TB Joshua “Ntaomba nikiwa milimani sitakula hadi adui yetu Corona aondoke”

TB Joshua “Ntaomba nikiwa milimani sitakula hadi adui yetu Corona aondoke”

kwa nini amuamini mtu anaweza kaa zaidi ya siku 20 bila kula chochote na asife?.
basi mnatakiwa kuamini inawezekana na ishawai tokea mara kadhaa,

viongozi wa dini wanatakiwa waumizwe na corona kama huyu tb joshua,corona ina kuuma mpaka unaamua kujitenga kufanya maombi mwanzo mwisho.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchungaji maarufu duniani anayetokea katika taifa la Nigeria TEMITOPE BALOGUN JOSHUA alimaarufu kama TB JOSHUA ameamua kufunga na kupanda milimani kwa ajili ya maombi maalumu kuombe janga la Corona.
View attachment 1434414
Duk9kpTURBXy85MWI5MGY5NTk0MmRjZTViYjRmNjFjMDg5NGVkNmUwYi5wbmeRkwXNAxTNAbyBoTAB.jpg


Kupitia ukurasa wake wa Twitter Mchungaji huyo ameamua kwenda kukaa milimani akiomba huku akidai kwamba hatashuka wala hata kula chochote mpaka pale janga hili la Corona litakapoondoka. “SITAKULA CHOCHOTE MPAKA PALE ADUI ATAKAPOONDOKA”
Ha ha ha haa korona itafichua manabii wa uongo wote ambao mpaka leo hawatibu cancer wala HIV wala kwenda hospitali kutibu wagonjwa wa kweli. Atakufa na njaa huyo kama ni kweli hakuna hata mtu mmoja anaye mpelekea chakula.
 
Unajua jambo hili ni gumu kulifanya kama hauko vizuri kiroho,lakini kama una uhakika mahusiano yako na Mungu yako vizuri,huwezi kuogopa wala kuwa na mashaka kwa yatakayokupata kwa kufanya maombi ya aina hiyo.Ukumbuke sio kufunga tu ni kufunga na kuwa kwenye maombi constantly,kwahiyo hata kama utakufa ukiwa katika kuiombea dunia na watu wake bado utakuwa umefia kwenye mikono salama ya Mungu,na kumbuka kuwa kinachokufa ni mwili na sio roho kwahiyo hana haja ya kuogopa hata kama atakufa,amejitoa kwa ajili yake na watu wengine,kwahiyo kifo chake hakitakuwa sawa na wewe utakaefia ukiwa Bar......
 
Ameenda kuomba huko mlimani akiwa na mpiga picha pamoja na kuzipost twitter. Mpaka hii CORONA kuisha tutaona na kusikia mengi.
As far as I know hizi picha ni kutoka maktaba, ni za wakati ule ndio anapokea WITO. Kuhakikisha hilo, angalia size ya mwili wake na sasa hvi, utagundua hapa alikua mwembamba sana wakati sasa hivi ni mnene kiasi fulani.
 
Si angeomba kimya kimya kwani Mungu asingesikia?

Hata hivyo Mungu ni mkubwa wenzetu wasioamini hizo shortcut wanakesha maabara kutupatia chanjo na tiba ya corona.
 
Mchungaji maarufu duniani anayetokea katika taifa la Nigeria TEMITOPE BALOGUN JOSHUA alimaarufu kama TB JOSHUA ameamua kufunga na kupanda milimani kwa ajili ya maombi maalumu kuombe janga la Corona.
View attachment 1434414
Duk9kpTURBXy85MWI5MGY5NTk0MmRjZTViYjRmNjFjMDg5NGVkNmUwYi5wbmeRkwXNAxTNAbyBoTAB.jpg


Kupitia ukurasa wake wa Twitter Mchungaji huyo ameamua kwenda kukaa milimani akiomba huku akidai kwamba hatashuka wala hata kula chochote mpaka pale janga hili la Corona litakapoondoka. “SITAKULA CHOCHOTE MPAKA PALE ADUI ATAKAPOONDOKA”
Amebeba na chaja?

Jr[emoji769]
 
Kama alishindwa kuutabiri ndio ataweza kuuombea utokomee?

Jr[emoji769]
MT. 6:5 SUV
 
TB Joshua kamuiga JIWE maana JIWE alilala juu ya mawe kule Chamwino
 
huwezi kujua majibu ya hii kitu yatapitia wapi? yawezekana kwa wanasayansi ama kwa imani ....

Mussa aliwaokoa wana wa Islael kwa Imani ...Sasa kubeza si kuzuri - kama unaamini COVID -19 inaweza kuisha kwa kuvaa Barakoa, Kuosha mikono na kujifungia ndani - well and good my Friend.

Wakati wa vita kila mmoja kwa karma yake, mwanasayansi haya, na mtu wa maombi haya - whatever is going to work fine...tunaopona ni sisi wanadamu wote.
Ukweli ni kwamba huyu amejitenga anajirinda na hatari ya korona
ndiyo maana akadai hatorudi mpaka korona iishe
huyo wala hatoishi hapo kwa muda wote huo
atakaa karantni sehemu
hapo ni pa kuja kupigia picha tu za
kuwaaminisha na kuwalubuni wafuasi wake
kuamini kwamba yeye anaweza kushinda na njaa kwa muda wote
mpaka corona
hy itakua si akiri ya kawaida
bali itakua akili ya kushikiziwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
. 6:5-15

MT. 6:5-15 SUV

Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.] Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.



Jr[emoji769]
 
Jaman 2cpende kukosoa uamuzi wa wa2 wa mungu
Jose bhana... Watu wa Mungu ni wewe mwenyewe na Bible yako ikitanguliwa na matendo yako!

Kuna wengine hadi wanatuambia ukitoa sadaka hupati coronavirus halafu hujashituka tu jomba!!

Anyway, I don't judge you if you have all your faiths in these people but if it where me, I'd invest my faith in the Bible than to these Spiritual Entrepreneurs!!
 
wenzie walivaa magome ya miti,hawakwenda na godoro

na walifunga kweli
 
Back
Top Bottom