theprogrammer C++
Senior Member
- May 17, 2013
- 150
- 385
Mimi naona kuna kitu CCM inapaswa kukielewa vizuri kuhusu Watanzania. Watanzania kwa ujumla ni watu watulivu sana. Wengi hawataki maandamano, hawataki vurugu, hawataki nchi isambaratike. Mwananchi wa kawaida anataka maisha yake, biashara yake, familia yake na amani yake. Lakini pamoja na hayo yote, anataka kitu kimoja kidogo sana... HAKI YA KUCHAGUA
Anataka akifika kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa mtaa awe na mtu zaidi ya mmoja wa kuchagua. Anataka diwani awe mtu anayemtaka yeye, sio mtu ambaye tayari ameamuliwa. Anataka mbunge amchague kwa kura yake. Na mwisho rais amchague kwa kura yake. Hii feeling ilikuepo kabla ya 2015,baada ya hapo kwa chama tawala kutaka shortcut ikaharibu.
Kwa mtazamo wangu tatizo lilianza sana baada ya 2015. Magufuli alipokuja alitaka ku-consolidate power haraka sana, kutoka level moja kwenda nyingine. Upinzani ukabanwa, political activities zikapungua, watu wakaogopa, wengine wakahamia CCM na kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mambo yakawa mabaya zaidi. Kwa muda mfupi CCM ikawa very powerful, lakini naamini ile ilikuwa shortcut. Shortcut inaweza kukupa control haraka, lakini haimaanishi umejenga political stability ya muda mrefu.
Sasa gharama yake ndio tunayoiona. Ukimnyang’anya mtu option ya kuchagua kwa miaka kadhaa, usishangae siku moja akawa na hasira nyingi kuliko unavyodhani. Na hii haimaanishi kila Mtanzania ni CHADEMA au anataka CCM iondoke. Hapana. Watu wengi hawana shida na CCM yenyewe. Wanataka tu wahisi kwamba kama wanataka CCM, wameichagua CCM...kama wanataka CHADEMA, wameichagua CHADEMA.
Kwa hiyo mimi ningeshauri CCM isione political competition kama threat. Iione kama insurance ya nchi. Wape watu space, waruhusu wapinzani wafanye siasa, waruhusu wananchi wachague viongozi wao kuanzia chini kabisa. Kama CCM bado ina nguvu yake, network yake, historia yake na watu wake, itashinda. Na ikishinda kwenye uwanja ambao kila mtu ameruhusiwa kucheza, hakuna mtu atakayeweza kusema ushindi ulikuwa wa kulazimisha.
Kwa kifupi, Magufuli alifanikiwa sana kujenga nguvu ya CCM kwa muda mfupi, lakini huenda alifanya hivyo kwa gharama ya political space ambayo Tanzania ilikuwa imeanza kuijenga kabla ya 2015. Na sasa gharama hiyo inaonekana. CCM bado ina nguvu kubwa sana. Hawahitaji kutumia nguvu zaidi. Wanaweza tu kurudisha wananchi kwenye feeling kwamba “hii ni nchi yangu, na kura yangu ina maana.”