Tawala nyingi za kiafrika hunguka kutokana na Wakuu wa Nchi kupotoshwa na wapambe wao

Tawala nyingi za kiafrika hunguka kutokana na Wakuu wa Nchi kupotoshwa na wapambe wao

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Kiongozi wa nchi anakuwa na wapambe wa kila namna. Hawa wanakuwa na jukumu la kumjuza mkuu wa nchi juu ya masuala muhimu ya taifa analoongoza .

Hata akina Nkwame Nkurumah walipotoshwa na baadae wakajikuta wanapinduliwa. Maana kiongozi akipotoshwa huwa hasimamii kweli na madhara yake hufanya maamuzi yasiyofaa.

Ni wazi kuwa ili kiongozi wa nchi atawale vizuri lazima apate washauri wazuri ambao watamchana ukweli. Huko nyuma viongozi walipinduliwa kwa mitutu na bastora lakini miaka hii ya ulimwengu wa kidigital mapinduzi hufanyika ndani ya mioyo ya wananchi na hapo wananchi humkataa mkuu wa nchi kwa kila namna.
 
Huyu mtu amerudi, kwani ulipotelea wapi, isije kuwa mambo ya teuzi.
 
Inasemwa kuwa, busara ya kiongozi haitokani na wapambe wazuri bali, wapambe wazuri hutokana na kiongozi mwenye busara.

Ukiona kiongozi ana wapambe wabovu jua tatizo liko kwake.
 
Inasemwa kuwa, busara ya kiongozi haitokani na wapambe wazuri bali, wapambe wazuri hutokana na kiongozi mwenye busara.

Ukiona kiongozi ana wapambe wabovu jua tatizo liko kwake.
[emoji106][emoji106]! Rais Obama aliwahi kuulizwa siri ya mafanikio yake ya urais wa miaka 8 bila kashfa, alijibu hivi, "As a leader, always make sure you are surrounded by smart people ".
 
ni kweli hata Jiwe kaangushwa na wapambe akina Kabudi, Bashiru, kijazi et al
 
[emoji106][emoji106]! Rais Obama aliwahi kuulizwa siri ya mafanikio yake ya urais wa miaka 8 bila kashfa, alijibu hivi, "As a leader, always make sure you are surrounded by smart people ".
Hapa bongo anakuwa salaundedi na waganga njaa
 
Inasemwa kuwa, busara ya kiongozi haitokani na wapambe wazuri bali, wapambe wazuri hutokana na kiongozi mwenye busara.

Ukiona kiongozi ana wapambe wabovu jua tatizo liko kwake.
Ndio maana Prof Baregu alisema hataki awe mshauri wa Mtu Mpumbavu. Maana akiendeleza upumbavu ataonekana anashauriwa upumbavu na mshauri wake.

Ili uwe mshauri wa mtu hakikisha huyo mtu mwenyewe akili anazo.
 
Back
Top Bottom