TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

Nimesoma commengts za watu wengi humu ndani hawaangalii TBC na kuanza kujiropokea tu. Kwa aarifa yako waambieni vijana wenzenu wanaotafuta fursa sasa TV yao iwe TBC wasikae kumuangalkia Dimind na wendinea wasika lie Ndombolo badala ya kutafuta fursa. TBC imeanza kuboreka saaana! Hivyo toeni constructive critisimm. Angalau MDAY huyu ametoa na suggestion.
 
Vipindi vyao vingi havina mvuto kwa mtazamaji, wao kazi kusifia tuu, yaani mtu anasifiwa mpaka unaamua kuzima tv
Tanzania tuna matatizo mengi mno, lakini kwenye taarifa ya habari huoni wakiripoti, wao kusifia tuu mmekua kama nyamwazi aisee mnatia hasira sana
 
naomba TBC mzingatie kuweka majina ya watu mnaowahoji kwenye Taarifa zenu mnazoturushia.

Unakuta mnachukua taarifa Fulani halafu mnayemhoji/mnaowahoji hamuweki majina wala tittle zao kama wafanyavyo ITV.

Hili linatukera sana sisi wafuatiliaji wa TBC.

Kama sijaeleweka, niambieni hamjaelewa wapi nifafanue zaidi.

Ni kero mno hii
 
Katika televisheni yenye kuboa ni yenu! Mnakumbusha TV za kichina enzi za Mao the tung!. Mnasifia tu hamuoneshi changamoto nyingine za upande wa pili. Mfano Hivi hiyo TBC ni ya chama tawala?. Je mkionesha Sera za vyama vingine mtaugua? Acheni ushamba wa karne ya 47! Hata Nyerere alipinga wazo la kumsifia kizushi nyie sijui mmepata Wapi Hii tabia. Kifupi hamfai kwa kuwa hamvutii
 
Tbc mnaegemea mlengo fulani ndio maana watu wanalalamika mimi tangu chanel zimekatwa na kubakia tbc nimehamia Dstv kwa ajili ya michezo pekee kwaherini nitarejea yatakapo fanyika marekebisho makubwa
 
Kwa habari za Kimataifa wana download za aljazeer, CNN nk sasa sijui kama wataweza kutenganisha
 
bado hawawez kubalance Sauti ... PIA mtangazaji anasema Tupate taarifa Kamili, wanabak wameganda km Dakika nzima... Hakuna ubora kabisa. Km mitambo feki wekeni mipya ...mmezubaa Sana had huruma
 
Em subiri kwanza. Hivi hii TV station bado ipo?
 
Mnaegemea kwenye chama cha jiwe
Mnaacha vyama Vingine
Hiyo ni double standard
 
Kila ukiwasha tv unakutana neno safari ya dodoma hiyo tbc siangalii mimi siielewi,chaneli inasifia vitu vya ajabu ajabu habar yenyewe haina mvuto
 
Hivi ninaweza kuiangalia wapi taarifa za habari zilizopita kwa mfano ya jana tarehe 11/11/2018?
 
hiyo channel inapatikana wapi, kwenye king'muzi changu DSTV&AZAM HAMNA KABISA.
Lakini ni bora tu niendelee kutazama UBC
 
Tbc iwe general coverage ya marika yote wekeni vipindi vya burudani sana kwa maana wafuatiliaji wengi ni vijana
 
Siku mkiaza kutangaza habari zenu kama TV ya taifa na si kama ya 'sisiemu', nishtueni.
Mlipoamua kutoa station zingine kwenye DSTV ndo ilikua mara yangu ya mwisho kuitizama TBC. Infact nilikua naangalia TBC zinapoanza habari za kimataifa hadi kwenye michezo tu. So, sijui nini kinaendelea TBC sku hizi. Rudisheni station zingine za local kwenye ving'amuzi vyetu pendwa tafadhalini sana.
 
TBC ni uchafu.....cha msingi ijitenge na serikali ya CCM ijiendeshe hasa kwa kutokuingiliwa...

TBC mnatakiwa kumrudisha Tido Mhando..

Msipomrudisha mtafeli kila siku!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…