TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

Tbc mje mjibu hoja za watu huku, au mnatusumbua kushauri afu mnatuchora tu
 
TV imejaa ma mama hayana mvuto, picha mbaya yan bora niishie hapa
 
Nawaangalia watu wanavyojisumbua kuishauri tbc
 
Kila ukiwasha tv unakutana neno safari ya dodoma hiyo tbc siangalii mimi siielewi,chaneli inasifia vitu vya ajabu ajabu habar yenyewe haina mvuto
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ eti safari ya Dodoma
 
Hivi zaidi ya kumwagia SIFA Magufuli hii Tv ina nini cha zaidi?
 
[emoji23][emoji23]ndio hivyo nakushauri washa tv yako ndio matangazo yatakayokuchosha sana
mi mwenyewe nna kisimbuzi cha Azam ndo balaaaa yani,,hakuna channel hata moja yenye taarifa ya habar nzuri,,,nakomaa na channel za kihindi dadekii
 
mi mwenyewe nna kisimbuzi cha Azam ndo balaaaa yani,,hakuna channel hata moja yenye taarifa ya habar nzuri,,,nakomaa na channel za kihindi dadekii
[emoji23][emoji23]pole sana upo unakomaa na sultan umekaribia kupajua mumbai kupitia channel za kihind
 
Kumbe upo? Zile nyuzi zako bana enzi zile
 
Inaegemea sana upande mmoja bila kuangalia upande wa 2 ni kumsifu saana mtu flani bila kutoa kamwe ubaya wake hauonyeshiewi pia . Hakuna mtu ambaye ni mzuri 100
 
nashauri tbc wajifunze wezao wa chaneli za za asia, kama vile nhk world, ama arirang, wana vipindi vyenye ubora wa hali ya juu sana, hata kama kipindi ni cha siasa , uandaaji wake unafanya hata wewe usiyekuwa raia wa huko asia upende kuangalia, kazi sasa hapa kwetu,
ubunifu wa toka miaka ya 90 kwenye uandaaji wa vipindi ndio huohuo unaotumika hadi leo, hivi tbc haiajili wasomi waliosomea masuala ya media, mbona ubunifu ni zero shubamiti z**u nyie
 
TBC 1,turushieni LIVE mechi ya Taifa Stars vs Lesotho. Huu mtanange ni muhimu kwa kila Mtanzania na ni tukio la kitaifa pia. Tuunganisheni na vijana wetu jamani
 
Hongera sana Dokta Ryoba kwa nia ya dhati ya kuisuka upya TBC. Maoni yangu ni haya kaka 1. Iongezwe chaneli ya burudani na michezo ili kuonesha Sana'a, miziki na maigizo ,2. TBC1 iwe na kipindi cha kueleza kero moja kwa moja kwa viongozi. Mfano, k jumapili anaalikwa kiongozi studio na kupokea simu moja kwa moja toka kwa wananchi, 3. Pawe na kipindi cha matukio ya wiki toka kila mkoa, 4. TBC irushe mechi zote za timu ya Taifa, icheze ndani au nje, mwisho vyama vingine pia vipewe fursa kutumia TBC
 
Acha kuzunguka, asiifanye tbc kuwa kituo cha propaganda za ccm
 
Safi sana. Bonge la ushauri. Kwa kweli watangazaji wao wa kike wamezubaa na vipindi ni vya kizee plus muonekano wa vipindi vyao ni mbaya.
Jamani uzee sio tatizo, Yupo Richard Quest kule CNN anafanya vizuri sana, na wengine wengi watu wazima wapo kule Aljazeera, huwezi kuchoka kuwatazama vipaindi vyao, pia kunenepa sio kosa, Yupo Sara Kipingu pale ITV nae anafanya vizuri tu, Tatizo kuu la TBC ni kujibandika UCCm, naichukia sana kwa hili, na naamini ndilo chuizo la watu wengi, sitegemei kuipenda hata ikibaki peke yake kama wanavyotaka, hii ni television ya taifa inaendeshwa kwa kodi zetu, halafu inakalia kufanya porojo za ccm na policcm,
Inawezekana hiyo rangi ikawa nzuri kama watafanya Haki na Usawa tukamuona pale Mbowe au Halima Mdee akijimwaga akiwahuru, sio kila jambo wakitaka kufanya mpaka wamuulize Jiwe, Ni malofa sana hawa Tbc wanashindwa kuonesha Bunge Live halafu wanaweka mamiziki ya hovyohovyo kule Tbc2, hili nalo ni janga tulipige vita, unawekaje matangazo ya ccm katikati ya taarifa ya habari ?, Utasikia mafanikio ya magufuri, mtu unaweza kuivunja screen bure, sisi wengine tuna hasira sana
 
Angekuwa Rioba yule wa gazeti la RAI original angekusikia, mimi tuwaache wafanye wanavyotaka kwani haitusaidii lolote kuwashauri, watajua wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…