Tazama baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika majina ya ajira za Ualimu yaliyotolewa. Jina la 'ABADALLAH LEONARD SHONDE lajirudia mara 196

Tazama baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika majina ya ajira za Ualimu yaliyotolewa. Jina la 'ABADALLAH LEONARD SHONDE lajirudia mara 196

Raisi wetu mpendwa Magufuli,sisi wananchi na wanachama wa CCM kipindi cha kampeni tulikuahidi kukupa miaka mitano tena na tukakuomba pindi utakaporudi madarakani ubadilike kwa maana ni mengi uliyafanya katika awamu ilopita lakini mapungufu yalikuwa mengi"unafiki ni mwiko"
Mimi na wanachama wenzangu kwa moyo mmoja tulikuomba ubadilike pindi tutapokupa ridhaa ya kutuongoza tena
Lakini mpaka sasa mwelekeo unaonekana mbaya tukianza na kilichofanyika TAMISEMI
Jana. TAMISEMI wametoa majina ya walimu baada ya miezi miwili tangu ajira zilivyotangazwa cha kusikitisha na kuhuzunisha kuna madudu mle mpaka yanakatisha tamaa,madudu yenyewe ni haya
Mosi ni jina la mtu mmoja kujirudia mara 196 kwa maana hyo kawazibia wengine nafasi lakini pia swali ni inakuaje taasis kubwa kama ile inaweza kufanya kitu cha kijinga namna hyo,lakini katika kufatilia inaonekana kamaliza 2019 na kafeli je hii ina tafsir ipi?
Pili,ni mtu kupangiwa kufundisha hesabu na history,inamaana kuna kombi ya "HKM"
Tatu,ni namna ambayo mmejaza watu certificates tafsiri yake ni nini
Wale wengi walopata wa degree ni wenye watu wao hko je inakuaje kwa watoto wa maskini ambao wengi wao wamekimbilia ualimu
Nimesahau pia mtu kumaliza 2019 na kupangiwa chuo je mtu hyo kamaliza chuo mwaka gani na cheti kapata wapi lakini pia kwenye maombi ilionekana watu wa 2019 hawatakiwi kuomba hzo ajira sasa imekuaje?
Nimalize kusema hivi Raisi MAGUFULI unahitaji kubadilika haraka sana we unajiita raisi wa wanyonge lakini mambo unayofanya yanavuka mipaka
Katika yale majina yalotoka ukiangalia kwa makini kuna madudu mengi je imekuaje watendaje wako wawe na ujasiri wa kufanya hayo kama sio maagizo kutoka kwako???
 
Ule uzi wa warembo&madem wakali uko Jamii photos si mchz

Ova
 
Watz mko vzur, walizan n enzi hzo za kutazamia matokeo internet cafe unakuwa umepewa muda kwahyo unakuwa fasta kutazama jina ulilotaka tu,hongeren kwa kuibua usenge huu
 
Ali Maulid Mtawatawa-1997

Beatrice Apolinary Lyimo -1999

Charles Nyagaya John -1995

Miaka 20+ iliyopita alikuwa wapi hadi mwaka huu ndio waajiriwe?
Wakati miaka ya jakaya alikuwa ana ajiri wote waliohitimu,tena bila kutuma maombi,INA maana wao waligoma kwenda
 
Hii serikaliya hovyo haijawai kutokea sasa sijui hapa wanamuhadaa nani... kiukweli JK licha ya mapungufu yake but alikuwa mtu makini na smart haya mambo usingeweza kuyakuta. JPM na serikali yake hakuna linalofanyika bila kasoro
 
Hahaha inawezekana ni uvcc a.k.a JESHI LA AKIBA mtiifu, au ndiye mwalimu pekee kwenye list nzima.
 
Hapana sio GPA wala nini....kama haya majina nayoyaona mitandaoni yametoka kwa viongozi wa umma tena wa taasisi nyeti basi tunasafari ndefu...

Na Rais asipoliangalia hili nitakuwa na mashaka na anayokuwa anahubiri kila siku.

Penye ukweli tuseme....nimeona jina la mtu kurudiwa zaidi ya mara 100.
Daby watu tunapomlalamikia Rais sio kwamba huwa hatuna akili, tatizo nambari one nchi hii ni huyu top huyu, ametengeneza system fulani fulani hivi za mizngwe mizengwe na uongo uongo mwingi kiasi kwamba kila mtu ameshaadapt kufanya kazi kwa uongo, kuna system za hovyo zinaelekea kuwa culture nchii hii, mfano kupika data.

We unaamini kabisa haya majina hayajapita katika mikono ya watu zaidi ya 10? Sasa imekuwaje yametoka kama yalivyo. Jijibu its either walipanga kudanganya umma au walipanga wafanye hivyo halafu Rais ajifanye ametumbua watu halafu ajipatie misifa isiyokuwa na maana.
 
Mhe.Rais na Wasaidizi wako Mimi Kama Kada Nasema hivi Malalamiko Ni mengi Sana kuhusu hili Suala.Mhe.Rais na wote mnaoona Mliweke sawa Hili.
Mhe.Rais Hawa wanaolalamika pia ni Makada Pia Kuna wakati watachoka Familia zao pia zimejawa na lawama kubwa kwa Serikali yetu.Hili Suala Mhe.Rais liangalie na Upyaaaa na kwa Mapana.Watu Washaanza kukosa imani na Serikali yetu.
 
Huyo aliechapisha nae ni binaadam ana mapungufu yake hivo pengine amekosea tu
Kama kweli kakosea bhas hao sio Tamisemi ni UVCCM Kuna kitu wanafunika Kama sio Covid-19 bhas Kuna kitu kinataka kifunikwe.

Ayo makosa ndo yatajadiliwa afu hamna mtu atakayeajiliwa
 
Ni kweli kuna kadudu mengi kwenye hizi ajira, lakini kwenye jina la huyo msela inaweza kuwa ni makosa ya kiuandishi. Kwenye excel huwa kuna ile ya ku-command heading ya kwenye table itoke kwenye kila page, sasa huyu mwandishi atakuwa alijichanganya badala ya kuhighlight ile line ya kwanza yenye vichwa vya habari aka-highlight kwenye line ya pili. Hayo ndiyo yaliyotokea kwenye hilo jina kujirudia! Wataalam wa excel watanisaidia!
Umewahi kufanya kazi popote ndugu? Kwamba huko ofisini huwa mtu mmoja anajifungia ofisini kwake anaandika majina na kuyatoa mtandaoni? Yeye peke yake? Seriously!
 
Back
Top Bottom