Tazama Ramani ndiyo uwe Wimbo wa Taifa, Mungu iwe Sala ya Taifa

Tazama Ramani ndiyo uwe Wimbo wa Taifa, Mungu iwe Sala ya Taifa

Rozela

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2024
Posts
845
Reaction score
2,235
Tazama Ramani umekaa kizalendo zaidi, uwe wimbo wa Taifa haraka iwezekanavyo, Mungu ibariki Africa iwe sala ya Taifa.
=====

1. Tazama ramani utaona nchi nzuri
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2.

2. Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako nikiburudika,
Nakupenda sana hata nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2

3. Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde name nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2
 
Moderator edit Title hapo namaanisha Mungu Ibariki iwe sala ya Taifa.
 
Na Rozela iwe juisi ya taifa haraka sana...

Maana inaongeza damu kwa wingii😋
 
Kuna sehemu kunatajwa karume, umekosea
 
Kuna sehemu kunatajwa karume, umekosea
Kwenye official Song Karume hayupo ingawa miaka ya 2000 kuna waimbaji waliongeza jina lake na wimbo huo unachezwa TBC Taifa na TBC 1 ukiwa na maboresho hayo lakini si rasmi.
 
Tazama Ramani umekaa kizalendo zaidi, uwe wimbo wa Taifa haraka iwezekanavyo, Mungu ibariki Africa iwe sala ya Taifa.
=====

1. Tazama ramani utaona nchi nzuri
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2.

2. Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako nikiburudika,
Nakupenda sana hata nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2

3. Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde name nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2
Kabisa huu wimbo ni Number one na huwa nikiimba unanipa hisia kali sana za utaifa!
 
Ni wimbo mzuri sana (una melody nzuri sana na umejaa maneno yenye hisia na kuimbika) lakini unahitaji maboresho kuufanya uwe wimbo wenye hadhi ya kuwa wimbo wa taifa, hususani kwenye chorus. Chorus imejaa propaganda kwa 100%.
Kwa mfano;
1. kutaja majina ya watu (Nyerere na Karume) tena kwenye Chorus sio sahihi.

2. Maudhui ya wimbo hayaendani kabisa na maudhui ya Chorus. Ni mbingu na ardhi, moto na maji.

3. Maudhui ya utumwa hayana maana yoyote kwa sasa, na yanapelekea kutunga uongo. Utumwa ulikomeshwa na kufutwa kabisa na wazungu wao wenyewe kabla hata ya kuwepo taifa la Tanganyika, tena kabla ya Nyerere au Karume kuzaliwa.


MAPENDEKEZO YANGU.
-Chorus iboreshwe kwa kuondoa majina ya watu na maudhui ya Chorus yabadilike kuendana na wimbo.
-Ufanywe kuwa wimbo rasmi mashuhuri wa kuimbwa na kushangiliwa na watanzania wote popote katika matukio yoyote rasmi na yasiyo rasmi.
 
Huo wimbo na ule wimbo wa 🎶Tanzania yetu ni nchi ya furaha🎶 una mvuto wa kihisia balaa.

Ikitokea upigwe kama surprise mahali huko ughaibuni halafu wewe uwe umekaa kitambo hajafika Tz, yaani uwe umeimiss fulani Tz unaweza ukajikuta mpaka machozi yanakutoka
 
Kwenye official Song Karume hayupo ingawa miaka ya 2000 kuna waimbaji waliongeza jina lake na wimbo huo unachezwa TBC Taifa na TBC 1 ukiwa na maboresho hayo lakini si rasmi.
Thank you, ndio maana kila source naona karume hayupo kumbe ndo hivyo.
 
Haufai kabisa, wimbo umekaa kama wa kuombeleza japo una hisia sana. Wimbo wa taifa umekaa kiukakamavu, kiuzalendo Sanaa, halafu ni rahisi kukaa kichwani, ni rahisi kuukariri na umepangika vizuri sana.
 
Haufai kabisa, wimbo umekaa kama wa kuombeleza japo una hisia sana. Wimbo wa taifa umekaa kiukakamavu, kiuzalendo Sanaa, halafu ni rahisi kukaa kichwani, ni rahisi kuukariri na umepangika vizuri sana.
Ile ni Sala, wimbo wenye hisia za kizalendo ni huu.
 
Tazama Ramani umekaa kizalendo zaidi, uwe wimbo wa Taifa haraka iwezekanavyo, Mungu ibariki Africa iwe sala ya Taifa.
=====

1. Tazama ramani utaona nchi nzuri
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2.

2. Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako nikiburudika,
Nakupenda sana hata nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2

3. Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde name nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2
Huu wimbo unahisia sana ukiimba tofauti na Huu wa Sasa wa Taifa.Sema mwimbo wa Taifa haupendezi kuwa Mrefuuu
 
Back
Top Bottom