TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

Ukweli kwenye orodha ya channel ya kisimbuzi changu TBC niliifuta kabisa. Ni TV ya serikali lakin wanarusha habari za Mlango flani hivi.

Pia sahizi wana safari channel toka ianzishwe wanarudia vipindi vile as if wameweka mkanda Wa VHS, kama lengo ni kutangaza utalii basi kuweni wabunifu. Nashindwa kuelewa vijana wanafanya nini pale zaidi ya kutangaza Mpira.

Jifunzeni, elimikeni, badilikeni muendane na wakati. Onesheni ukongwe wenu sio mbaya mkajifunze AZAM MEDIA Kwa Tido
 
Mi napmba nijue, Ni lini mtaboresha mitambo yenu kwa wneo la kilolo milima ya udzungwa; ngangange, bomalangombe, masisiwe, udegenda na vijiji vingie ili tuwapate vizuri km mnavyojinadi kuwa niliondokewa ninyi ni bora!?
Umesahau idete, mbawe, mwatasi,masige,kibengu,mapanda
 
Mimi TBC kwangu ndiyo bora kabisa kwani vipindi vya elimu navipata kwa ubora kabisaa
 
Toa changamoto wafanyaje ili waboreshe sio kulalamika tuu,hivi wakati wa tido kipi kikubwa kilikuwepo haswa manake mie sikukiona hasa sema wewe

Utakua kipofu na kilaza kama hukuona mabadiliko ya TBC
 
Tbc..acee naja Happ field next month. Tv programmer. Tv producer
Bila shaka naja na nondo mpya
 
 
Wakuu,

Napokea maoni mengi sana huko PM. Nakutana na kila aina ya maswali na jumbe za shauku ambazo watu wanahitaji kufanya kitu for TBC1.

Nasikitika kwamba nashindwa kuzijibu zote na kusemea chochote kwa sababu mimi sio mwajiriwa na wala sina mahusiano yoyote ya kikazi na TBC.

Niombe wote ambao mna maoni, ushauri, mapendekezo au mahitaji muyaweke hapa inatosha. Kwa bahati mbaya, huko PM sitoweza kusaidia chochote.

Miongoni mwa mawazo mazuri niliyopokea ni haya:

 
TBC ya Mhando ilikuwa bora kuliko tv station zoote tz
Kwa kweli TBC mh, wiki iliopita tulilamika kuhusu mtangazajia wao wa habari za biashara Stanley, sasa hivi wamemtoa simuon tena, Habari za biashara zinasomwa direct, hatukumaanisha kumtoa ila awe serious na kazi yake na apewe IPAD ili awe wa kisasa zaidi ya kukunja makaratasi,sielewi wanafail wapi,hata mavazi yao kiujumla sasa sijui ni picha ndo zinawafanya wasiwe na mvuto?
 
Picha ni mbovu sana badilisheni ziwe za hd waigeni TV E na Clouds tv picha zao zinang'aa, kuacha kuegemea upande mmoja wa chama cha siasa kwa sasa waachieni ch. 10 wafanye kazi hiyo, vipindi ni vibovu sana wengi wetu tunapendelea movie na michezo mbalimbali rejea kipindi cha Jumba la Dhahabu, Channel zenu kupatikana bure kwa dish la ft 8 wakati channel zingine zinapatikana kwa dish ft 6, kushindwa kuhakikisha channel zenu zinaonyeshwa bure kwenye ving'amuzi vyote vya Tanzania.
 
Wameomba ushauri toeni ushauri mimapovu kede kede ya nini sasa.
Bolesheni ubora wa vipindi. Wapelekeni watangazaji kwenye mafunzo hata ya mwezi waendane na hali ya mtazamaji wa sasa.
 
Wameomba ushauri toeni ushauri mimapovu kede kede ya nini sasa.
Bolesheni ubora wa vipindi. Wapelekeni watangazaji kwenye mafunzo hata ya mwezi waendane na hali ya mtazamaji wa sasa.
Mafunzo ya mwezi kivipi? Unaweza fananisha viwango vya elimu vya TBC na chombo chochote nchini? Wao huajiri kujari sana elimu mnaotaka sauti muonekano nendeni TV za mitaani jua hiyo ni ya serikali kamwe haiwezi fanana na binafsi
 
Naam,ubora wa picha si mzuri kuonekana kwenye dish futi 8 hio aina ya satellite watumiayo,hilo la kuonekana ving'amuzi vyote mbona iko hivyo TBC 1na utalii,labda TBC 2 ndio ya kulipia je kisimbuzi gani TBC na utalii si za bure? Au sijakuelewa?
 
Daaa nyie hatakuwashaur hatujui wapi pa kuanzia......... Labda kwanza mungeibadir iyo T iwe Ccm Broadcasting Television CBT. Kifupi mnatuboa saana mpka kutoa ushaur tunaona uvivu
 
Wenzetu Kenya television yao ya taifa wanaonyesha michuano ya afcon wao wanakaz ya kusifia vjna wa Lumumba🤕🤕🤕🤕🤕🤕🤕
 
Mafunzo ya mwezi kivipi? Unaweza fananisha viwango vya elimu vya TBC na chombo chochote nchini? Wao huajiri kujari sana elimu mnaotaka sauti muonekano nendeni TV za mitaani jua hiyo ni ya serikali kamwe haiwezi fanana na binafsi
Kama mtaeshimu michango yetu ili mbadilike nina uwakika mtaboresha TBC. Ikiwa mnajibu kifedhuli kama hivi mjue ilo chombo kitakufa kwa midomo yenu michafu.
Mafunzo ya vitendo kwa vyombo vingine na msione aibu nendeni hata private television mkajifunze kwa kujitolea...
Kusoma sio mpaka muingie darasani..
 
Daaa nyie hatakuwashaur hatujui wapi pa kuanzia......... Labda kwanza mungeibadir iyo T iwe Ccm Broadcasting Television CBT. Kifupi mnatuboa saana mpka kutoa ushaur tunaona uvivu
Haiwezekani ccm wanayo yakwao chanelten,TBC 1 ya serikali toa mapendekezo kipi kifanyike acha kupotosha watu au kupoteza maana ya huu ukurasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…