahi hata wewe kaka yangu hilo unalitambua?
Ni ngumu kumsahau 'mtoto mzuri'...

Aspirin anaifanya ionekane kama vile hakuna mahusiano bila infidelity (Naweza kuwa nakosea kumsoma) ilhali sivyo ilivyo.
 
hakuna ujustifiable justification my dear, kama amejustify ina maana ndio justification yenyewe:rant::rant::rant:

ntakutandika bakora asa ivi, naona unaleta utani asubuhi hii:rant::rant::rant::rant:
Umeanza lini kuwa abusive?

Wewe na aspirin ndo mnaleta mzaha kwenye hili

Hebu kwanza niulize hapa hapa MTM. Kuna mahali humu watu wamemwambia MJ1 kuwa hali aliyonayo ni alama kuwa 'amekuwa'

Hivi ukikua ndo hujali tena kama mwenzi anaweza kuwa na nyumba ndogo? Ndo hujali tena kuhusu uaminifu, maradhi, heshima ya mahusiano au ni nini hasa?
 

..., sasa tumeelewana; hata mimi niko kwenye hao TUSIOJIHUSISHA KABISA, ASILANI!! ila hapa nazungumzia context yake na kwamba siishi porini

watu tunasahau kabisa post namba wani ya hii sredi, na kuanza kuleta hoja nyingine... nakumbuka thread ya Boss ya namna ya ku-keep nyumba ndogo ilichangiwa; na ya RR ya kupinga nyumba ndogo ilichangiwa... sasa hapa tunataka ku-connect zote mbili ndio tatizo

tumesahau dhima
 
Nafurahi hata wewe kaka yangu hilo unalitambua?
Ni ngumu kumsahau 'mtoto mzuri'...

Aspirin anaifanya ionekane kama vile hakuna mahusiano bila infidelity (Naweza kuwa nakosea kumsoma) ilhali sivyo ilivyo.

Labda kwa sababu ya umri huu unaokimbia kama mshale wa sekunde...mie namuelewa kwamba infedelity ni jambo la kawaida sana kwenye jamii zetu....Yaani, watu wengi (sijui ni asilimia ngapi) ni waumini wa hii kitu...

Bahati nzuri wapo watu wachache ambao si waumini na wamedumu katika hiyo hali kwa muda mrefu katika maisha yao...bila kulazimishwa na masharti ya kazi yao kama wale ndugu zetu wanaojifungia kwenye majumba ya watumishi wa Bwana na kuwakwepa wadau wao!!

Kwa hiyo usihofu sana au kutishwa na data hizo za Babu mwenzangu, Asprin......

Babu DC
 
Nyumba ndogo zimeanza kukubalika eeeh?Kina mama mkiwezeshwa huwa mnaweza kweli, lol!
 

Haswaaaaaaaa,

Wengi wentu tunaongea mambo yanayotokea kwenye jamaa na naamini ni watu wachache wanajiongelea...

Kuna watu hawa wakieweka confessions zao hapa hawataaminika kabisa....

Babu DC!!
 
hapo red hongera mkuu.huwa najiuliza kwanini ufanye kitu unajua kabisa ni kosa na usaliti.mimi nilishajiapiza kama kuna dhambi sitofanya tena ni kutembea na mume wa mtu. hata haina maana .
 
Hiyo ni dalili ya kukua dada, hata siku ikitokea unakua kwenye hali nzuri ya kufanya maamuzi na kukabiliana na ukweli. Bahati mbaya sana hasa sisi wanawake tunajiwekea nadhiri za kwamba haitakaa itokee mume kuwa na nyumba ndogo. Natamani hata wakati wa mafundisho ya ndoa wangekuwa wanasema ukweli kwamba inaweza kutokea ili mtu ajijue anaingia kwenye uhalisia wa mahusiano ambayo unaishi na mtu miaka nenda rudi bila likizo (kama kazi zenu sio za kusafiri ndio kasheshe hamna likizo) na kuna dhoruba zinaweza kutokea. Kwenye maisha ya ndoa mnajijua kama mmekua pale ambapo limepita wimbi la infidelity kwa pande zote yani kwa mume na mke na mkaweza kukaa meza moja kujadili na kusonga mbele na ndoa au kufanya maamuzi sahihi ya kutunza watoto hata mkiwa mmetengana bila ya kulaumiana kwamba mmoja ni shetani na mwingine ni malaika. Kama wimbi hilo halijapita ni vema kujadiliana likitokea mtafanyaje.
 
hapo red hongera mkuu.huwa najiuliza kwanini ufanye kitu unajua kabisa ni kosa na usaliti.mimi nilishajiapiza kama kuna dhambi sitofanya tena ni kutembea na mume wa mtu. hata haina maana .


Kumbe na wewe sasa umekua kama MJ1!!!

Karibu sana kwenye club!!


Babu DC!!
 
Duh, yaani mie ni generation ya zamani
Najua hivi vitu vipo tu

Generation hii ndo mnatakiwa mvipige vita
Maana hamvielewi wala kuvikubali

Mie nasema kwa anayeshindwa kuwa na mmoja Use 'condom' ya nyumba dongo
Do the wrong thing right.

Ukitaka kujua hali halisi, maambukizi ya VVU ni makubwa kwa wana ndoa.
nyumba ndogo free generation it begins with you

 
Kwa atheist siwezi waongelea maana sijui wanapimaje baya na zuri

Ila kwa wenye dini, ni dhambi ngapi tunafanya?
Kwani misahafu haituambii ni dhambi?

Dhambi ilianza bustani ya eden, huu ni mwendelezo tu
hapo red hongera mkuu.huwa najiuliza kwanini ufanye kitu unajua kabisa ni kosa na usaliti.mimi nilishajiapiza kama kuna dhambi sitofanya tena ni kutembea na mume wa mtu. hata haina maana .
 
hapo red hongera mkuu.huwa najiuliza kwanini ufanye kitu unajua kabisa ni kosa na usaliti.mimi nilishajiapiza kama kuna dhambi sitofanya tena ni kutembea na mume wa mtu. hata haina maana .


Kumbe na wewe sasa umekua kama MJ1!!!

Karibu sana kwenye club!!


Babu DC!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…