Unaweza kuuthibitisha huo mfumo uliokufanya uwepo bila Mungu kuhusika?
Naweza kuthibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hahusiki kwenye uwepo wangu hapa bila hata kuthibitisha huo mfumo ulionifanya niwepo ni upi.
Naweza kujua kwamba Washington DC, USA si mji mkuu wa Chad, Central Africa, bila hata kujua mji mkuu wa Chad, Central Africa, ni mji gani.
Kama ninavyoweza kuthibitisha kwamba, mwanamme mwenye miaka 60 leo hawezi kuwa na mama mzazi binti mwenye miaka 5 leo.
Yani nakuambia hivi.
Ukiniwekea baba ana miaka 60 leo hapa, ukaniwekea na binti mdogo ana miaka 5 leo hapa.
Ukasema kwamba, huyu binti mwenye miaka 5 leo, ndiye mama mzazi aliyemzaa huyu baba mwenye miaka 60, naweza kukukatalia kwamba huyu binti wa miaka 5 leo, hawezi kuwa mama mzazi wa huyu baba wa miaka 60 leo.
Kwa sababu huyu baba kazaliwa miaka 60 iliyopita, huyu binti kazaliwa miaka 5 iliyopita.
Wakati huyu baba anazaliwa, huyu binti alikuwa hajazaliwa bado, alizaliwa miaka 55 baadaye.
Na hapo, hata kama simjui mama halisi wa huyu Baba wa miaka 60, nitajua tu kwamba huyu binti wa miaka 5 si mama mzazi wa huyu baba wa miaka 60.
Unachofanya hapa, ni sawa na kuniletea binti wa miaka 5 na Baba wa miaka 60.
Unasema huyu binti wa miaka 5 ndiye mama mzazi wa huyu Baba wa miaka 60.
Nakwambia hilo haliwezekani, kimantiki haiwezekani binti wa miaka 5 leo awe mama mzazi wa Baba wa miaka 60 leo.
Unaniuliza swali.
Kama huyu binti si mama mzazi wa huyu Baba, huyu Baba mama yake mzazi ni nani?
Sihitaji kujua mama mzazi wa huyu Baba wa miaka 60 ili kujua kwamba binti wa miaka 5 hawezi kuwa mama mzazi wa Baba wa miaka 60.
Kwa sababu binti wa miaka 5 kuwa mama mzazi wa Baba wa miak 60 ni contradiction.
Sihitaji kujua kilichoniweka hapa ni nini ili kujua kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hahusiki katika mchakato wa kuniweka hapa.
Kwa sababu uwepo wa Mungu huyo pamoja na dunia ambayo inaruhusu mabaya ni contradiction sawasawa na binti wa miaka 5 leo kuwa mama mazazi wa kumzaa Baba aliye na miaka 60 leo