Tatizo Serikali iliyopo haikuchaguliwa kihalali na imeshavunda bado kuoza

Tatizo Serikali iliyopo haikuchaguliwa kihalali na imeshavunda bado kuoza

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
hakuna asiejua kuwa ushindi wa CCM katika uchaguzi Mkuu uliopita ,ulikuwa ushindi wa kulazimisha liwe liwalo na mwishowe kuapishwa waliosadikishwa kuwa wameshinda.

Asilimia kubwa ni waumini hapa Tanzania ,baada ya dhulma milango ya dua ilikuwa wazi kwa waliodhulumiwa, yanayotokea leo ni mambo ya kuabika ndani ya CCM, laana ya uchaguzi inawapiga MaCCM.

Wananchi wanapodai ufanyike uchaguzi wa wazi kwa haki na uhuru,anaeshinda au wanaoshinda wapewe ushindi wao,wanamaanisha hakutakuwa na wa kubeba msalaba, lakini leo kila siku serikali inachanika na wametia viraka hadi ni kiraka juu ya kiraka, dhulma kitu kibaya sana, wapiga domo wakubwa wa CCM leo wanapita wakizomewa, akina Bashiru na Polepole na wengine, hao watetezi wa kuitetea CCM leo wanalana nyama, kama si laana ni kitu gani?

Mwisho wanao ielekeza nchi ni kuivuruga maana aibu yao haibebeki na kila mmoja wao anajiona yeye yupo sawa kuliko mwengine, si mkubwa si mdogo. Laana sio ndogo maana walioshirikia na kushinda kwa dhulma wamo mashehe na mapadre wote wametenda dhambi unategemea ikishuka laana kutakuwa na salama?
 
Back
Top Bottom