Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Kumbe treni ya Tazara bado ipo! Treni hii inaendeshwa na vilaza wabobezi.View attachment 3657307Kutokana na changamoto za kiutendaji zinazotokana na kufungwa kwa muda kwa njia mbili za reli katika sehemu ya Kapwila-Msanza nchini Zambia na sehemu ya Mwakanga-Mzenga nchini Tanzania, mabadiliko yafuatayo ya muda katika uendeshaji wa treni za abiria yatatumika:
View attachment 3657309
TAARIFA KWA UMMA
MABADILIKO YA MUDA KATIKA UENDESHAJI WA TRENI ZA ABIRIA 26 AGOSTI 2026
1. Treni ya Abiria ya Kuvuka Mpaka ya Mukuba
Treni ya Mukuba ambayo kwa sasa inaelekea Kapiri Mposhi Mpya:
Itaondoka New Kapiri Mposhi kwenda Nakonde saa 12:00 jioni leo, Jumatano, 26 Agosti 2026;
Itafanya huduma ya ndani kati ya Kapiri Mposhi Mpya na Nakonde, na kurejea kutoka Nakonde kwenda Kapiri Mposhi Jumamosi, 29 Agosti 2026; na
Baada ya hapo itabaki Kapiri Mposhi Mpya ikisubiri safari yake inayofuata iliyopangwa Jumanne, 1 Septemba 2026, ambapo huduma za kawaida za Treni ya Abiria ya Kuvuka Mpaka ya Mukuba kwenda Dar es Salaam zinatarajiwa kuanza tena.
2. Treni ya Abiria ya Udzungwa
X Safari ya Treni ya Udzungwa iliyopangwa kuondoka Mlimba leo, Jumatano, 26 Agosti 2026, imeghairiwa.
Huduma itaanza tena Jumamosi, 29 Agosti 2026, ikifanya safari kutoka Mlimba hadi Makambako kwa mujibu wa ratiba yake ya kawaida.
Tunajutia kwa dhati usumbufu uliosababishwa na hitilafu hizi za kiutendaji na tunawashukuru abiria wetu wapendwa kwa uvumilivu, uelewa na kuendelea kutuunga mkono.
Imetolewa na Uongozi
26 Agosti 2026
Pia soma ~ TAZARA boresheni huduma zenu! Kama mnasitisha safari toeni taarifa mapema, mnakwaza sana
Hapana mkuu, wale vilaza wabobevu walishashindwa wakamuuzia mchina.Kumbe treni ya Tazara bado ipo! Treni hii inaendeshwa na vilaza wabobezi.
Hii treni inalipa sana! Ina abiria wengi na mizigo mingi ya kusafirisha (kwa upande wa Tanzania)! Kipengele kipo kwa upande wa Zambia! Usimamizi umekuwa ni mbovu kupitiliza! Wafanyakazi na hasa Ma-TT kwa miaka mingi walikuwa wanakusanya hela kwa manufaa yao kupitia tiketi zao binafsi! Hao Wazambia muda wote ukiwakuta kwenye treni wamelewa! Wao ni kupenda bata tu!Hapana mkuu, wale vilaza wabobevu walishashindwa wakamuuzia mchina.
Naona mchina anafanya marekebisho makubwa, pia ni utaratibu mzuri kutoa taarifa mapema ili abiria wajipange tofauti na wale vilaza walioamua kuirudisha kwa aliyeijenga.
Yes! Mkuu unachosema ni sahihi. Nipo upande wa Zambia kwasasa. Hawa ndugu zetu wanafeli sana hasa kwenye mapambano ya kuinua uchumi wao.Hii treni inalipa sana! Ina abiria wengi na mizigo mingi ya kusafirisha (kwa upande wa Tanzania)! Kipengele kipo kwa upande wa Zambia! Usimamizi umekuwa ni mbovu kupitiliza! Wafanyakazi na hasa Ma-TT kwa miaka mingi walikuwa wanakusanya hela kwa manufaa yao kupitia tiketi zao binafsi! Hao Wazambia muda wote ukiwakuta kwenye treni wamelewa! Wao ni kupenda bata tu!
Usimamizi ulikuwa ni mbovu na wa kutegeana! Kiukweli ngozi nyeusi haina maana hata kidogo! Utashangaa baada ya kubinafsishwa, watu walewale watafanya kazi kwa bidii kwa sababu tu wanasimamiwa na Wachina (ngozi nyeupe)!!!
Soma tarehe iliyotolewa taarifa na tarehe ya matukio, vyote ni tarehe 26/08! Sijui hiyo mapema ipo wapi.Hapana mkuu, wale vilaza wabobevu walishashindwa wakamuuzia mchina.
Naona mchina anafanya marekebisho makubwa, pia ni utaratibu mzuri kutoa taarifa mapema ili abiria wajipange tofauti na wale vilaza walioamua kuirudisha kwa aliyeijenga.
Mkuu kama pamoja na kubinafshishwa Bado mambo ni yaleyale bhasi tukubali kwamba waafrika tunashida kwenye ubongo wetu, maana itamlazimu mchina alete wachina kwaajili ya shughuli za uendeshaji. Sasa sijui tutalilia ajira au tutalia kwamba tunatawaliwa tena.Soma tarehe iliyotolewa taarifa na tarehe ya matukio, vyote ni tarehe 26/08! Sijui hiyo mapema ipo wapi.
Mwezi wa sita jirani yangu alisafiri kwa treni toka Dar saa 10 jioni walilala njiani baada ya baadhi ya mabehewa kukatika jambo ambalo si la kawaida, walitegemea mafundi wangefika asubuhi ila la! Hawakuja mpaka jioni, walishinda na njaa na ndani ya treni hamna maji ila kuna mapipa ya maji vyooni! Tazara hii siyo ya miaka ya 80.
Cape gauge hiyo haijafika standard gaugeHivi TAZARA ni SGR?