Pre GE2025 Tazama Video Watu wamiminika na kufurika kwa Rais Samia mpaka Aamua kujipiga picha kwa furaha

Pre GE2025 Tazama Video Watu wamiminika na kufurika kwa Rais Samia mpaka Aamua kujipiga picha kwa furaha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii haijawahi kutokea popote pale Barani Afrika kwa Kiongozi kupendwa kiasi hiki mpaka watu wanaishia nguvu za kusimama kutokana na kuzidiwa na furaha na upendo kwa Rais Samia. Kwa hakika Rais Samia ni chaguo la Mungu Mwenyewe.huyu siyo mtu wa kawaida.katika jicho la kiroho inaonyesha namna Mungu alivyo pamoja na Rais Samia.
Uchawa first class
 
Najiuliza kama watanzania wa 2024 wapo na uzuzu hivi ... Je wa 1961 walikuwaje? tuna safari ndefu sana
Basi kwa taarifa yako hiko kizazi cha miaka ya 60 mwisho 80 kilikua kizazi jeuri kweli kweli huwaambii kitu, Nyerere alinusurika kupinduliwa mara mbili
Na bado kwenye mikutano watu walikua wanakuja kubishana
 
Walikubali vp Nyerere kutawala kiimla na kuacha ombwe hili la CCM mpaka leo? Ikiwa unasema walikuwa Wabishi?! Wale ndio wamezalisha hichi kizazi Ovyo cha leo.
 
Mkuu wale walijitambua sana, kwanza walipata elimu ya kikoloni iliyokuwa na viwango, huyu wetu sijui amesoma wapi ila haiwezi kuwa Tukuyu
Kwa taarifa yako kizazi kile ndio kimezaa kizazi hiki. Kama wangejitambua wale tusingefika hapa leo.
 
Mimi Sitafuti uteuzi ndugu yangu.mimi ni Mzalendo naye fanya kazi kwa kujitolea na kwa hiyari kabisa
Tanabaisha kazi yako sasa,maana unaleta mambo ya CHAMA tu,sema wewe umejiajiri au umeajiriwa kufanya kipi,watu wakujue pale LUMUMBA au DODOMA makao makuu.
 
Comment yako imenitoa machozi ya furaha😂😂😂😂.

Ila mimi nakukubali sana. Nikiingia kwenye siasa nitafanya juu chini uwe mpambe wangu.
Chawa si mpambe.Mpambe lazima awe na akili huyu hana akili kabisa sijui anavukaje barabara.
 
Alianza kuweka namba ya simu, sasa hivi anaweka majina yake matatu yote, soon tutarajie namba yake ya NIDA ila jamaa wamemfungia vioo kama hawamuoni.

Wakiendelea kumpuuza atafungua ID mpya aje kuwatukana humu kama hajafungua bado.
Huenda anayo kuna mwingine amefungua uzi sijui ni pacha wake
👇
 
Comment yako imenitoa machozi ya furaha😂😂😂😂.

Ila mimi nakukubali sana. Nikiingia kwenye siasa nitafanya juu chini uwe mpambe wangu.
 
Alianza kuweka namba ya simu, sasa hivi anaweka majina yake matatu yote, soon tutarajie namba yake ya NIDA ila jamaa wamemfungia vioo kama hawamuoni.

Wakiendelea kumpuuza atafungua ID mpya aje kuwatukana humu kama hajafungua bado.
Ww umejuaje kama wamemfungia vioo, kwasababu hajateuliwa au?
 
Inafurahisha sana.....watu Wana mahaba na Mama Samia.
Nchi imetulia,furaha ipo kwa wananchi..mioyo imejaa matumaini.
 
kuna watu wamama wa sisiemu wameunda mavikundi ya chawa wanataka wam recruit na wife et jmos kuna safar ya dodoma usafari kwenda na kurud bure ili kumuhadaa bimkubwa kwamba ni kipenz cha watu kumbe watu wanapewa posho kwenda kumshangilia hatendewi haki kabisa amir jesh mkuu wetu
 
Back
Top Bottom