Ni vigumu sana kuamini Binadamu na uhai kwa ujumla ulizuka tu kutoka michakato asilia ya kifizikia na kikemikali, hapo ndipo Mungu anapoingia kwenye picha.
Mkuu.
Naona kama unataka kujenga hoja ya msingi.
Hebu tuichambue hoja yako.
Umefanya kitu kinaitwa "logical non sequitur".
Logical non sequitur ni kosa la kimantiki la kuunganisha mambo mawili ambayo hayana muungano wowote, kimakosa.
Ni sawa na mtu asema.
1. Rais wa Tanzania ni mwanamke kutoka Zanzibar. (sawa kabisa)
2. Fatma Karume ni mwanamke kutoka Zanzibar (sawa kabisa)
Sasa sikiliza logical non sequitur inapoingia hapa,
3. Kwa kuwa rais wa Tanzania ni mwanamke kutoka Zanzibar, na Fatma Karume ni mwanamke kutoka Zanzibar, basi lazima Fatma Karume ni Rais wa Tanzania.
Yani umeunganisha mambo mawili ambayo hayana muungano.
Hebu turudi kwenye hoja yako.
Unasema kwamba "Ni vigumu sana kuamini kwamba Binadamu na uhai kwa ujumla ulizuka tu kutoka michakato asilia ya fikzikia na kikemikali..."
Kwanza kabisa, I am not interested na habari za "kuamini". Twende tutafute kujua, ama tunajua ama hatujui.Tusipojua tutafute kujua, si kuamini.
Pili, ni vigumu au haiwezekani? Hayo ni mambo tofauti. Ni vigumu mtu kupigwa na radi, siku ya harusi, lakini kuna mtu kapigwa na radi siku ya harusi!
Zaidi, hata kama uhai haujazuka tu kwa michakato ya kiasili ya kemia na fizikia, hilo halimaanishi kuwa uhai umeletwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote. Kuna mengi sana hatuyajui, kwa nini unakimbilia kusema habari za Mungu? Ushahidi wako uko wapi?
Mbona huyo Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote akiwekwa kwenye mizani midogo tu ya kimantiki, kama ya "the problem of evil" anaonekana hawezekani kuwepo?