Una maana kama mabaya yote ya dunia uliyotaja yasingekuwapo ungekiri kwamba Mungu yupo?
Je wewe unaweza kuthitisha kuwa Mungu hayupo?
Ulimwengu ambao una mabaya unathibitisha Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote hayupo.
Ulimwengu usio na mabaya unaweza kuwa kiashiria cha kuwepo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, lakini hauthibitishi Mungu bado kuwa Mungu huyo yupo.
Ni kama tuseme tumehakikisha Kiranga leo kavaa shati jekundu.
Tukiweka picha za watu zilizopigwa leo, halafu hakuna mtu aliyevaa shati jekundu, tutajua Kiranga hayupo.
Na tukiweka picha za watu, na kuna watu wamevaa mashati mekundu, hayo mashati mekundu yqnaashiria kwamba inawezekana Kiranga akawa mmoja wa hao waliovaa mashati mekundu.
Lakini hilo pia halithibitishi mtu yeyote aliyevaa shati jekundu ni Kiranga.
Kwa sababu anaweza kuwepo mshabiki wa Simba tu kavaa shati jekundu, wala si Kiranga.
Kwa mara nyingine tena, uwepo wa ulimwengu huu unaoweza kuwa na mabaya ni uthibitisho Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote hayupo.
Ulimwengu huu uko mutually exclusive na huyo Mungu.
Maananyake, ulimwengu huu ukiweza kuwepo, Mungu huyo hayupo.
Mungu huyo akiwepo, ulimwengu huu hauwezi kuwepo.
Ulimwengu huu upo.
Hivyo Mungu huyo hayupo.
Je, wewe unaweza kuthibitisha Mungu huyo yupo?