Sijaandika kuwa umekataa kwamba huyo hana mzazi.
Nami pia nakatataa mtu wa miaka 60 kuwa na mzazi binti wa miaka 5.
Hata nami sikatai kwamba ulimwengu una mwanzo.
Wewe unakataa kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ndiye chanzo cha ulimwengu. Na hiyo ndiyo tofauti yetu kubwa.
Umetumia mfano wa mtoto binti wa miaka 5 kwamba hawezi kuwa mama wa mwanaume wa miaka 60 ili kuhalalisha kuwa Mungu sio
chanzo cha ulimwengu. Sijui kama unamaanisha kuwa Mungu ni sawa mtoto binti wa miaka 5, na ulimwengu sawa na mwanaume wa miaka 60! Hata hivyo siamini kabisa kama Mungu ni mdogo wa umri kuliko ulimwengu.
Hiyo ndiyo sababu halisi inayokuaminisha kuwa Mungu sio chanzo cha ulimwengu, na unaamini pia kuwa hiyo ndiyo sababu ya kutofautiana kimantiki na utata wa asili.
Mfano wako wa mtoto binti wa miaka 5, kuzaa mwanaume wa miaka 60, una mfumo wa sayansi ya kibaolojia. Katika mfumo wa kibaolojia, mzazi ni lazima awe na umri mkubwa na sio vinginevyo.
Tofauti na mfumo wa kibaolojia, pia kuna mfumo wa sayansi ya kiufundi. Mfumo wa kiufundi unahitaji ukubwa wa maarifa na uwezo ili kutengeneza kitu kikubwa kwa kipimo hata kuliko fundi mwenyewe. Huo ndiyo mfumo wa uumbaji. Mungu alitumia mfumo wa kiufundi kutengeneza ulimwengu.
Kwa kuzingatia mifumo hiyo miwili, mfano wako hauna uwiano na uumbaji wa ulimwengu. Mtaji wa mfano wako ni umri, na mtaji sayansi ya kiufundi uwezo na maarifa.
Kama vile hoja ya mtoto wa miaka 5 kuwa mama mzazi wa mwanamme wa miaka 60 ilivyo na contradiction, kwamba mama mzazi wa mwanamme wa miaka 60 ni lazima awe mkubwa kuliko huyo mwanamme, ndivyo hoja ya kuwapo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ambaye kaumba ulimwengu wenye kuweza kuwa na mabaya, licha ya kuweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani ilivyo na contradiction.
Contradiction hii pande zote mbili, kwa mtoto wa miaka 5 ambaye pia ni mama mzazi wa mwanamme wa miaka 60, na kwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ambaye kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea, inaonesha habari hizi ni dhana tupu, hazipo katika ukweli.
Na zaidi, uwepo wa ulimwengu unaoruhusu mabaya kutokea ni mutually exclusive na uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.
Hivyo.
1. Inawezekana awepo Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, bila ya kuwepo ulimwengu unaoruhusu mabaya kutendeka.
2. Inawezekana ukawepo ulimwengu unaoruhusu mabaya kuwepo, bila ya kuwepo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.
3. Haiwezekani viwili hivi, Mungu huyo mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote na ulimwengu huo unaoruhusu mabaya, vyote kuwepo.
4. Kwa uzoefu wetu wa maisha, tunaona ulimwengu unaoruhusu mabaya upo. Ni huu tunaoishi ndani yake kika siku.
5. Hivyo, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.