Tazama baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika majina ya ajira za Ualimu yaliyotolewa. Jina la 'ABADALLAH LEONARD SHONDE lajirudia mara 196

Tazama baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika majina ya ajira za Ualimu yaliyotolewa. Jina la 'ABADALLAH LEONARD SHONDE lajirudia mara 196

Kuna mwingine kapangiwa , kufundisha , history , kiswahili na mathematics ,

Sasa sijui huyu alisoma combination ipi?
Huyo alifanya additional Maths ama chuo alikuwa na option ya hisabati
 
Kusema ukweli hizi ajira ni MAGUMASHI, hazina uhalisia wowote. Jina moja linajirudia mara nyngi na kituo ni kilekile.

Kuna wengine wamemaliza fom4 mwaka 2019 eti na wao wameajiriwa.

Swali: Kwanini hawajaandika vyuo walivyosomea? Kwanini hawajaweka serial number?

MUNGU TUNUSURU


---

---

---


PIA SOMA:
= > TAMISEMI yatangaza ajira za walimu shule za msingi na sekondari. Walimu waliopata ajira watakiwa kuripoti kuanzia Desemba mosi, 2020
Sasa toka 1997 anaajiriwa leo ? Hatari na nusu.
 
Tumeomba Takukuru ipelekewa majina yote yaliyopitishwa kuajiriwa kabla hawajaripoti kwenye vitu vya kazi. Tanzania Kuna watu wanatumia fursaya mfumo kupiga deal au kuiba.kuna ufisadi mkubwa Sana Tamisemi hasa kupitia ajira za wasalimu wapya 2020.
Mkuu maisha yanaedelea ujue hilo
 
Na inasemekana huyo Abdallah wa page 196 amemaliza form four 2019 na alipata DIV 1V-31.
 
Mkuu uki resit index namba haibadiliki hata kidogo inabaki ileile kwa sababu hupewi index mpya ila matokeo ndo yatakayobadikika tu.

Uongo ka hujui ka kimya mzee

Kila unapofanya mtihani no ya kituo na yako lazima vibadilike mzee
 
Wee nae kilaza kweli embu angalia index no yake ya form inaonyesha kamaliza shule mwaka 2019
Au mwenzetu hukufika hata form 4 ila kama umefika utaona mfano S.101.202.2017 huyu unajua kamaliza 2017 sasa mtoa mada anamaanisha index no ya huyo Halima inaishia na 2019 je alisoma chuo kwa miaka mi ngapi na kumaliza hiyo kozi iwe certificate au diploma
Hebu mkubali kujulishwa vitu na sisi walimu kwenye hili

Ipo hivi Ukiona namba ya mtihani ya mtahiniwa inaanzia na S01860.....Jua kuwa huyu mtahiniwa ndio Mara yake ya kwanza kufanya huo mtihani wa kidato Cha nne ,lakin Ukiona namba yake ya mtihani inaanzia na P01860.... Fahamu huyu alishawahi kufanya huko nyuma na sasa ameamua kurudia Tena huo mtihani wa kidato Cha nne

Hivvyo huyo anaweza kuwa alikwenda kusoma ualimu na Sasa ameamua kusafisha cheti chake kimatokeo mazuri zaidi
 
Anarudia mtihani wa form four wa nini kama alishafika chuo na akasomea ualimu? How can people be this foolish hata kuchambua vitu virahisi? So kasomaje chuo hadi aje aresit saivi smh
Hjjawahi kusikia mtu ana PhD lakini anasomea certificate ya kitu kingine?
Mbona unaonekana Kama c mtanzania mwezutu vile!
 
Kwanzia baba mpaka watoto wote wadanganyifu. Hamna pakukimbilia Ni kuwa wapolee tuu. Ukihoji Sana utaambiwa umetumwa na mabeberu.
 
Mkuu uki resit index namba haibadiliki hata kidogo inabaki ileile kwa sababu hupewi index mpya ila matokeo ndo yatakayobadikika tu.
Acha kabisa kudanganya watu wewe!hakuna hicho kitu kabisa!unafahamu maana ya index number wewe?Acha uongo kabisa
 
Bado najiuliza ni rushwa ,kujuana au maagizo.
Katika ajira zilizotoka jana za ualimu limetokea jina la Bint Halima Saidi Mohamed na amepangiwa kituo cha kazi mkoa wa Lindi wilaya ya Kilwa katika shule ya msingi Nandembo...

Ukistaajabu ya Halima utashangaa ya Mahera Kupokea Majina ya Covid19 tar 19 kutoka chadema huku Nusrat akiwa ndani na tar 20 Mahela akakanusha kwamba hawajapokea majina.
 
We boya mtahiniwa anakuwa identified na Index number hata ufanye mtihani mara 100.. Sijui kwa nn mnashindwa kujielimisha kabla ya kuropoka
Tatizo udumavu wa akili mkuu, akili ikidumaa reasoning inashuka Sanaa....
 
"Najaribu kuwaza kwa sauti ,huyo muhusika anapoenda kureport kwa mkurugenzi wa halmashauri(sehemu kituo chake cha kazi kilipo ,kiutaratibu anatakiwa aende akiwa na vyeti vyake original kikiwemo cheti chake cha taaluma,,nawaza tu huyu mtu atasubmit nini???? Ukishafikiria kote huku hapa ndo utajua wala hayo sio makosa ,ni planned issue kabisa,,
 
Back
Top Bottom