Tatizo ninaloliona ni hilo jina la filamu hii. Kama mtu ni Mtanzania mwenye asili ya Kiafrika, mtu mweusi, unaishi hapa hapa Magomeni, unazaa mtoto wako wa kiume na unampa jina “Prince William”, basi wengine wataona mwenzetu ni “British” sana na watakusifia kwa uzungu wako. Lakini pia wapo wengine wengi watakuona kituko; mtu usiyejitambua na kujithamini! Kulikuwa na ulazima gani kuiita hiyo filamu “The Royal Tour” wakati wangeweza kuiita jina lingine lolote lenye uzito na heshima ya kujitambua? Mfano: The Presidential Tour”? Jamani, jamani, jamani! Heshima ya ‘Royal’ ina nchi zake na Tanzania hatuko kati ya hizo nchi. Hili wazo la kutoa jina hilo lilipata baraka zote za wakuu wa Wizara, Serikali na Mkuu wa nchi yetu? Hivi kweli hakuna hata mtu mmoja aliona upungufu huo na kushauri inavyopasa? Aibu zingine huko duniani tunajitakia wenyewe.