Tazama kionjo (trailer) cha filamu ya The Royal Tour aliyoshiriki Rais Samia

Kama mambo ndio haya basi Tanzania kama kuna wakati tumepata Rais bora na wa kweli nadhani ni sasa,Tufanye kazi kwa bidii sana,

Hakika huyu Mama ni Mpango wa Mungu,

#WATANZANIA TUFANYE KAZI KWA BIDII
 
"Kwa mwendo huu Tanzania tutafika tunakotaka kwenda tena kwa kuwahi sana, Hongera Mama Samia, Watanzania tuko nyuma yako We chapa kazi achana na Wasio na jema"
 
Hii kazi ni kubwa sana,

WATANZANIA hakika Mama huyu anatupenda sana,

Tuchape kazi kwa bidii
 
 
Hapo mwanzoni naona wameizungumzia Ngorongoro nama wamasai na wanyama wanavyoishi pamoja.

Na bado kuna watu wanapiga kelele waondolewe.

Inasikitisha mno.
 
Tatizo ninaloliona ni hilo jina la filamu hii. Kama mtu ni Mtanzania mwenye asili ya Kiafrika, mtu mweusi, unaishi hapa hapa Magomeni, unazaa mtoto wako wa kiume na unampa jina “Prince William”, basi wengine wataona mwenzetu ni “British” sana na watakusifia kwa uzungu wako. Lakini pia wapo wengine wengi watakuona kituko; mtu usiyejitambua na kujithamini! Kulikuwa na ulazima gani kuiita hiyo filamu “The Royal Tour” wakati wangeweza kuiita jina lingine lolote lenye uzito na heshima ya kujitambua? Mfano: The Presidential Tour”? Jamani, jamani, jamani! Heshima ya ‘Royal’ ina nchi zake na Tanzania hatuko kati ya hizo nchi. Hili wazo la kutoa jina hilo lilipata baraka zote za wakuu wa Wizara, Serikali na Mkuu wa nchi yetu? Hivi kweli hakuna hata mtu mmoja aliona upungufu huo na kushauri inavyopasa? Aibu zingine huko duniani tunajitakia wenyewe.
 
Nia yake ni kuwavutia hao wenye jina hilo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…