baba anjela
JF-Expert Member
- Mar 17, 2013
- 431
- 310
Binafsi naona tatizo la baadhi ya watu kugomea chanjo limesababishwa na serikali yenyewe na ( viongozi wa dini). Kwa kawaida kunapotokea upotoshwaji wowote kwa makusudi au kwa Bahati mbaya utakaofanywa na Kiongozi wa serikali. Kinachofata ni uwajibikaji. Kwa kuwajibishwa au yeye kujiwajibisha mwenyewe. Ni vigumu sana kwa MTU yoyote kukubali maelezo Juu ya chanjo yanayotolewa na watu walewale ambao mwanzo walitumia Nguvu kubwa kupinga uletaji wa chanjo na ubora wa chanjo hizo.
Viongozi hawa wangejiuzulu au kuondolewa na serikali kupisha sura Mpya na maelezo mapya Juu ya ukweli wa chanjo.
Bila kufanya hivyo hofu na Mashaka vitaendelea kuwepo ...lakini pia hawa viongozi hawana confidence ya kueleza hiki wanachotueleza sasa...sababu wanazikumbuka kauli zao
UPANDE WA VIONGOZI WA DINI PIA KUNA TATIZO
Viongozi wa dini ...wakatuaminisha tumeomba na CORONA imekwishwa Tanzania. Leo nao wako kimya, wengine kauli zao zimebadilika, Kwani Mungu kabadilika si ni yuleyule kama alituponya CORONA ya kwanza sasa kwa nini tusimwombe tena Juu ya hii KORONA Mpya ...au Magufuli kaondoka na Mungu wake.
Tena viongozi wa dini wakampa Magufuli certificate ya ushindi, kwa kaishinda korona kwa kumtanguliza Mungu mbele. .Narudia viongozi wa dini na wauliza tena ...Magufuli kaondoka na Mungu?
Wananchi tumechezewa sana....hawa viongozi wa serikali wawajibishwe kama kweli viongozi wetu mnatupenda wananchi wenu...
Walichokifanya hawa viongozi hakistahili msamaha hata kidogo.
Na viongozi wa dini Mungu hatowaacha kamwe mlituaminisha CORONA imekweshwa na sadaka za Shukrani kwa Mungu tukatoa na mkazipokea sadaka zetu.
"sasa najiuliza nani anawalinda hawa viongozi wa serikali waliopotosha taifa??" Na je walifanya upotoshaji huu kwa faida ya nani na kwa nini?...Je ni kwa Bahati mbaya au kwa makusudi..?

- Walitumia Nguvu nyingi kutuaminisha na tukakubali na kutekeleza..mfano.
- Nyungu - mpaka Mawaziri, wabunge wanaposti picha wakipiga Nyungu
- Michanganyiko ya mapilipili, malimao na tangawizi ...tukapata mpaka na vidonda vya tumbo....
- Ndege ikatumwa kwenda kuleta dawa ya CORONA,,( picha zikatumwa mitandaoni tena si kwa Bahati mbaya ,waziri anakunywa dawa ya CORONA) ....mpaka Leo kimya.